TRA wanafanya wizi mkubwa kwa Watanzania

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
26,461
Reaction score
40,069
WanaJF,
TRA kitengo cha Customs ambapo hushughulikia ushuru wa magari na bidhaa zinazoingizwa nchini kupitia bandarini wamekuwa ni mawakala wa wizi wa fedha za walipa kodi wa nchi hii.

Unakuta mtu ameagiza mzigo ama gari na lipo njiani na pia Bill of Lading imetumwa kwa wakati na inawasilishwa customs office kwa ajili ya ukokotozi wa gharama za ushuru, Kwanza utakuta unabambikiziwa uchakavu (ongezeko) kwa utashi wa afisa anayeshughulikia ukokotoaji huo. Sidhani kama kuna mtu aliyewahi kuagiza gari nje aliyekwepa hili tatizo. Bei halisi ambayo imeambatanishwa kwenye invoice na ambayo hulipwa kupitia mfumo wa kibenki huwa wanaiona siyo gharama halisi ya gari bali wanakuongezea gharama kwa kukadiria thamani wanayoiona wao.

Pili hii inahusu hata wale wanaolipia road lincence kwani utakuta disc inachelewa kwa kisa cha MTANDAO UPO CHINI. Na utasubiri hadi wiki kadhaa zipite ndo upate disc, tukirejea kwenye ishu ya magari unaweza ukakuta MTANDAO upo chini hadi gari inafika, inakaa bandarini kuvuka siku za kuanza kulipia gharama za storage ambapo hadi mtandao umekaa wima utakuta mteja analazimika kuingia gharama nje ya bajeti halisi inayotakiwa kulipia ushuru na charges zingine.

Hivi ninavyoandioka hapa ni kwamba Mtandao upo chini (due to Mkongo wa Taifa kukatika) na huduma zoote customs zimesimama na kuna mlolongo wa mizigo na magari vinapaswa kulipiwa ili yatoke lakini hakuna plan B wala C ya kuondoa tatizo la msongamano. Nimejiuliza, nani anawajibika kulipia UZEMBE wa TRA kutokuwa na mfumo mbadala endapo mfumo rasmi kushindwa kufanya kazi? Server wanayoitumia imeonesha wazi kabisa ni ndogo na haikidhi viwango vya ongezeko la wateja wanaotumia Bandari na kwa nini hawanunui server inayokidhi viwango? Kama server inakuwa down wana BACKUP plani gani kuondoa udhia kwa wateja ambao wanasubirishwa kwa muda mrefu? Kwa wale wanaikuja nchini kufuata cargo ili kupeleka nchi jirani wanalipiwa na nani gharama za ongezeko la siku wanazokaa nchini kusubiri mtandao kutengemaa?

Endapo Mtandao hautatengemaa hadi kuvuka siku za mteja kulazimika kulipia bandari storage charges nani anawajibika ktk hilo?

Watanzania tuachane na mazoea ya HEWALA kwa kila udhaifu unaofanywa na serikali kwa uzembe wa watu wawili watatu ambao wanapaswa kutimiza majukumu yao. Serikali inakosa mapato kwa uzembe wa majizi yaliyojazana forodha pale hadi kufikia inaamua kuwaumiza wanachi kwa kuanzisha ushuru wa kadi za simu.

Mwenye kulifafanua hili tafadhali toa msaada....
 
Kama ni kelele zimepigwa mpaka basi; wewe sio wa kwanza, watu hadi wamelia machozi lakini kimeishia kuwa kilio cha samaki. So, hiyo ni hali unayopaswa kuizoea Mkuu. Jambo bora zaidi unaloweza kulifanya ni kumlilia Mwenyezi Mungu aingilie kati.
 
WanaJF,
TRA kitengo cha Customs ambapo hushughulikia ushuru wa magari na bidhaa zinazoingizwa nchini kupitia bandarini wamekuwa ni mawakala wa wizi wa fedha za walipa kodi wa nchi hii.

