Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 22,690
- 29,909
Tumewekewa ndimu na kachumbari njiani ili tusiendelee kuhoji mkataba mbovu baina ya JMT na Dubai Port World.
Pamoja na kwamba serikali kupitia mamlaka na mihimili yake wamefunga ndoa ya kufilisi na kujimilikisha binafsi rasilimali kuu za uchumi wetu, lakini mhimili moja (Mahakama) umesema wao wamefungwa mikono na wanakiri Dubai PW siyo nchi hivyo nao badala ya kutafsiri kuwa mkataba ule unakksa merits za IGA wao wakatoa baraka uendelee....
Serikali imejipanga kuanza utekelezaji wa Mkataba kuanzia Novemba mwaka huu. Hivyo tutegememee mapicha picha ya kutosha pale bandarini kutuaminisha kuwa kila jambo litafanyika kwa faida yetu bali ukweli ni kwamba Mwekezaji siyo manamba, hivyo hawezi kutunufaisha sisi kwanza kabla yeye hajanufaika.
Pia kwenye mkataba huu mwovu imeelezea wazi kabisa kuna shughuli ambazo JMT inapaswa kufanya kama hatua za awali kuweka mazingira wezeshi ndo maanantunaona kuna kandarasi zimetangazwa, na viwanda vya uongo vinaendelea kuzalisha maneno kuwa hakuna bandari iliyouzwa.
Ingawa kwenye mkataba, hakuna mahala ambapo mwekezaji anawabijika na gharama za uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanyika wa kusimika mitambo kulikoanzwa na awamu ya tano. Waliosaini mkataba na walioupitisha kwa kishindo hawana uchungu na fedha za mkopo ambazo zitageuka mwiba kwetu kwa kulipa deni kubwa bila hata majaribio ya uwekezaji huo hayajafanyika.
Kupitja hizi trends, inawezekana kabisa hata huu mkwamo unaoendelea kwenye umeme na mafuta ni staged ili kutuondoa kwenye reli ya kuhoji ikiwezekana kuwawajibisha wahusika wa mtego huu muovu wa kugenisha bandari zetu. Kuna teuzi za bandika bandua zimefanyika ambapo unaona kabisa lengo ni kutengeneza headlines. Na kupitia hizo headlines tunawekwa bize kujadili trends badala ya msingi wa ule mkataba wa hovyo.
Rai yangu wa serikali. Kama inajiona ni kikundi cha indomitables basi wafanye kila wanalotaka kulifanya lakini zama hizi hazitakuwa za kale pale ambapo Watanzania wenyewe watajiona siyo dhalili tena kupitia sanduku la Kura ama njia zingine halali kuwawajibisha wote wanaojipa umungu mtu ktk Taifa letu.
Mengi nilishayasema na yametokea kwa haraka mno. Lakini yanakuja ambayo yalishaanza kuja. Majira na muda ni nyenzo tu kama ilivyo kwa mtoto anayekua.
Chuki inakua. Hofu inaelekea kudumaa. Uthubutu umeshapandwa na utakua.
Mkataba wa bandari ni mwiba na utaendelea kulichoma taifa.