True story; kifo cha gen. Tewete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

True story; kifo cha gen. Tewete

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Fidel80, Jan 2, 2012.

 1. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #1
  Jan 2, 2012
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Yule binti aliye mchoma kisu gen.mmewe wake wa zamani ambae wamezaa nae watoto wawili walio kuwa wakisomeshwa na gen. Tewete nae yupo jela baada ya kumchoma mwanaume mwingine kisu baada ya kumfumania akila bata na Aisha.

  Ni mwaka wa tatu sasa mme wa Aisha yupo jela na sasa Aisha nae anamfuata mmewe huko huko jela baada ya kumuua gen. Tewete fundi wa madege ya jeshi.

  Watoto watateseka sana baba jela mama nae jela kwa kuchoma visu.

  Source: Masao bwile.
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Jan 2, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  mmmmh! Ngoja nije nisome tena upya.
   
 3. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Hii ni hand-work ya Fidel80 kweli? Hebu ifanye GT material tafadhali, kha!
   
 4. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #4
  Jan 2, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  Like Husband Like Wife
   
 5. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #5
  Jan 2, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Hii story sijaielewa! Labda am missing some link na kitu kilichowahi kutokea
   
 6. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #6
  Jan 2, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  i think im drunk.....
   
 7. Thomas Odera

  Thomas Odera Verified User

  #7
  Jan 2, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 644
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Sijaelewa labda mmleta mada aeleze kwa ufasaha
   
 8. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #8
  Jan 2, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  hujaelewa nini hapo?

  huyu binti mwanzao alikuwana mume...huyo mume akamufaminia aisha akila bata na mwanaume mwingine...huyo mume wa aisha akamchoma kisu huyo jamaa...mume wa aisha akawekwa ndani...aisha akabaki uraian na watoto wawili aliozaa na mumewe aliyeko jela..na sasa hawa watoto walikuwa anasomeshwa na gen....juzi aisha kamuona gen akila bata na rafiki yake nae akafanya kama alivyofanya mume wake miaka 3 iliyopita...akamchoma gen(fundi wa madege y jeshi) kisu...sasa aisha nae anapelewa gerezana na huenda huko akakutana na mume wake wa zamani...umeelewa?
   
 9. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #9
  Jan 2, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Hata mimi pia namiss kitu hapa,labda atuchomekee na link ya thread mama then tutaenda sambamba
   
 10. Leonard Robert

  Leonard Robert JF-Expert Member

  #10
  Jan 2, 2012
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 9,143
  Likes Received: 2,465
  Trophy Points: 280
  rudia! Sijaelewa.
   
 11. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #11
  Jan 2, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,506
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Edson,unafaa kuanzisha chekechea ya great thinkers. Asante.
   
 12. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #12
  Jan 3, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  kabila gani hao watu?
   
 13. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #13
  Jan 3, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,431
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  :hatari:
   
 14. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #14
  Jan 3, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Inaonyesha huyo dada amezoea damu
  Toka alivyo ona damu ya mwanaume mwingine aliye uawa na mmewe
  dah inasikitisha sana, mjane ndo hivyo anazika mauti ya mmewe.
   
 15. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #15
  Jan 3, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Hivi Edson kule jela wanaweza onana kweli?
   
 16. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #16
  Jan 3, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Mwanajeshi aliyeuawa kusafirishwa leo
  [TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]na Lucy Ngowi


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD] MWILI wa marehemu, Meja John Tawete, ambaye ni askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kikosi cha Anga, unatarajiwa kusafirishwa leo kwenda Pongwe, mkoani Tanga kwa mazishi.
  Akizungumza na waandishi wa habari jana nyumbani kwa marehemu eneo la Banana kwenye kambi za jeshi hilo Kikosi cha Anga, mtoto wa pili wa Meja huyo, Sunday Tawete, alisema kuwa mwili wa baba yake utasafirishwa.
  Mtoto huyo wa marehemu, akisimulia kifo cha baba yake alisema kuwa siku hiyo, alionana naye mchana majira ya saa tisa alasiri wakati alipompelekea vyeti vyake vya kuzaliwa eneo analofanyia kazi katika ‘super market' ya jeshi.
  "Ilipofika saa sita usiku nikawa nampigia baba simu yake ya kiganjani kwa ajili ya kumtakia heri ya mwaka mpya lakini sikumpata, saa saba nilirudia tena hali ikawa hivyo hivyo hadi ilipofika asubuhi tulipopata taarifa hizi," alisema.
  Tawete alisema, mama yao aliondoka wiki moja iliyopita na kwenda mkoani Kilimanjaro kwa dada yao Mariamu ambaye ni ofisa magereza, kwa ajili ya matibabu kwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya kupooza mkono na mguu.
  Hata hivyo alisema kuwa dada yake huyo na mama wangewasili jana kwa ajili ya kuungana na familia kwenye msiba huo.
  Marehemu huyo alifariki baada ya kuchomwa kisu tumboni na mgongoni na mpenzi wake aliyemkuta marehemu akiwa na mwanamke mwingine.
  Meja huyo inasemekana alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Saada Musa (30) na Aisha Ally (27) ambao ni wahudumu wa kampuni ya utoaji wa huduma ya vyakula ya Nice inayohudumia kikosini hapo.
  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Faustine Shilogile, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi hilo kwa upelelezi zaidi.

