Trafiki wa kike atekwa akiwa barabarani

Trafiki wa kike atekwa akiwa barabarani

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,267




Alexander Msowoya (35), ambaye ni mkazi wa Chang'ombe, jijini Dar es Salaam, amefikishwa katika Mahakama ya Mwanzo Magomeni akikabiliwa na shtaka la kumteka nyara askari wa kike wa usalama barabarani.


Akiwa anaendesha gari, mshtakiwa huyo anadaiwa kumteka Kostebo Ester katikati ya maeneo ya Tameke na Chang'ombe kabla ya kukamatwa maeneo ya katikati ya Mabibo na Ubungo baada ya msako mkali wa polisi waliokuwa wakitumia redio za upepo.

Hati ya mashtaka iliyosomwa mbele ya hakimu Mwanaidi Ngoda ilidai kuwa Julai 11, mwaka huu, saa 9:00 alasiri, eneo la kati ya Temeke na Chang'ombe, mshtakiwa alimteka nyara askari polisi Konstebo Ester, alipotakiwa kuonyesha leseni yake.

Ilidaiwa kuwa Afande Ester alimkamata mshtakiwa huyo akiwa anaendesha gari lenye namba za usajili T 495 BKJ na kumtaka aonyeshe leseni yake, lakini hakufanya hivyo.

Baada ya hapo, ikadaiwa kuwa trafiki huyo wa kike akamwamuru dereva huyo aliyekuwa anaendesha gari aina ya Rav4 ya rangi ya bluu kuweka gari lake pembeni, lakini alikaidi kwa kudai ana haraka.

Kutokana na hali hiyo, ilidaiwa kuwa askari aliingia ndani ya gari kwa kupitia kwenye mlango wa nyuma na kuamuru waende kwenye kituo cha polisi Chang'ombe.

Hata hivyo, ilidaiwa kuwa badala ya kuelekea alikoelekezwa, mshtakiwa alianza kwenda anakokujua yeye, hivyo kukiuka amri halali ya polisi na kitendo hicho kuhesabika kama ni utekaji nyara.

Awali, kabla ya kesi hiyo kusomwa, askari polisi mmoja alimwambia mwandishi wa habari hizi kuwa kilichomuokoa afande Ester ni redio ya mawasiliano aliyokuwa nayo, ambayo kwa kiasi kikubwa ilifanikisha kujua walipo na wanakoelekea.

Hivyo, walikuwa wakifanya mawasiliano na askari wengine waliokuwa maeneo mbalimbali gari linapopita na ikasaidia kukamatwa.

"Afande amepumzika nyumbani kwake. Kwa sasa hali yake si nzuri ana presha kutokana na tukio hili," alisema askari mmoja wa kiume mahakamani hapo, ambaye hakutaka kutaja jina lake.

Hata hivyo, alidokeza kuwa kuna uwezekano mkubwa kesi hiyo ikapelekwa kwenye mahakama za juu kutokana na uzito wake, kwani ni ya utekaji nyara.

Mshtakiwa alikana shtaka hilo na kupelekwa rumande. Kesi hiyo imepangwa kuendelea tena Julai 27, mwaka huu

Chanzo: Nipashe
 
Huyu jamaa kama hana leseni kweli imekula kwake. ndio hawa hawa wanaosababisha ajali. Mama angeongeza shitaka jingine la kutaka kubakwa. achezee mvua huyu fedhuli.
 
au jamaa alitaka kuoa ile kizamani?

usukumani wanaita chagulaga unachukua unaweka begani halafu unatuma wazee wanaenda kwa wazazi but in this case jamaa alikuwa hana nia ya kuteka coz afande kaingia mwenyewe garini bila kulazimishwa na inawezekana jamaa alikuwa hajui kituo cha polisi kilipo akawa anaweweseka mitaani na tatu angekuwa hana leseni angeshitakiwa pia kwa kosa hilo it seems leseni alikuwa nayo chezea kubambikiza kesi na ukute trafik anapigwa na bosi basi nae anakuwa bosi
 
hivi hii kitu ya askari kufungua mlango na kuingia kwenye gari bila idhini ya mwenye gari inakuwaje????? mi huwa siilewi....
Tunao wataalam wa sheria humu watatusaidia. Lakini inaudhi sana polisi anapokukamata na kukulazimisha umsafirishe wewe hadi kituoni bila malipo. Huyu angeumizwa ingekuwa fundisho kwa hawa wezi.
 
Back
Top Bottom