Ufunguo
JF-Expert Member
- Aug 18, 2012
- 330
- 231
Umechanganya madesa ndugu yangu nasikitika kukujulisha kuwa TRA hawana mfumo huo unaouongelea. Usiwe mvivu wa kusoma nakushauri uingie kwenye website yao Tanzania Revenue Authority - Calculators & tools halafu u-download document yao inayoonyesha namna wanavyofanya valuation. Hakuna kilicho siri siku hizi wako wazi mno, tatizo labda kama huwezi kufuata mahesabu yao namna yanavyokwenda, ni pm siku moja nilkuelekeze vizuri, au uwaulize wenyewe customer service watakusaidia. Hawa watu sasa hivi wanafanya kazi vizuri mno inabidi kuwapongeza badala ya kuwalalamikia.
Uwazi unaousema ni upi?. Mbona katika calculator yao Hiace zote ziko kwenye eneo moja lakini unapokuja kufanya malipo unaambiwa eti hiace yenye viti ndani(wagon) ina ushuru mkubwa kuliko ile isiyokuwa na viti ndani (van). Sasa niambie idadi ya viti katika hiace inaongeza vipi kodi ya gari?, au ni sheria gani inayotumika na ambayo iko wazi kwa public kuhusiana na jambo hili?. Kwahiyo, wanataka kusema kwamba hiace zenye viti viondolewe kwanza hukohuko zinapotoka kabla hazijafika TZ ili kulipa ushuru wa kawaida?. Usiamini kutokana na uwepo wa calculator na/ama baadhi ya taarifa katika mtandao wa TRA, amini unapoona taarifa hizo zinafanya kazi vizuri (zinatoa matokeo yaliyotarajiwa).