TRA wanavyofunga biashara za wazalendo

Tatizo TRA wanafanya kazi kwa hofu.

Bwana yule kawapa targets ambazo hazina uhalisia, na wasipo fikia targets hizo wanaonekana wameshindwa kazi na hivyo kujiweka kwenye hatari ya kutumbuliwa.

Kwa maana hiyo basi wanalazimika kukusanya kodi kwa mabavu haijalishi hata kama wanawaumiza walipaji, mradi tu waendane na matakwa ya bwana yule.

Sent from my M100 using JamiiForums mobile app
 
Maneno ya busara mkuu.
 
Ushauri: Mtu yeyote asifanye biashara yenye mkono/uhusiano wa TRA wala kusajiliwa na TRA.

Inabidi pawe na uzi wa orodha ya biashara mbalimbali ambazo hazihusiani na TRA wala ukiifanya hiyo biashara hauhitajiki kusajiliwa na TRA.
Hii ni kweli kabisa,fanya mpango uanzishe huo Uzi maana bila hivyo wengi tutakufa mapema kwa upuuzi wa Jiwe na TRA yake.
 
Ushauri: Mtu yeyote asifanye biashara yenye mkono/uhusiano wa TRA wala kusajiliwa na TRA.

Inabidi pawe na uzi wa orodha ya biashara mbalimbali ambazo hazihusiani na TRA wala ukiifanya hiyo biashara hauhitajiki kusajiliwa na TRA.
Mkuu, ni zipi hizo?
 
Pole zake nyingi.
 
Wafanyabiashara wa Tanzania walio wengi hawapendi professionalism, wengi wanaweza ajiri accountant au kumlipa pale anapokuja kumuwekea hesabu sawa Ila wengi hawawataki mwishowe wanaishia kulalamika
Huu ni ukweli
 
Ukiwa maskini mara nyingi unakua mchawi, shida yke watu wote wawe kama yeye, hizi roho mbya na husda sijui huwa zinamsaidia nn
Easier say than do. Unalipa na nini? Wala sio kulia. TRA iko kwa mujibu wa sheria. Na hawako juu ya sheria. Msijidanganye. Mwenzako akinyolewa, wewe tia maji
 
Ni kweli mkuu.
Tatizo ni kwamba wafanyabiashara wengi hawazijui haki zao kutokana na kutoelewa sheria.
Na wafanyakazi wengi tu TRA hawazijui sheria za kodi.
Watu wa system wakiamua kuna cha sheria...mwendo wa ubabe tuu
 
So mliambiwa muandamane Kura zimeibiwa za lisu mdai haki yenu mkatuona wasenge. Sasa mlinywe mnalialia ili iweje sasa. Mlidhani sisi watoto wa maskini ndo tutaumia tu kwa kukosa ajira. Mana ajira imekuwa issue sasa hivi na zilizopo zinayeyuka kila kukicha..

Jifunze I kudai haki kwa migomo na kuandamana Kama ilivyokenya bila kujali kupigwa mabomu. Otherwise mtabinwa Sana na lisu Yuko zake ughaibuni aliwawatete Sana mkamuona kachanganyikiw
 
Ukiwa maskini mara nyingi unakua mchawi, shida yke watu wote wawe kama yeye, hizi roho mbya na husda sijui huwa zinamsaidia nn

Na kwa kweli wengi wao misheni kubwa ni kuona wote tunakuwa maskini. Nina shaka sana kama hiyo ndio kazi waliyopewa.
Haya maandishi yetu hayaendi bure. Wakae mkao wa kula. Ilani ya CCM imeeleza wazi umuhimu wa private sector. Wao wanaivuruga kwa manufaa ya nani?
 
Akalipe, kodi ina sehemu mbili mapato(mauzo ghafi)/matumizi mapato yako msotly TRA wanakuwa nayo. ni wajibu wako kuthibitisha matumizi yako kwa risiti/viambatanisho kinyume cha hapo utaona ni wa kuonewa.
 
Akalipe, kodi ina sehemu mbili mapato(mauzo ghafi)/matumizi mapato yako msotly TRA wanakuwa nayo. ni wajibu wako kuthibitisha matumizi yako kwa risiti/viambatanisho kinyume cha hapo utaona ni wa kuonewa.
Mtabaki wenyewe sasa. Tutaona mtakusanya wapi kodi. Mwenzenu wa Zanzibar kashashtuka baada ya kuchungulia bara kinachoendelea kwa wafanyabiashara na biashara kwa ujumla zinavyofungwa. Kwa sasa nina imani ili kufikia malengo ndio imefikia sasa kuwabambikiza watu kodi kubwa ili kufidia gape ya wale waliofunga,hayo ndio matatizo yake,mzigo mkubwa wameanza kubeba watu wachache. Nina uhakika ikiendelea hivi miaka hata miwili mbele,hakuna biashara itabaki,mtakusanya hela zenu mfukoni
 
ukiona wanakimbili huko maana yake kuna loopholes za kukwepa kodi nakufanya biashara zisizo nyooka,wakibana na huko watakibia tena. ukinyooka TRA HAWANA HATA SHIDA NA WEWE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…