Unakuta mtu ameagiza mzigo ama gari na lipo njiani na pia Bill of Lading imetumwa kwa wakati na inawasilishwa customs office kwa ajili ya ukokotozi wa gharama za ushuru, Kwanza utakuta unabambikiziwa uchakavu (ongezeko) kwa utashi wa afisa anayeshughulikia ukokotoaji huo. Sidhani kama kuna mtu aliyewahi kuagiza gari nje aliyekwepa hili tatizo. Bei halisi ambayo imeambatanishwa kwenye invoice na ambayo hulipwa kupitia mfumo wa kibenki huwa wanaiona siyo gharama halisi ya gari bali wanakuongezea gharama kwa kukadiria thamani wanayoiona wao.

Umechanganya madesa ndugu yangu nasikitika kukujulisha kuwa TRA hawana mfumo huo unaouongelea.
 
WanaJF,......
Unakuta mtu ameagiza mzigo ama gari na lipo njiani na pia Bill of Lading imetumwa kwa wakati na inawasilishwa customs office kwa ajili ya ukokotozi wa gharama za ushuru, Kwanza utakuta unabambikiziwa uchakavu (ongezeko) kwa utashi wa afisa anayeshughulikia ukokotoaji huo. Sidhani kama kuna mtu aliyewahi kuagiza gari nje aliyekwepa hili tatizo. Bei halisi ambayo imeambatanishwa kwenye invoice na ambayo hulipwa kupitia mfumo wa kibenki huwa wanaiona siyo gharama halisi ya gari bali wanakuongezea gharama kwa kukadiria thamani wanayoiona wao.
Mwenye kulifafanua hili tafadhali toa msaada....

Umechanganya madesa ndugu yangu nasikitika kukujulisha kuwa TRA hawana mfumo huo unaouongelea. Usiwe mvivu wa kusoma nakushauri uingie kwenye website yao Tanzania Revenue Authority - Calculators & tools halafu u-download document yao inayoonyesha namna wanavyofanya valuation. Hakuna kilicho siri siku hizi wako wazi mno, tatizo labda kama huwezi kufuata mahesabu yao namna yanavyokwenda, ni pm siku moja nilkuelekeze vizuri, au uwaulize wenyewe customer service watakusaidia. Hawa watu sasa hivi wanafanya kazi vizuri mno inabidi kuwapongeza badala ya kuwalalamikia.
 
Ina maana MAHAKAMA haina nguvu tena dhidi ya sheria kandamizi kama hizi?
 
Serikali ya ccm sio sikivu. Hata ufanyeje hawatajali. Wakikosa mapato kwa njia hii watatafuta njia nyingine ya kukwapua fedha toka kwako.

Itabidi tulie tu mpaka chama kingine kiongoze nchi.
 
Umechanganya madesa ndugu yangu nasikitika kukujulisha kuwa TRA hawana mfumo huo unaouongelea. Usiwe mvivu wa kusoma nakushauri uingie kwenye website yao Tanzania Revenue Authority - Calculators & tools halafu u-download document yao inayoonyesha namna wanavyofanya valuation. Hakuna kilicho siri siku hizi wako wazi mno, tatizo labda kama huwezi kufuata mahesabu yao namna yanavyokwenda, ni pm siku moja nilkuelekeze vizuri, au uwaulize wenyewe customer service watakusaidia. Hawa watu sasa hivi wanafanya kazi vizuri mno inabidi kuwapongeza badala ya kuwalalamikia.
Nashukuru kwa kunirekebisha mkuu. Siongezi neno hapo inawezekana kuna something hakijaeleweka vyema kwenye calculations zao.

Turejee kwenye hili la system downtime. Kwa nini MTEJA awajibike kwa system failure? Hamna Plan B?
 
KUNA KIPINDI TULIHOJI KITU KAMA HIKI LAKINI HAKUKUWA NA JIBU LOLOTE........ TAFADHALI SOMA KWA MAKINI

https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/307564-hizi-kodi-za-tra-za-kuingiza-magari-nchini-zikoje.html

Wadau kuna rafiki yangu kaniuliza kuhusu kodi za kuingiza magari yaliyo tumika toka Japan. Sasa ananiambia ameona kanuni za kukokotolea kodi kwenye tovuti yao http://www.tra.go.tz/index.php?option=com_content&task=view&id=460&Itemid=59. Lakini kilichomshtua ambacho hata mimi nimekiona ni kwamba kodi inatozwa kodi....
Ona hapo chini...

