TRA wanavyofunga biashara za wazalendo

Nimeipenda point namba 4. 👍👍👍
 
Haya yote lisu alikuwa anapigia kelele kwa kujiamini kabisa sababu alishakuwa anapata taarifa sahihi tra wanaagizwa na magufuli kubambikia wafanyabiashara kodi kubwa hasa wale ambao hawaichangii ccm
Sasa jambo hili lakukamata akaunti za bank ndio baya zaidi
 
Hawa jamaa mimi nawaogopa sana. Hata kufungua bank account naogopa. Cjui pesa zangu zikiwa nyingi ntaziweka wapi.
Unaagiza gunia la mchele kutoka majuu..unalilipia kodi. Baada ya kuliuza..unawakatia chao tena. Yaani wanakula mara nyingi kwa kitu kimoja hawa jamaa.
 
Mimi ni tax Consultants, nieleze tatizo ni nini nikusaidie
 
Wewe ni miongoni mwa makasuku wa ccm hapa jf , tulikuonya kwamba shetani hana rafiki ukapuuza , sasa zamu yako imefika unamlilia nani ?
 
Mkuu tupe ushauri mzuri

Sent using Jamii Forums mobile app
TAX BURDEN PRINCIPLE (KANUNI YA MIZANIA/MZIGO WA KODI)

Jambo kubwa nililojifunza kutoka kwa wachangiaji wa huu uzi ni kuwa ufahamu wa kodi ni tatizo kubwa kuliko kodi yenyewe. The problem is not "tax" but "understanding of tax".

Jambo muhimu kwa kila mfanyabiashara si tu kujua aina za kodi bali kujua MIZANIA YA KODI (TAX BURDEN) ktk aina hizo za kodi.

Laiti wafanyabiashara weng wangejua kanuni (principle) hii ya TAX BURDEN watafahamu kuwa kodi nyingi hazilipwi na wafanyabiashara bali wao ni wakusanyaji (Witholding tax agent) na watoa taarifa ktk mamlaka husika (file returns).

TAX BURDEN ni kanuni inayoonyesha ni nani haswa (Halisi) anawajibika kuilipia kodi fulani. Kwa dhana hii kuna tofauti kati ya mkusanyaji kodi na mlipaji wa kodi. Unaweza kuwa mkusanyaji kodi fulani lakini si wewe mlipaji wa kodi husika. Na hapa ndio wafanyabiashara wengi wameshindwa kuelewa kanuni hii na kuhisi wanaonewa au kulipa kodi kupita kiasi. Si sahihi

Kwanza, Mfano ni kodi ktk mishahara ya wafanyakazi inayoitwa PAYE anayelipa(kukatwa) ni mfanyakazi husika ila mwajiri anaiwakilisha tu ofisi za mapato

Pili, Kodi ya zuio (Withholding tax) ktk kodi ya pango (rent) na huduma (outsourced services) anayelipa/kukatwa ni Land Lord au anayepokea pango na sio mfanyabiashara anayelipa pango. Jukumu la mfanyabiashara ni kuikata na kuipeleka ofisi ya mamlaka.

Vivyo hivo ktk kodi ya ongezeko la thamani (Value added tax - VAT) pamoja na Capital gain tax ni kodi ambazo wafanyabiashara hawalipi wao direct ila wanakusanya kwa watu wengine na kuikabidhi kwa mamlaka husika.

Changamoto inakuja pale ambapo aliyepewa jukumu la kukusanya kodi kisheria hafanyi jukumu lake (failure to collect and remit tax to authority), hapo ndipo TAX BURDEN huhama kutoka kwa MLIPAJI halisi wa kodi husika kwenda kwa MKUSANYAJI., na wafanyabiashara wengi huishia kuumia kwa kubeba msalaba usio wao.

