Trafiki wa kike atekwa akiwa barabarani

Trafiki wa kike atekwa akiwa barabarani

Huyo askari ana makosa na waache kumtetea, haiwezekani akubali kuendeshwa na mtu asiye na leseni na kama alikubali kuendeshwa na mtu asiye na leseni that means hakukuwa na kosa kwa dereva huyo kuendesha gari hio bila leseni maana hata msimamizi wa sheria "polisi" naye alitumia gari hio hio na ikiendeshwa na mtu huyo huyo asiyekuwa na leseni!!!!!

Huwa siwaelewi hawa jamaa zangu ila kwakua najua wana njaa sana hua namalizana nao kimtindo ila kama nikuamua kukomaa mtu unawashinda kirahisi sana.
MANI
 
Last edited by a moderator:
usukumani wanaita chagulaga unachukua unaweka begani halafu unatuma wazee wanaenda kwa wazazi but in this case jamaa alikuwa hana nia ya kuteka coz afande kaingia mwenyewe garini bila kulazimishwa na inawezekana jamaa alikuwa hajui kituo cha polisi kilipo akawa anaweweseka mitaani na tatu angekuwa hana leseni angeshitakiwa pia kwa kosa hilo it seems leseni alikuwa nayo chezea kubambikiza kesi na ukute trafik anapigwa na bosi basi nae anakuwa bosi

kituo cha polisi anachokifahamu kipo Ubungo ndio maana akaja hadi huku, na trafki alifurahia utamu wa siti akajisahau kuelekeza njia
 
mm huwa wakinikamata namwambia niandikie hapa hapa, na receipt nipe, hataki naondoka. polisi yeyote hapandi gar yangu
 
huyo askari alikuwa hana haki ya kufungua mlango na kupanda hilo gari.

polisi wajanja wameipeleka kesi mahakama ya mwanzo coz wanajua kesi zote ziendazo mahakama ya wilaya mpaka mahakama kuu lazima wanasheria wa serikali wajiridhishe kama kuna uwezekano wa mtuhumiwa kupata kesi ya kujibu otherwise hawafungui kesi
 
Hii kesi ni nyepesi sana.
Hakuna utekaji hapo sana sana mshitakiwa atatiwa hatiani kwa kukataa kutii amri ya polisi basi.

Mtekaji gani anamwachia mateka awasiliane na radio!

haya ndiyo matatizo ya kukurupuka kwa prosecution katika nchi yetu. kuthibitisha hilo shtaka itawapa tabu sana
 
haya ndiyo matatizo ya kukurupuka kwa prosecution katika nchi yetu. kuthibitisha hilo shtaka itawapa tabu sana

Kwanza sheria inasema sio lazima dereva aonyeshe leseni yake hapo hapo atakapoombwa na trafiki polisi.

Inawezekana kutokana na haraka alizonazo dereva aliisahau nyumbani au sehemu yeyote hivyo alikuwa na haki ya kupewa muda ndani ya masaa 24 aiwasilishe kituo cha palisi.

Sasa huyo askari kukomaa mpaka kudandia gari ya mtuhumiwa ni kimbele mbele chake.

jamaa kama ana mwanasheria mzuri anaweza akamfukuzisha kazi huyo askari.
 
Alexander Msowoya (35), ambaye ni mkazi wa Chang’ombe, jijini Dar es Salaam, amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Magomeni akikabiliwa na shtaka la kumteka nyara askari wa kike wa usalama barabarani.

Hati ya mashtaka iliyosomwa mbele ya hakimu Mwanaidi Ngoda ilidai kuwa Julai 11, mwaka huu, saa 9:00 alasiri, eneo la kati ya Temeke na Chang’ombe, mshtakiwa alimteka nyara askari polisi Konstebo Ester, alipotakiwa kuonyesha leseni yake.

Hivi msamiati wa kuteka umekaaje kisheria?

Ilidaiwa kuwa Afande Ester alimkamata mshtakiwa huyo akiwa anaendesha gari lenye namba za usajili T 495 BKJ na kumtaka aonyeshe leseni yake, lakini hakufanya hivyo.

Baada ya hapo, ikadaiwa kuwa trafiki huyo wa kike akamwamuru dereva huyo aliyekuwa anaendesha gari aina ya Rav4 ya rangi ya bluu kuweka gari lake pembeni, lakini alikaidi kwa kudai ana haraka.

Kutokana na hali hiyo, ilidaiwa kuwa askari aliingia ndani ya gari kwa kupitia kwenye mlango wa nyuma na kuamuru waende kwenye kituo cha polisi Chang’ombe.

Hii imekaaje kisheria?
Ni kweli kuwa askari kunatosha kujiingiza ndani ya gari ya Mtu bila ridhaa yake?
Je huu ndiyo aina ya ukamataji unaotambuliwa na Sheria?
Wanasheria ebu njooni mdadavue hii kitu ili kuwe na uelewa katika Jamii.
na hasa Madereva.

Hata hivyo, ilidaiwa kuwa badala ya kuelekea alikoelekezwa, mshtakiwa alianza kwenda anakokujua yeye, hivyo kukiuka amri halali ya polisi na kitendo hicho kuhesabika kama ni utekaji nyara.

Hata hivyo, alidokeza kuwa kuna uwezekano mkubwa kesi hiyo ikapelekwa kwenye mahakama za juu kutokana na uzito wake, kwani ni ya utekaji nyara.

Mshtakiwa alikana shtaka hilo na kupelekwa rumande. Kesi hiyo imepangwa kuendelea tena Julai 27, mwaka huu

Chanzo: Nipashe

Polisi wanatakiwa kuanza kujifunza somo moja kutokana na tukio hili!
Imekuwa mazoea na hasa Trafiki barabarani kuingia ndani ya magari ya watu bila hata kukaribishwa na muda mwingine hata kufikia kiwango cha kuchomoa ufunguo !

