Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,647
- 119,254
Wanabodi,
Trend Setting ni kutengeneza mwelekeo au ku shape jambo linalokuja kutokea. Trend Setters ni wale watu ambao wakifanya jambo fulani, sehemu kubwa ya jamii hulifuata.
JF ni trend setter, baadhi ya mapendekezo yanayotolewa humu JF, serikali yetu sikivu huyatekeleza.
Baada ya zoezi la Uchaguzi Mkuu kukamilika, JF ilitengeneza trend ya Baraza jipya la Mawaziri na mimi naamini baadhi ya wateule kama Joyce Ndalichako was made from JF: Mapendekezo ya wananchi: Muundo wa Baraza la Mawaziri kwa Serikali ya Awamu ya Tano.
Kufuatia teuzi za baadhi ya wabunge wapya kwenye Bunge la Muungano, Trend reading zinaelekeza kufanyika kwa mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri hivi karibuni huku sura mpya kama Prof. Palamagamba Kabudi, Anne Kilango Malecela na Salma Kikwete wakitarajiwa kuwemo.
Japo kwa mujibu wa katiba yetu kazi ya kuteua mawaziri ni kazi ya rais wa JMT kwa mashauriano na Makamo wa Rais na Waziri Mkuu, viongozi wetu hawa nao ni binaadamu na wanaweza kukosea katika uteuzi au kuna watu wazuri tuu lakini jicho la rais haliwezi kuwaona ila jicho la JF ni kubwa.
Ni ukweli usiofichika kuwa kwenye Baraza hili kuna mawaziri ambao kweli ni ma performers wengine beyond expectations, kuna mawaziri non performers yaani wapo wapo tuu ili mradi wapo na kuna mawaziri kiukweli kabisa wame flop, hawa ni mawaziri mizigo, they should go.
Pia kwenye wabunge kuna wabunge ambao ni great potentials kumsaidia rais kuliko kuendelea kubeba mizigo hadi 2020.
Hivyo wana JF, hakuna ubaya kumshauri rais wetu, ambaye ni mtumishi wetu, sisi ndio waajiri wake kupitia kura zetu na ndio tunaomlipa mshahara wake kupitia kodi zetu, hivyo atazingatia maoni na ushauri wetu kwa jinsi ile ile anavyozihitaji kura zetu.
Nikianzia na maoni yangu;
1. First and Foremost anza na huyu kijana mpendwa wako, unayependezwa naye, ambaye japo sii Waziri na sii mbunge bali alikuwa ni zaidi ya Makamo wa Rais, ni zaidi ya Waziri Mkuu, ni zaidi ya Spika, ni zaidi ya Jaji Mkuu, ni zaidi ya IGP. Kijana shupavu, shujaa, hodari, mchapakazi Paul Makonda, he was an asset like a jewel on the sea, a very big asset na ni kweli amefanya makubwa katika kipindi kifupi, but its very unfortunately he has now turned into the biggest liability you have!, deal with it first, the sooner the better!.
2. Asante kututeulia wabunge wanawake 4. Bado mmoja, huyu mmoja. Kwa uteuzi wako mmoja wa mwisho uliobakia kwa mujibu wa katiba, ambaye lazima uwe wa mwanamke, tunakuomba ututeulie mwanamke kutokea upinzani, preferably Mama Ana Mngirwa.
Mkapa aliteua kutoka upinzani, Kikwete aliteua kutoka upinzani, why not you?. Japo hakuna sheria, kanuni wala taratibu inayokulazimisha umteue nani, lakini unapokuwa ni rais wa wote kuna vitu lazima uvifanye kuwaonyesha watu kuwa wewe ni rais wa wote, na huo uwote wako uonekane kwa wote, kama ilivyo kwenye kutoa haki, "justice must not be only done,but it must be seen to be done" kuwa haki sio lazima tuu itendeke, bali pia lazima ionekane kutendeka, hata kama huupendi vipi upinzani, hata kama huwapendi vipi wapinzani, ni watu ambao wapo kisheria kwa mujibu wa katiba japo kazi yao kubwa ni kukusoa wewe na serikali yako lakini amini usiamini ni watu wa muhimu sana kwako, kwa serikali yako na kwa taifa kwa ujumla tena wanakusaidia sana tuu hata kama hujui.
3. Kwa vile umeisha teua wanawake wengine wawili, katika mabadiliko madogo utakayoyafanya this time naamini yataakisi gender mainstreaming kwenye mabadiliko ya baraza lako. Pale mwanzo umetutelia mawaziri wanawake wanne tuu na hatukulaumu kwa hilo kwa sababu waelewa tunaelewa sababu, haupaswi kuziendeleza hizo sababu, kama rais wa nchi kuna vitu lazima ubadilike: Tuacheni Kumlaumu Rais Kuteua Wanaume, TZ Hatuna Wanawake Wenye Sifa na Vigezo vya Kuteuliwa!
4. Kwa maoni yangu, Kabudi mpe wizara ya Sheria, atakusaidia sana. Mwakyembe kwa vile kabla hajawa mwanasheria, alikuwa mwana habari, na ni mtu very sensational, mpe wizara ya habari, ila ivunje, ondoa michezo na utamaduni, mwache Nape.
Japo Prof. Maghembe umempa ili tuu usionekane umewabagua Wachagga, kwanza Mpare sio Mchagga, pili kiukweli huyu ni mzigo, alikuwa mzigo tangu kwa Kikwete, nahadi sasa ni mzigo. Maliasili na utalii inahitaji mawaziri vijana, damu chemka na smart, sio tuu smart kichwani, bali hata anavyoonekana, usione aibu kumrudisha Nyalandu, au tafuta smart lady or gentlemen smart kichwani but she must look attractive atuvutie watalii, kama ni mwanaume then awe HB, watu hawa bungeni unao.
Prof. Mpango japo ni mchumi mzuri, lakini hana uwezo wa kukusaidia, uless kama unachobabaikia ni huo uprofesa wake lakini hakuna kitu. Wizara ya fedha tafuta mtu anaijua pesa. Kwenye mabadiliko yako, achana na kasumba za Kisukuma za kutothamini wanawake!, ongeza idadi ya wanawake na watu kama Bashe, watakusaidia sana, watumie. na kuna wizara umeziunganisha ili uonekane umetengeneza baraza dogo, lakini muunganiko huo doesn't make any sense at all!. Muda huu umeishatosha kukuonyesha baadhi ya hizo wizara hazina tija na wastage of money and resources. Hili nililisema hapa.
Mnatambua kuwa baadhi ya Maamuzi ya Magufuli yanaligharimu Taifa ...
Sasa wana JF wenzangu, naomba tutoe maoni yetu nani ame perform anastahili kubaki, au alikuwa naibu anastahili kuwa waziri kamili, nani ameflop na hamsaidii tena rais hivyo apumzishwe. Pia kuangazia potentials zilizopo kama tulivyo muangazia Pro. Ndalichako na hatimaye akawepo.
Naomba kuwasilisha.
Paskali