David ngayanimo
Member
- Nov 8, 2018
- 19
- 20
Kisa cha Ibrah Da Huster Kwenye Jukwaa la Miaka 30 ya Bongo Fleva
Katika maadhimisho ya Miaka 30 ya Bongo Fleva yaliyofanyika Rock City Mall jijini Mwanza, kundi la Nako 2 Nako lilipata nafasi ya kupanda jukwaani na kuwakumbusha mashabiki baadhi ya nyimbo zao za zamani. Kundi hilo lilikuwa miongoni mwa makundi yaliyowahi kuwa sehemu ya historia ya Hip Hop Tanzania, likiwa na wasanii kama Bu Nako, G Nako, Lord Eyes na Ibrah Da Huster.
Hata hivyo, performance hiyo iliacha maswali, hasa kuhusu namna Ibrah Da Huster alichofanyiwa kila wakati akipotaka kuperform verse zake. Kwa mujibu wa simulizi ya tukio hilo, Nako 2 Nako walifanya takribani nyimbo tatu siku hiyo, lakini ilipofika sehemu ya Verse za msanii Ibrah Da Huster , mic yake ilizimwa na Dj nakupelekea msanii huyo kushindwa kupaform verse zake katika nyimbo takribani 3 walizopata fursa ya kuparform kama kundi na wezake G nako na Lord eyez.
Kwa upande wa wasanii Lord Eyes na G Nako wao wawili waliweza kuperform verse zao zote kikamilifu . Baada ya nyimbo za Nako 2 Nako kustop na DJ kuanza kucheza nyimbo za kundi lingine lililojulikana kama Weusi kampuni , Lord Eyes na G Nako waliendelea kubaki jukwaani na kufanya performance kwa sababu wakati huo walikuwa pia sehemu ya kundi hilo.
Kwa upande wa Ibrah Da Huster, hali hiyo ilijirudia kwenye nyimbo kadhaa, na hatimaye inadaiwa kwamba msanii huyo alikata tamaa na kuamua kukaa pembeni ya jukwaa. Tukio hilo linaweza kuonekana kama jambo dogo kwa mtu aliyekuwa akitazama tamasha kwa mbali, lakini kwa msanii aliyepanda jukwaani kuwakilisha historia yake, kukosa nafasi ya kusikika kwenye verse yake kunaweza kuibua maswali kuhusu namna ya mapokeo yake kwa dj & Emcee usiku huo wa tukio la miaka 30 ya Bongo Fleva Mwanza.
Jambo la muhimu hapa si kuwashutumu Lord Eyes au G Nako, kwa sababu wao waliendelea kufanya kile walichopewa nafasi ya kufanya. Hoja kubwa ni kwa nini Ibrah Da Huster hakupata nafasi sawa ya kuperform verse zake, wakati alikuwa sehemu ya historia ya kundi lab Nako 2 Nako.
Zaidi ya Ibrah, suala hili pia linafungua mjadala mpana kuhusu wasanii wengine wa zamani walioalikwa kwenye maadhimisho hayo miaka 30 ya Bongo fleva jijini Dar es Salaam & Mwanza kuna Baadhi yao waliopewa nafasi ya kuperform wimbo mmoja au miwili, wakati wasanii wengine wa zamani wenye majina makubwa walipewa nafasi ya kufanya performance ya nyimbo zaidi ya mmoja.
Hapa ndipo swali la usawa linapoingia. Kama lengo lilikuwa kuadhimisha Miaka 30 ya Bongo Fleva, je, nafasi za kiuchumi & majina makubwa nk. Je? Yalipaswa kuangaliwa zaidi kwa ukubwa wa namna hiyo au jina la msanii na muonekano wake kwa sasa, au mchango wake katika historia ya muziki?
Kwa sababu kuna wasanii ambao huenda majina yao hayana nguvu sokon kwa sasa kama zamani, lakini walikuwa ni sehemu muhimu ya Historia yabBongo Fleva. Kuwapa nafasi ndogo kwa sababu tu hawana majina makubwa kwa sasa kunaweza kufanya baadhi ya vipande vya historia visisikike ipasavyo.
Kwa Ibrah Da Huster, suala hili lina uzito zaidi kwa sababu alipanda jukwaani akiwa sehemu ya kundi la Nako 2 Nako, kundi ambalo lilikuwa sehemu ya historia ya Hip Hop Tanzania. Hivyo, alistahili kupewa nafasi ya kuperform verse zake kama walivyopewa wasanii wezake G nako na lord eyez .
Na uwezo wake wa kiuandishi unaonekana wazi kupitia verse yak katika wimbo huu unaojulikana kama hawatuwezi.. by nako 2 nako
«Sambo na thoughts, loss /
That's man of experience /
Flow hili reverend kwa frequency, draw /
Ni kama Runda na defence /
Ona difference ya illness na fakeness /
Kick na snare, na evidence /
Na-spit sense, future participle tense /
Collabo la 50 Cent /
Fake MCs wana-spit nonsense /
Hawa make sense, hii kwao ni rough sentence /
Nawaua mi kila sentence /
Hence, nakanyaga clutch /
Na-change gear na pace /
Ka ace, hence mpaka classic /
Sht World Cup, park ya Jurassic /
Wasanii mnaleta traffic /
Siwaafiki, nyie wanafiki /
Nawameza ka meli ya Atlantic /
Need a hustler, niko maabara /
Trap star, Viagra, muadhara /»
Verse hii inaonyesha aina ya uandishi wa Hip Hop uliokuwa ukitumia wordplay, rhyme, punchlines na mchanganyiko wa Kiswahili na Kiingereza. Kwa hiyo, nafasi yake kwenye jukwaa haikuwa tu kuhusu kuimba; ilikuwa pia ni nafasi ya kuwakumbusha mashabiki sehemu aliyokuwa nayo katika historia ya muziki.
Kwa hiyo, hoja hapa si kwamba Lord Eyes au G Nako hawakupaswa kuperform. Walikuwa sehemu ya historia ya Nako 2 Nako na pia walikuwa sehemu ya kundi la Weus kampuni hivyo walipoanza nyimbo za Weusi kampuni wao waliendelea na performance.
Hoja ni kwamba Ibrah Da Huster naye alistahili kupewa nafasi yake kama walivyopata wenzake.
Na zaidi ya Ibrah, hii iwe changamoto kwa waandaaji wa matukio kama haya: unaposema unasherehekea miaka 30 ya muziki, usiangalie tu majina ambayo bado yana nguvu leo. Wakumbuke pia wale waliowahi kujenga msingi wa muziki huo.
Miaka 30 ya Bongo Fleva inapaswa kuwa sherehe ya historia nzima, si ya majina machache pekee.
Swali la mwisho linabaki:
Kwa nini verse za Lord Eyes na G Nako zilisikika, lakini verse ya Ibrah Da Huster ikakatwa, wakati wote walikuwa sehemu ya historia ya Nako 2 Nako?
Ukwaju wa kitambo
0767 542 202