TRA wakamata mabomu ya Barrick Mwanza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TRA wakamata mabomu ya Barrick Mwanza!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Halisi, Dec 18, 2008.

 1. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kuna taarifa kwamba TRA Uwanja wa Ndege wa Mwanza Idara ya Ushuru wa Forodha, wamezuia makasha kadhaa ya kampuni ya Barick Gold, yaliyokuwa yakipelekwa North Mara, kule Tarime.

  Habari zinaeleza kwamba awali polisi walibishana na TRA wakitaka mizigo hiyo iruhusiwe ipite lakini baada ya maofisa wa TRA kuwa wakali na kusema sheria inataka mizigo ya milipuko kuelezwa wazi katika nyaraka ni milipuko ya aina gani na badala yake mizigo ya Barick iliandikwa "Ammunition" tu bila kusema ni baruti, mabomu au kitu gani. Ka nzi ketu kalikoruka ruka juu ya eneo la uwanja kalielezwa na Ofisa Mmoja wa Polisi Mstaafu aliyekuwapo eneo la tukio kwamba makasha hayo yalikuwa na mabomu ya kutupa kwa mkono na mabomu ya machozi.

  Hofu iliyokuwapo sasa ni kwamba kutokana na matukio ya hivi karibuni ya huko Tarime na hasa baada ya kuikataa CCM, upo uwezekano mkubwa wa kwamba Barick pamoja na kuongezewa ulinzi wa polisi, sasa wanaongeza na silaha.

  Upo uwezekano kwamba silaha hizo ni za kwao wenyewe wakitumia walinzi wao wakiwamo wale wanaowajiri kutoka nje ya nchi wakiwamo wale kutoka Napal wajulikanao kama GURKAS.

  Lakini pia inawezekana silaha hizo zikawa ni mali ya Jeshi la Polisi ambalo kwa kawaida huwa na mikataba na Barick ya ulinzi mikataba ambayo kampuni hulazimika kulipa KIHALALI pale Makao Makuu ya Jeshi la Polisi na hivyo upo wasiwasi kwamba sasa wamekubaliana hata kugharamia vifaa kwa polisi ikiwamo vile vya kukabiliana na fujo.

  Kwa mwenye maelezo ya kina anaweza kutuhabarisha wakati ka-nzi ketu kanarukie pale Uwanja wa Ndege wa Mwanza kujua kama polisi na TRA wameshaelewana ama kuzibwa midomo ama la.

  Miaka ya 1997 hadi mwaka 2000 wakati Bulyanhulu palipokuwa na vurugu na matukio ya ujambazi katika mgodi wa Kahama, Barick waliagiza silaha aina ya AK 47 na waliomba kibali Wizara ya Mambo ya Ndani. Bahati mbaya sana habari hiyo ikaandikwa na gazeti la RAI wakati huo chini ya Jenerali Ulimwengu na ndipo serikali ikawanyima kibali cha kuingiza AK 47 ambazo zilikuwa zitumiwe na GURKAS ambao walikuwa tayari wako Kahama.

  SWALI: Je, sheria za nchi yetu zinaruhusu kampuni binafsi kuingiza silaha kali kama kweli itakuwa ni mabomu?
  je, Kama serikali ilijadili na kukubaliana na suala hilo ndani ya vikao, kwanini siri hiyo isitolewe hadharani kama ile ya Mengi na Masha?
   
 2. M

  Mama JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Watasema ni baruti za kupasulia miamba.
   
