KUNA KIPINDI TULIHOJI KITU KAMA HIKI LAKINI HAKUKUWA NA JIBU LOLOTE........ TAFADHALI SOMA KWA MAKINI
https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/307564-hizi-kodi-za-tra-za-kuingiza-magari-nchini-zikoje.html
Wadau kuna rafiki yangu kaniuliza kuhusu kodi za kuingiza magari yaliyo tumika toka Japan. Sasa ananiambia ameona kanuni za kukokotolea kodi kwenye tovuti yao
http://www.tra.go.tz/index.php?option=com_content&task=view&id=460&Itemid=59. Lakini kilichomshtua ambacho hata mimi nimekiona ni kwamba kodi inatozwa kodi....
Ona hapo chini...
Formula:
- I/D = CIF * 25%
- EXA = (CIF+I/D) * 20%
- EX = (CIF+I/D) * 5%
- VAT = (CIF+I/D+EXA+EX) * 18%
Where:
- CIF Cost Insurance and Freight (Taxable Value)
- I/D Import Duty
- EXA Excise duty for vehicles aged more than 10 years
- EX Excise Duty
- VAT Value Added Tax
Sasa ukiangalia hapo juu kwenye hiyo kanuni (FORMULA) utagundua kuwa I/D (Import Duty) ambayo ni kodi nayo inatozwa kodi. Kwa lugha nyingine kwa wale wanaokumbuka milinganyo (a simple algebra), zile kanuni za pale juu ni sawa na kuziandika
- EXA = (CIF+I/D) * 20% = CIF * 20% + I/D * 20%
- EX = (CIF+I/D) * 5% = CIF * 5% + I/D * 5%
- VAT = (CIF+I/D+EXA+EX)*18% = CIF * 18% + I/D * 18% + EXA * 18% + EX * 18%
Sasa kimsingi swali ambalo hata mimi nimeshindwa kumjibu rafiki yangu...... ni halali kodi kutozwa kodi???? katika mlinganyo huo hapo juu inaonekana kuwa I/D (Import Duty ambayo pia ni kodi) lazima itozwe EXA, EX na VAT. Pia EXA (Excise duty for vehicles aged more than 10 years ambayo pia ni kodi) na EX (Excise Duty ambayo pia ni kodi) nazo zinatozwa kodi.
Nauliza tena hiyo ni halali??? Sheria zinasemaje kuhusu hili... Nina hamu sana kujua jinsi sheria jinsi zinavyo sema... vinginevyo mimi naweza sema hii si haki kwa watanzania kutoza kodi kwenye kodi.....
Maana mimi nilifikiri kuwa kila kodi itatozwa kutoka kwenye kiwango cha msingi (a base) kwa hapa tuna maanisha CIF ambayo hata TRA wenyewe kwenye valuation yao ya magari wanasema ndiyo inayopaswa kutoza kodi (taxable) lakini cha kushangaza wanatoza hata kwa kodi ambazo hazipaswi kutozwa kodi (non - taxable) ......
Mimi binafsi nilifkiri kanuni ya kodi ingekuwa kama ifuatavyo
I/D = CIF * 25%
EXA = CIF * 20%
EX = CIF * 5%
VAT = CIF * 18%
Halafu lingine la msingi ni kuwa, kwa nini EX na EXA ambazo ni kitu kimoja zinatozwa mara mbili? Kwa nini isitozwe mara moja tu. Kwa mfano unaweza ukasema Gari lenye umri wa chini ya miaka 8 Excise Duty ni 10% na Gari lenye umri wa zaidi ya miaka 8 Excise Duty ni 15% ili mlinganyo uwe kama ifuatavyo....
I/D = CIF * 25%
EX = CIF * Q% (Q inategemea umri wa Gari. < miaka 8 ni 10%; > miaka 8 ni 15%)
VAT = CIF * 18%
Wanajamii nikipata mawazo ambayo yanaegemea sheria nitafurahi zaidi.....
Naomba kuwasiilisha...