Kutokana na principle hii ya TAX BURDEN tayari tunaona kodi nyingi kimsingi hazilipwi na wafanyabiashara bali wao ni wakusanyaji tu (Collect and file returns). Ukielewa principle hii kama mfanyabiashara utafanikiwa sana katika biashara yako na utapunguza Tax liabilities zisizo na ulazima.

ITAENDELEA..
 
KWAHIYO?
 
Leo Kuna jirani yangu ana biashara yake maskini wanasema slope 18 MILIONI sijui kivipi au afungee mgahawa
 
Daylight robbery by Zanzimana from kijani kibichi green party .
 
Wafanyabiashara wa Tanzania walio wengi hawapendi professionalism, wengi wanaweza ajiri accountant au kumlipa pale anapokuja kumuwekea hesabu sawa Ila wengi hawawataki mwishowe wanaishia kulalamika
 
Mkuu ukiendelea unitag
 
Huo ndiyo ujinga wao wanaua biashara matokeo yake wanakosa kodi endelevu za mda mrefu

wamejaa wasomi bandia, wasiojua au kujari hata hesabu ndogo tu zinavyokwenda. Na kwa kweli sijui hizo ajira milion nane zitatoka wapi kama ilivyoelezwa kwenye ilani ya CCM ya uchaguzi, kama TRA itaendelea hivi.
Mitaji inakufa, biashara zinafungwa. Wao wanachojari ni rushwa tu. Wamejaa wala rushwa TRA
 
Kuna jamaa alipelekewa tax liability ya 70m.. akahoji ikabaki kama 2.7m ndo anapambana nao ailipe.
Aiseee jamaa wanapiga spana.
 
I wish Magufuli asome hii thread ,sio kusikiliza majungu ya kina msukuma sijui DED kununua Gari la million 400
Mh rais anakazi kubwa ya kufanya tax reforms ili kikuza biashara ndogo,suala la vitambulisho la wamachinga silikubali Sana,maana ukiendekeza tabaka Fulani lilisilipe Kodi ,unatengeneza kizazi kibaya Sana
 
Wafanyabiashara wa Tanzania walio wengi hawapendi professionalism, wengi wanaweza ajiri accountant au kumlipa pale anapokuja kumuwekea hesabu sawa Ila wengi hawawataki mwishowe wanaishia kulalamika
Prevention is better than cure, kama VAT tu ambayo inatakiwa kuwa rahisi inawashinda hesabu zake na kuishia kulalamika kubambikiziwa malipo.

Income tax si ndio kasheshe huko naona ndio wanatandikwa mpaka wanatia akili.

Sitoshangaa nikisikia 90% ya wafanyabiashara wakitanzania awaelewi ‘2008 income tax act’.

Hao wachache ambao wanaijua kwa kuangalia mwenendo wa malalamiko sidhani kama wanaweza tengeneza income statement sambamba na sheria kuweza kufanya expense adjustments za ‘allowed and disallowed expenditures’, uelewa wa treatments za depreciation of assets, capital allowances; etc kwa manufaa yao ili kupunguza kodi wanayotakiwa kulipa.

Solution ya haya matatizo ni accounting services na mtaalamu mmoja wa tax kutoa kitabu cha income tax kinachokuwa updated annually baada ya budget kuwasaidia accountants kwenye kufanya hesabu zao. That’s what other people do in the world.

So far kwetu kwenye maswala taxation mwerevu wa sheria ni mmoja tu “TRA” wafanyabiashara wapo at his mercy; balance inahitajika wafanyabiashara lazima na wao watumie wataalamu kuwaandilia hesabu.

Tatizo ninalo liona ‘knowing us Tanzanians’ mijitu itakayotoa hizo services itaanza tamaa kuja na charges za millions na kuwafanya watu waone gharama kwenda. Badala ya kufikiria in terms economic of scale. We ukipata wateja 300 wa kuwafanyia tax kila mmoja ukamcharge laki moja tu kwa mwaka maisha umeyapatia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…