Malengo makuu ya kufanya hivyo ni kutengeneza mazingira ya kupokea chochote kwa urahisi na nje ya macho ya wapita njia.
 
mtekwa nyara anaongea na Radio Call? ? only in Tz hii! ! sioni cha maana hapa, kama sheria ikizingatiwa mwenye kosa ni Traffic, maana hakuna sheria inayomruhusu kuingia kwenye gari la mtuhumiwa hata kama amekataa kutii sheria! yeye aliingia kufanya nini? tena mlango wa nyuma??? kalazimishwa? but poor him (jamaa) bongo hamnaga sheria, huku ni kulazimishana na kunyanyasana!
 
Hivi na hiki kitendo cha hawa askari wa barabaranu kuchukua ufunguo wa chombo cha usafiri ni sahihi??
Maana najiulizaga sipati majibu
 
Koma kupanda magari ya wanaume ,mtu katoka kilombero huko kaja mjini kuuza mazao unamla rushwa,ndo maan mnakufaga kibudu,ila pole kwa ugonjwa
 
Hivi na hiki kitendo cha hawa askari wa barabaranu kuchukua ufunguo wa chombo cha usafiri ni sahihi??
Maana najiulizaga sipati majibu
Gari yangu ya jasho langu funguo anachukua ye kama nani???!!!
Kupanda tu labda lifti, nikiwa na kosa atanielekeza wapi pa kwenda sio kuongozana naye kwenue gari yangu!!!!!!

Never!!!!
 
Gari yangu ya jasho langu funguo anachukua ye kama nani???!!!
Kupanda tu labda lifti, nikiwa na kosa atanielekeza wapi pa kwenda sio kuongozana naye kwenue gari yangu!!!!!!

Never!!!!

Naonaga wanavyo wasumbua wadada. Dats why nikiwaga na bro yey nyuma huwa ana tundika kombati lake la jeshi. Hawaleti shobo
 
Hii kesi ni nyepesi sana.
Hakuna utekaji hapo sana sana mshitakiwa atatiwa hatiani kwa kukataa kutii amri ya polisi basi.

Mtekaji gani anamwachia mateka awasiliane na radio!

nakusihi uwe wakili wa mshitakiwa
 
Alexander Msowoya (35), ambaye ni mkazi wa Chang’ombe, jijini Dar es Salaam, amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Magomeni akikabiliwa na shtaka la kumteka nyara askari wa kike wa usalama barabarani.

Akiwa anaendesha gari, mshtakiwa huyo anadaiwa kumteka Kostebo Ester katikati ya maeneo ya Tameke na Chang’ombe kabla ya kukamatwa maeneo ya katikati ya Mabibo na Ubungo baada ya msako mkali wa polisi waliokuwa wakitumia redio za upepo.

Hati ya mashtaka iliyosomwa mbele ya hakimu Mwanaidi Ngoda ilidai kuwa Julai 11, mwaka huu, saa 9:00 alasiri, eneo la kati ya Temeke na Chang’ombe, mshtakiwa alimteka nyara askari polisi Konstebo Ester, alipotakiwa kuonyesha leseni yake.

Ilidaiwa kuwa Afande Ester alimkamata mshtakiwa huyo akiwa anaendesha gari lenye namba za usajili T 495 BKJ na kumtaka aonyeshe leseni yake, lakini hakufanya hivyo.

Baada ya hapo, ikadaiwa kuwa trafiki huyo wa kike akamwamuru dereva huyo aliyekuwa anaendesha gari aina ya Rav4 ya rangi ya bluu kuweka gari lake pembeni, lakini alikaidi kwa kudai ana haraka.

Kutokana na hali hiyo, ilidaiwa kuwa askari aliingia ndani ya gari kwa kupitia kwenye mlango wa nyuma na kuamuru waende kwenye kituo cha polisi Chang’ombe.

Hata hivyo, ilidaiwa kuwa badala ya kuelekea alikoelekezwa, mshtakiwa alianza kwenda anakokujua yeye, hivyo kukiuka amri halali ya polisi na kitendo hicho kuhesabika kama ni utekaji nyara.

Awali, kabla ya kesi hiyo kusomwa, askari polisi mmoja alimwambia mwandishi wa habari hizi kuwa kilichomuokoa afande Ester ni redio ya mawasiliano aliyokuwa nayo, ambayo kwa kiasi kikubwa ilifanikisha kujua walipo na wanakoelekea.

Hivyo, walikuwa wakifanya mawasiliano na askari wengine waliokuwa maeneo mbalimbali gari linapopita na ikasaidia kukamatwa.

“Afande amepumzika nyumbani kwake. Kwa sasa hali yake si nzuri ana presha kutokana na tukio hili,” alisema askari mmoja wa kiume mahakamani hapo, ambaye hakutaka kutaja jina lake.

Hata hivyo, alidokeza kuwa kuna uwezekano mkubwa kesi hiyo ikapelekwa kwenye mahakama za juu kutokana na uzito wake, kwani ni ya utekaji nyara.

Mshtakiwa alikana shtaka hilo na kupelekwa rumande. Kesi hiyo imepangwa kuendelea tena Julai 27, mwaka huu

Chanzo: Nipashe

kisheria trafik hakuwa na haki ya kupanda hilo gari.angemuamuru aendr polisi.ila akiomba anaeeza kumpakia.
 
Hapo mwenye kesi ya kujibu ni askari: ni kosa kuingia ndani ya gari la mtu bila ridhaa yake.

If the police search your car without a warrant,your permission,or a valid reason,they are violating your constitutional rights.Nevertheless, police can search a car without a warrant in a number of circumstances.
 
Back
Top Bottom