Trend Setting: Mapendekezo ya JF kwa mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yanayotarajiwa hivi karibuni

Nyie mnaowaza mama Anna wa ACT wazalendo hamfuatilii mambo ya siasa vizuri. Jamaa akiwa Zanzaibar alimshangaa Shein kuteua wapinzani ndani ya serikali yake wakati amepata zaidi ya 90% ya kura. alimalizia kwa kusema kwamba licha ya yeye kupata 58% ya kura zote hawezi kumteua mpinzani ndani ya serikali yake. Mmesahau? Hata wewe Paskal wa habari za uchunguzi umesahau?
 
Wanabodi,
Trend Setting ni kutengeneza mwelekeo au ku shape jambo linalokuja kutokea. Trend Setters ni wale watu ambao wakifanya jambo fulani, sehemu kubwa ya jamii hulifuata.

JF ni trend setter, baadhi ya mapendekezo yanayotolewa humu JF, serikali yetu sikivu huyatekeleza.

Baada ya zoezi la Uchaguzi Mkuu kukamilika, JF ilitengeneza trend ya Baraza jipya la Mawaziri na mimi naamini baadhi ya wateule kama Joyce Ndalichako was made from JF.Mapendekezo ya wananchi: Muundo wa Baraza la Mawaziri kwa Serikali ya Awamu ya Tano

Kufuatia teuzi za baadhi ya wabunge wapya kwenye Bunge la Muungano, Trend reading zinaelekeza kufanyika kwa mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri hivi karibuni huku sura mpya kama
Prof. Palamagamba Kabudi, Anne Kilango Malecela na Salma Kikwete wakitarajiwa kuwemo.

Japo kwa mujibu wa katiba yetu kazi ya kuteua mawaziri ni kazi ya rais wa JMT kwa mashauriano na Makamo wa Rais na Waziri Mkuu, viongozi wetu hawa nao ni binaadamu na wanaweza kukosea katika uteuzi au kuna watu wazuri tuu lakini jicho la rais haliwezi kuwaona ila jicho la JF ni kubwa.

Ni ukweli usiofichika kuwa kwenye Baraza hili kuna mawaziri ambao kweli ni ma performers wengine beyond expectations, kuna mawaziri non performers yaani wapo wapo tuu ili mradi wapo na kuna mawaziri kiukweli kabisa wame flop, hawa ni mawaziri mizigo, they should go.

Pia kwenye wabunge kuna wabunge ambao ni great potentials kumsaidia rais kuliko kuendelea kubeba mizigo hadi 2020.

Hivyo wana JF, hakuna ubaya kumshauri rais wetu, ambaye ni mtumishi wetu, sisi ndio waajiri wake kupitia kura zetu na ndio tunaomlipa mshahara wake kupitia kodi zetu, hivyo atazingatia maoni na ushauri wetu kwa jinsi ile ile anavyozihitaji kura zetu.