  Mwanajeshi aliyeuawa kusafirishwa leo

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 17. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #17
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,445
  Likes Received: 5,833
  Trophy Points: 280
  Ni meja na sio jenerali
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Jan 3, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,546
  Likes Received: 18,203
  Trophy Points: 280
  Fidel80 ni kweli umepost thread ambayo haiko straight kueleweka kwa urahisi, ndio maana tufike mahali tukubali, kazi ya kutoa habari nayo ni kazi ya watu!

  Issue yenyewe ni simple tuu na iko hivi.

  Mwanamke mmoja aitwa Aisha ambae ameolewa na kubahatika kupata watoto wawili na mumewe. Miaka mitatu iliyopita, mumewe na Aisha alimfumania mkewe (Aisha), hivyo kumchoma kisu mgoni wake, kitendo kilichompeleka jela mpaka sasa bado yuko jela akitumikia kifungo cha miaka mitatu.

  Wakati mume wa Aisha akiwa jela, ndipo Aisha akapata mwanamume mwingine msamaria, aliyekubali kuwa mpenzi wake, na kukubali kuwasomesha wale watoto wawili wa Aisha, ambao baba yao yuko jela!. Mpenzi huyo wa sasa wa Aisha ndio huyu Mjeshi, Gen. Tawete!.

  Aisha nae, alimfumania Gen. Tawete na mwanamke mwingine, hivyo akamchoma kisu kilichomuua Gen. Tawete, hali iliyopelekea Aisha kupelekwa gerezani, ambako hatimaye atahukumiwa kifungo na huko kifungoni atakutana na mumewe ambaye ndie baba watoto wake!.

  Mtoa mada akasisitiza sasa watakao teseka ni watoto, kwani baba yao alipokwenda jela, msamaria Gen. Tawete, ndiye aliyemtunza mama yao, kuwatunza wao na kuwalipia ada, lakini sasa mama yao, amemuua huyu msamaria hivyo sasa hawana msaada wowote, kwasababu baba yuko jela, mama yuko jela msamaria ndio huyo kauwawa, hivyop kwao ni mateso mara 3!.

  My Take.
  Hii ni story ya kusikitisha na kuhuzunisha, kwanza kwa Generali wa jeshi kuuliwa kwa kisu kama kujinja kuku na sio tuu kuuliwa kwa kisu tuu bali muuaji mwenyewe ni mwanamke!, hiki ni kifo cha aibu, achilia mbali aibu ya General kufia kwa kimada, wakati yeye ni mtu wa heshima zake na hadhi ya juu kabisa katika jamii!.

  Pili huyo Mwanamke Aisha, japo kwanza atafunguliwa shitaka la mauaji, akipata wakili mahiri, shitaka hilo litageuzwa kutoka murder (kukua kwa kukusudia) mpaka manslaughter (kuua bila kukusudia) na wakili huyo akiitumia vizuri defence ya 'provocation' na akawatumia madaktari bingwa wa afya ya akili, kuthibitisha hiyo 'provocation' ilifikia kiwango cha kusababisha 'insanity', na kuprove beyond reasonable doubt kuwa wakati anamchoma kisu, she was insane!, huyo mama ataachiliwa kwa compassion ya kuwenda kuwalea watoto wake wanaomtegemea maana na baba yao yuko jela!
   
 19. MwafrikaHalisi

  MwafrikaHalisi JF-Expert Member

  #19
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 1,746
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wafungwa ME na KE waonane gerezani? Never heard before.
   
 20. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #20
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,445
  Likes Received: 5,833
  Trophy Points: 280
  Wataonana lakini hawata conjugate
   
Loading...