Formula:

  • I/D = CIF * 25%
  • EXA = (CIF+I/D) * 20%
  • EX = (CIF+I/D) * 5%
  • VAT = (CIF+I/D+EXA+EX) * 18%

Where:

  • CIF – Cost Insurance and Freight (Taxable Value)
  • I/D – Import Duty
  • EXA – Excise duty for vehicles aged more than 10 years
  • EX – Excise Duty
  • VAT – Value Added Tax

Sasa ukiangalia hapo juu kwenye hiyo kanuni (FORMULA) utagundua kuwa I/D (Import Duty) ambayo ni kodi nayo pia inatozwa kodi. Kwa lugha nyingine kwa wale wanaokumbuka milinganyo (a simple algebra), zile kanuni za pale juu ni sawa na kuziandika

  • EXA = (CIF+I/D) * 20% = CIF * 20% + I/D * 20%
  • EX = (CIF+I/D) * 5% = CIF * 5% + I/D * 5%
  • VAT = (CIF+I/D+EXA+EX)*18% = CIF * 18% + I/D * 18% + EXA * 18% + EX * 18%

Sasa kimsingi swali ambalo hata mimi nimeshindwa kumjibu rafiki yangu...... ni halali kodi kutozwa kodi???? katika mlinganyo huo hapo juu inaonekana kuwa I/D (Import Duty ambayo pia ni kodi) lazima itozwe EXA, EX na VAT. Pia EXA (Excise duty for vehicles aged more than 10 years ambayo pia ni kodi) na EX (Excise Duty ambayo pia ni kodi) nazo zinatozwa kodi.
Nauliza tena hiyo ni halali??? Sheria zinasemaje kuhusu hili... Nina hamu sana kujua jinsi sheria jinsi zinavyo sema... vinginevyo mimi naweza sema hii si haki kwa watanzania kutoza kodi kwenye kodi.....

Maana mimi nilifikiri kuwa kila kodi itatozwa kutoka kwenye kiwango cha msingi (a base) kwa hapa tuna maanisha CIF ambayo hata TRA wenyewe kwenye valuation yao ya magari wanasema ndiyo inayopaswa kutoza kodi (taxable) lakini cha kushangaza wanatoza hata kwa kodi ambazo hazipaswi kutozwa kodi (non - taxable) ......
Mimi binafsi nilifkiri kanuni ya kodi ingekuwa kama ifuatavyo

I/D = CIF * 25%
EXA = CIF * 20%
EX = CIF * 5%
VAT = CIF * 18%

Halafu lingine la msingi ni kuwa, kwa nini EX na EXA ambazo ni kitu kimoja zinatozwa mara mbili? Kwa nini isitozwe mara moja tu. Kwa mfano unaweza ukasema Gari lenye umri wa chini ya miaka 8 Excise Duty ni 10% na Gari lenye umri wa zaidi ya miaka 8 Excise Duty ni 15% ili mlinganyo uwe kama ifuatavyo....

I/D = CIF * 25%
EX = CIF * Q% (Q inategemea umri wa Gari. < miaka 8 ni 10%; > miaka 8 ni 15%)
VAT = CIF * 18%

Wanajamii nikipata mawazo ambayo yanaegemea sheria nitafurahi zaidi.....

Naomba kuwasiilisha...
 