Nikianzia na maoni yangu.
1. First and Foremost anza na huyu kijana mpendwa wako, unayependezwa naye, ambaye japo sii Waziri na sii mbunge bali alikuwa ni zaidi ya Makamo wa Rais, ni zaidi ya Waziri Mkuu, ni zaidi ya Spika, ni zaidi ya Jaji Mkuu, ni zaidi ya IGP. Kijana shupavu, shujaa, hodari, mchapakazi Paul Makonda, he was an asset like a jewel on the sea, a very big asset na ni kweli amefanya makubwa katika kipindi kifupi, but its very unfortunately he has now turned into the biggest liability you have!, deal with it first, the sooner the better!.
2. Asante kututeulia wabunge wanawake 4. Bado mmoja, huyu mmoja. Kwa uteuzi wako mmoja wa mwisho uliobakia kwa mujibu wa katiba, ambaye lazima uwe wa mwanamke, tunakuomba ututeulie mwanamke kutokea upinzani, preferably Mama Ana Mngirwa. Mkapa aliteua kutoka upinzani, Kikwete aliteua kutoka upinzani, why not you?. Japo hakuna sheria, kanuni wala taratibu inayokulazimisha umteue nani, lakini unapokuwa ni rais wa wote kuna vitu lazima uvifanye kuwaonyesha watu kuwa wewe ni rais wa wote, na huo uwote wako uonekane kwa wote, kama ilivyo kwenye kutoa haki, "justice must not be only done,but it must be seen to be done" kuwa haki sio lazima tuu itendeke, bali pia lazima ionekane kutendeka, hata kama huupendi vipi upinzani, hata kama huwapendi vipi wapinzani, ni watu ambao wapo kisheria kwa mujibu wa katiba japo kazi yao kubwa ni kukusoa wewe na serikali yako lakini amini usiamini ni watu wa muhimu sana kwako, kwa serikali yako na kwa taifa kwa ujumla tena wanakusaidia sana tuu hata kama hujui.
3.Kwa vile umeisha teua wanawake wengine wawili, katika mabadiliko madogo utakayo yafanya this time naamini yataakisi gender mainstreaming kwenye mabadiliko ya baraza lako. Pale mwanzo umetutelia mawaziri wanawake wanne tuu na hatukulaumu kwa hilo kwa sababu waelewa tunaelewa sababu, haupaswi kuziendeleza hizo sababu, kama rais wa nchi kuna vitu lazima ubadilike.
Tuacheni Kumlaumu Rais Kuteua Wanaume, TZ Hatuna Wanawake Wenye Sifa na Vigezo vya Kuteuliwa!

Sasa wana JF wenzangu, naomba tutoe maoni yetu nani abaki na nani atoke. Nani ameflop na hamsaidii tena rais. Pia kuangazia potentials zilizopo kama tulivyo muangazia Pro. Ndalichako na hatimaye akawepo.

Naomba kuwasilisha.
Paskali

KAKA SHIDA YAKO WEWE HUSHIKILII KITU KIMOJA. HAPA MI NIMEKUELEWA SANA.
 
Wanabodi,
Trend Setting ni kutengeneza mwelekeo au ku shape jambo linalokuja kutokea. Trend Setters ni wale watu ambao wakifanya jambo fulani, sehemu kubwa ya jamii hulifuata.

Nikianzia na maoni yangu.
1. First and Foremost anza na huyu kijana mpendwa wako, unayependezwa naye, ambaye japo sii Waziri na sii mbunge bali alikuwa ni zaidi ya Makamo wa Rais, ni zaidi ya Waziri Mkuu, ni zaidi ya Spika, ni zaidi ya Jaji Mkuu, ni zaidi ya IGP. Kijana shupavu, shujaa, hodari, mchapakazi Paul Makonda, he was an asset like a jewel on the sea, a very big asset na ni kweli amefanya makubwa katika kipindi kifupi, but its very unfortunately he has now turned into the biggest liability you have!, deal with it first, the sooner the better!.

Naomba kuwasilisha.
Paskali
Sitaki kusoma zaidi ya hapo
 
Japo sipingi wazo lako lakini kipaombele chetu kwa sasa ni hali ya uchumi. Kwa ujumla uchumi unadorora huku tukilishwa ahadi za matumaini kama awamu zilizopita. Sifa tunazoziona ni kushikishana adabu tena kwa utashi wa viongozi. Kwa ujumla uteuzi wa mawaziri sioni ukileta tija zaidi ya faida binafsi za mteuliwa. Sitarajii hilo baraza jipya kuja na ule utoto ulioanza nao awamu hii ya kwenda kufungia mageti wachelewaji mbele ya camera. Pia ni vizuri mngetuambia mafanikio na mapungufu ya baraza hili na sio kutuletea sura mpya lakini matokeo ni hayohayo ya mawaziri kusema kutekeleza nia njema ya rais wetu.
...sijui itakuja kuwekwa wazi huko mbeleni juu ya kauli ya Mahakama ya Rufaa na udhaifu wa wanasheria waliokimbilia kushinikiza mazuio ya dhamana ya Mh. Lema. Kwamba walifanya vile kwa kutokujua sheria au kutimiza matakwa ya waliowatuma. Na je, na hii itakuwa na athari gani pale watu waliokula viapo kulinda sheria zilizoandikwa kuamua kuzibwaga na kufuata sheria za kuelekezwa kwa mdomo.
Wanaoniona nimetoka kwenye hoja wanisamehe hapa tafadhali!
 
katika yote kumteua mama mngirwa naona umewaza mbali sana yule mama ana uwezo Mkubwa na ni mtulivu kujenga hoja

pia ni mtulivu ana uwezo Wa kufanya tafakari tunduizi
His excellent Mhe rais tunaomba umuone huyu mama
Hayo ndiyo yatakayofanya asiteuliwe maana mkuu hataki wajuvi sana.
 
