TANMO
JF-Expert Member
- Apr 12, 2008
- 11,527
- 11,303
Na hapa umezungumzia Compliance za TRA pekee.Niwaambie TU wanajf
Hamna mfanyabiashara anapenda kukwepa Kodi kwa maendeleo ya nchi yake
Tatizo Ni
1. mfumo wetu wa Kodi umekaa kinyonyaji sana, anaetunga sheria na kanuni za Kodi ni mwanasiasa bill kumhusisha mfanyabiashara na hayajui mazingira halisi ya biashara.
Ukiifuata sheria ya Kodi inavotaka unafilisika mchana kweupe na hakuna anaekuonea huruma, kiukweli Kodi zetu sio rafiki kwa mfanyabiashara yeyote mzalendo.
2. Matumizi ya Kodi,
Inaumiza Sana unalipa Kodi kizalendo afu unaskia Kodi yako uliolipa Kuna wahuni wanafuja fuja TU kwa maslahi Yao binafsi Tena kwa majigambo lukuki wakiitana majina wanayojua wao kana kwamba sisi wengine hatuna akili wametupa limbwata.Inaumiza sana na kuvunja Moyo.
Bado mfanya biashara huyo huyo anadaiwa Leseni, Fire, Afya, Ulinzi Shirikishi, Wakala wa Vipimo, TBS, Usafi, Parking n.k n.k..
Na wote hao kila mmoja anakuja au unamfata kwa wakati wake.
Hii nchi mfanyabiashara ili Ufanikiwe ni lazima utaonekana haramia tu..
Wakati huo huo Ripoti za CAG kila mwaka zinataja matumizi mabaya ya Pesa za Umma miongoni mwa Watendaji wa Umma. Na hakuna hatua zinachukuliwa kudhibiti hili