Ina maana MAHAKAMA haina nguvu tena dhidi ya sheria kandamizi kama hizi?
kama kuna mtu hakuridhika na ukokotozi wa kodi, basi anakata rufaa kwa Commissioner general wa TRA,(Mkurugenzi mkuu wa mamlaka) huko nako asipopata ahueni ya tozo yake, anaweza kwenda kwenye Tax Revenue Appeals board, na tribunal, ( bodi ya rufaa za kodi)
 
nadhan picha halisi hata kama kuna watetezi apa ambao nadhan labda wanafanya kazi serikalini ni kwamba unapoona hata jirani zako wote wanakulalamikia basi ujue kuna tatizo......... haiwezekani wafanya biashara wa rwanda, congo, zambia, burundi na uganda walalamikie kitu icho icho alafu mseme si kweli??? kuna tatizo!!!
 
Nashukuru kwa kunirekebisha mkuu. Siongezi neno hapo inawezekana kuna something hakijaeleweka vyema kwenye calculations zao.

Turejee kwenye hili la system downtime. Kwa nini MTEJA awajibike kwa system failure? Hamna Plan B?

swala la mkongo wa taifa si la TRA bali wizara ya mawasiliano, science na technology! Plan B ni manual work mkuu kitu ambacho ni hatari kwa wahasibu. Benki penyewe mtandao ukiloga huchukui pesa, labda kuweka
 
Machine ndogo ya hesabu dukani inauzwa 1.5M Sidhani kama thamani yake ni kiyo kiukweli
 
Nchi imeshuhudia vurugu za wafanyabiashara kupinga kuuziwa mashine za VAT kwa gharama kubwa!
Ikumbukwe lengo kuu la mashine hizi ni kuwezesha TRA kukusanya mapata kwa ufanisi, kudhbiti wakwepa kodi pia kuwapa wafanyabiashara kumbukumbu za mauzo yao.
Ingekuwa busara kwa TRA kuzitoa hizi mashine bure na zibaki kuwa mali yao kwan faida kwao ni kubwa ukilinganisha na wafanyabiashara.
 
swala la mkongo wa taifa si la TRA bali wizara ya mawasiliano, science na technology! Plan B ni manual work mkuu kitu ambacho ni hatari kwa wahasibu. Benki penyewe mtandao ukiloga huchukui pesa, labda kuweka
Mkuu huo ndo unaitwa UDHAIFU na wizi.

Mtandao unbapokuwa haufanyi kazi vizuri kwa nini mlipa kodi AADHIBIWE?
Pia ukisoma ukokotozi aliouweka eliakeem hapo juu utaona wazi kabisa kwamba UJAMBAZI umehalalishwa kwenye sheria zilizopitishwa na Bunge.

Mnapofanya vitu kana kwamba ndio mnaoamua HATIMA za mifuko ya watu mnakosea sana.

TRA wanaongoza kwa WIZI kuliko hata mafisadi wa nchi hii.
 
Umechanganya madesa ndugu yangu nasikitika kukujulisha kuwa TRA hawana mfumo huo unaouongelea. Usiwe mvivu wa kusoma nakushauri uingie kwenye website yao Tanzania Revenue Authority - Calculators & tools halafu u-download document yao inayoonyesha namna wanavyofanya valuation. Hakuna kilicho siri siku hizi wako wazi mno, tatizo labda kama huwezi kufuata mahesabu yao namna yanavyokwenda, ni pm siku moja nilkuelekeze vizuri, au uwaulize wenyewe customer service watakusaidia. Hawa watu sasa hivi wanafanya kazi vizuri mno inabidi kuwapongeza badala ya kuwalalamikia.

nataka uniambie kwanini mtu anaepeleka mzigo mwanza anaachakulipa Sirari anaenda kulipia mtukula then ndio aende mwanza,na ni kwanini wafanyabiashara kanda ya ziwa wanatumia bandari ya mombassa wanakimbia Tanga na Dar? unajua kwanini?
 
WanaJF,
TRA kitengo cha Customs ambapo hushughulikia ushuru wa magari na bidhaa zinazoingizwa nchini kupitia bandarini wamekuwa ni mawakala wa wizi wa fedha za walipa kodi wa nchi hii.