Mawaziri wafuatao wawekwe pembeni kwani morali wao umekata:-
Mahiga ( Sera zake hazifanyi kazi kwa Jpm maana hajui masuala ya Diplomasia)

January(hawaelewani na Naibu wake )

Waziri wa Viwanda( Huyu mpaka muda huu hajui anafanya nini na anaelekea wapi)

Nape (Morali umekata kwa sababu anaona Chama kinavurugwa badala ya kujengwa,kumbuka huyu kakulia na kulelewa kichama ni kada mahiri)

Naibu Waziri wa Maji( huyu ni mpiga kelele tu hajui hata majukumu yake)

Maghembe aka Faru John( huyu pumzi imekata)
Nadhan nimekuelewa sana point hizi 3, 4&6
.
.
.
Kyenekyaka mkighanile une
 
Kwa maoni yangu:
  • Anna Mghwira apewe Ubunge wa JMT.
  • Makamba aende Mambo ya Nje.
  • Mahiga aende Muungano - mtaalamu wa kutatua migogoro.
  • Bashe apewe Viwanda,Biashara na Uwekezaji.
  • Mwijage atoke.
  • Prof. Maghembe atoke.
  • Dk. Mwakyembe atoke.
  • Stanslaus Mabula apewe TAMISEMI.
  • Mwigulu aende Wizara ya Fedha.
  • Simbachawene aende Mambo ya Ndani.
  • Angelina Mabula awe Waziri kamili wa Ardhi - amemsoma vizuri Waziri wake.
  • Lukuvi apewe Maliasili na Utalii - amefanya kazi nzuri Ardhi.
 
Mawaziri wafuatao wawekwe pembeni kwani morali wao umekata:-
Mahiga ( Sera zake hazifanyi kazi kwa Jpm maana hajui masuala ya Diplomasia)

January(hawaelewani na Naibu wake )

Waziri wa Viwanda( Huyu mpaka muda huu hajui anafanya nini na anaelekea wapi)

Nape (Morali umekata kwa sababu anaona Chama kinavurugwa badala ya kujengwa,kumbuka huyu kakulia na kulelewa kichama ni kada mahiri)

Naibu Waziri wa Maji( huyu ni mpiga kelele tu hajui hata majukumu yake)

Maghembe aka Faru John( huyu pumzi imekata)

Mkuu, sasa kama Waziri haelewani na Naibu wake, kwa nini unamwondoa Waziri???? hujatwambia sababu... Lkn ni kweli hawaelewani??????
 
Bashe bora abak mbunge aendelee kuichagiza serikal maana uko hawez kutumbuka akiwa wazir mkuu tutarijie bashe tofaut au utumbuz yakinifu umuandame
 
Kwa maoni yangu:
  • Anna Mghwira apewe Ubunge wa JMT.
  • Makamba aende Mambo ya Nje.
  • Mahiga aende Muungano - mtaalamu wa kutatua migogoro.
  • Bashe apewe Viwanda,Biashara na Uwekezaji.
  • Mwijage atoke.
  • Prof. Maghembe atoke.
  • Dk. Mwakyembe atoke.
  • Stanslaus Mabula apewe TAMISEMI.
  • Mwigulu aende Wizara ya Fedha.
  • Simbachawene aende Mambo ya Ndani.
  • Angelina Mabula awe Waziri kamili wa Ardhi - amemsoma vizuri Waziri wake.
  • Lukuvi apewe Maliasili na Utalii - amefanya kazi nzuri Ardhi.
Mkuu Mungo Park, thanks for this very objective.

Paskali
 
Back
Top Bottom