Unakuta mtu ameagiza mzigo ama gari na lipo njiani na pia Bill of Lading imetumwa kwa wakati na inawasilishwa customs office kwa ajili ya ukokotozi wa gharama za ushuru, Kwanza utakuta unabambikiziwa uchakavu (ongezeko) kwa utashi wa afisa anayeshughulikia ukokotoaji huo. Sidhani kama kuna mtu aliyewahi kuagiza gari nje aliyekwepa hili tatizo. Bei halisi ambayo imeambatanishwa kwenye invoice na ambayo hulipwa kupitia mfumo wa kibenki huwa wanaiona siyo gharama halisi ya gari bali wanakuongezea gharama kwa kukadiria thamani wanayoiona wao.

Pili hii inahusu hata wale wanaolipia road lincence kwani utakuta disc inachelewa kwa kisa cha MTANDAO UPO CHINI. Na utasubiri hadi wiki kadhaa zipite ndo upate disc, tukirejea kwenye ishu ya magari unaweza ukakuta MTANDAO upo chini hadi gari inafika, inakaa bandarini kuvuka siku za kuanza kulipia gharama za storage ambapo hadi mtandao umekaa wima utakuta mteja analazimika kuingia gharama nje ya bajeti halisi inayotakiwa kulipia ushuru na charges zingine.

Hivi ninavyoandioka hapa ni kwamba Mtandao upo chini (due to Mkongo wa Taifa kukatika) na huduma zoote customs zimesimama na kuna mlolongo wa mizigo na magari vinapaswa kulipiwa ili yatoke lakini hakuna plan B wala C ya kuondoa tatizo la msongamano. Nimejiuliza, nani anawajibika kulipia UZEMBE wa TRA kutokuwa na mfumo mbadala endapo mfumo rasmi kushindwa kufanya kazi? Server wanayoitumia imeonesha wazi kabisa ni ndogo na haikidhi viwango vya ongezeko la wateja wanaotumia Bandari na kwa nini hawanunui server inayokidhi viwango? Kama server inakuwa down wana BACKUP plani gani kuondoa udhia kwa wateja ambao wanasubirishwa kwa muda mrefu? Kwa wale wanaikuja nchini kufuata cargo ili kupeleka nchi jirani wanalipiwa na nani gharama za ongezeko la siku wanazokaa nchini kusubiri mtandao kutengemaa?

Endapo Mtandao hautatengemaa hadi kuvuka siku za mteja kulazimika kulipia bandari storage charges nani anawajibika ktk hilo?

Watanzania tuachane na mazoea ya HEWALA kwa kila udhaifu unaofanywa na serikali kwa uzembe wa watu wawili watatu ambao wanapaswa kutimiza majukumu yao. Serikali inakosa mapato kwa uzembe wa majizi yaliyojazana forodha pale hadi kufikia inaamua kuwaumiza wanachi kwa kuanzisha ushuru wa kadi za simu.

Mwenye kulifafanua hili tafadhali toa msaada....
lipa kodi mkuu wewe unafikiri maendeleo yanatoka mbinguni?TRA wanapiga kazi nzuri sana na wanastahili pongezi,kuhusu hayo masuala technical sio swala la tra pekee mkonga wetu wa taifa una matatizo!
tatizo la sisi watz hatupendi kulipa kodi tumejaa porojo nyingi ,then tunajiita wazalendo kama yule jamaa aliyesema 2010 tukimchagua cement 5000?
 
Mkuu,
usidhani kila mtu hapendi kulipa kodi. Tunapenda kulipa kodi lakini ukusanyaji wa kodi usiwe kero ya kusababisha hasara kwa MTEJA.

Kuhusu Mkongo wa Taifa ni suala la serikali haihusu sekta binafsi. Kama mkongo umeharibika ni lazima kwa TRA kuwa na backup plan ili kutosimamisha shughuli.

Najua wewe huoni tatizo pale mtandao unapokuwa chini ambapo mnapiga soga bila kufanya kazi huku mkingojea mshahara wa bure (kwa timeframe ta mtandao kuwa chini). Tatizo siyo kukwepa kodi acha kukariri rudi juu usome post yote utagundua uzembe wako wa kusoma
 
Back
Top Bottom