 3. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2008
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,560
  Likes Received: 1,923
  Trophy Points: 280
  Hii kali...Tanzania ishakuwa hivi..Ni GURKAS ndo mdudu gani?
  Yani tunaingiziwa majambazi nchini na kusema wanalinda..Nani kasema hatuwezi kulinda nchi yetu?
  Na hizo AK 47 wanataka kuuwa wananchi kwa style gani? What about hayo mabomu kama ni kweli...?Vita ya wenyewe kwa wenyewe bado inapaliliwa? Tanzania naisikitikia sana...Ila something tells me that we will be free one day.
  Kwasababu Uhuru gani huu?
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hapa kuna harufu kwanza ya rushwa na hao Polisi walio kuwa wanashinikiza yaruhusiwe.
  Hapo kazi kweli kweli lazima kuna mchezo mchafu kumbukeni maeneo yenye madini ndo chanzo cha machafuko barani Africa sasa kama hiyo kampuni inaruhusiwa kulinda basi hata hayo mabomu wanaweza kuyatumia kuangamiza raia wanao dai siku zote haki zao huko huku sirikali ikiwa imeweka mapamba maskioni kama vile inawaona raia hao wakimbizi na hao wenye ngozi nyeupe wanaonekana kama ndo wazawa.
  Kwa mtindo huu basi tunasubili maafa Mungu epusha mbali wazibue hawa sirikali pamba maskioni mwao.
   
 5. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #5
  Dec 18, 2008
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 182
  Trophy Points: 160
  Je, huu ni udhaifu wa Security System yetu au ni baadhi ya watu kutowajibika ipasavyo?

  Inashangaza sana . . .
   
 6. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #6
  Dec 18, 2008
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Kama huwajui ndio hawa:

  BBC NEWS | UK | Who are the Gurkhas?
   
 7. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #7
  Dec 18, 2008
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Halisi,

  Imekuwaje makampuni ya Tanzania yanaajiri walinzi kutoka nje ya nchi? Hivi hatuna uwezo hata wa kutoa walinzi?

  Tunalalamika vijana wetu hawana ajira huku kazi zinaenda kwa wageni?

  Inabidi waandishi wa habari muanze kuyavalia njuga haya mashirika yanayoajiri wafanyakazi wa nje hata kwa kazi ambazo Watanzania wanaweza kufanya.

  Hilo la mabomu kali.
   
 8. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #8
  Dec 18, 2008
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  OMG!

  Why this time?
   
 9. K

  Koba JF-Expert Member

  #9
  Dec 18, 2008
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ..haya ndio matokeo ya ufisadi wa kina Karamagi kwenda kusign mikataba kwenye vyumba vya Hotel London!
   
 10. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #10
  Dec 18, 2008
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  JK anashindwa kutimiza ahadi ya ajira kwa vijana wetu lakini watu wake wanawaruhusu wawekezaji waajili walinzi kutoka Nepal!! what a contradiction. Hiring these blood thirsty nepalese Gurkas is synonymous to murdering your own people.Please people in government can you get out of your slumber.
   
 11. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #11
  Dec 18, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hii sasa too much baadae tutaajiri mpaka Migambo kutoka nje watadai ili kuongeza ufanisi wa Halmashauri nchini.
   
 12. M

  Mutu JF-Expert Member

  #12
  Dec 18, 2008
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ndio hivyo hatujui mikataba wanayo sign inasema nini ndani yake inawezekana yote haya yako ndani ya mikataba.Na unaambiwa ni siri
   
 13. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #13
  Dec 18, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu hao askari wanahusika moja kwa moja na hili na ndio maana walikuwa wanabishana na jamaa wa TRA
   
 14. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #14
  Dec 18, 2008
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Isikuwa ni silaha za kutumaliza zinaingizwa kijanja,halafu polisi ndio anashinikiza ziingizwe kwani polisi na TRA si ni watoto wa baba mmoja kuna Barrick.Watanzania watchout msijegeuzwa chambo na mafisadi.
   
 15. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #15
  Dec 18, 2008
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Isijekuwa ni silaha za kutumaliza zinaingizwa kijanja,halafu polisi ndio anashinikiza ziingizwe kwani polisi na TRA si ni watoto wa baba mmoja kunani Barrick.Watanzania watchout msijegeuzwa chambo na mafisadi.
   
 16. M

  Mama JF-Expert Member

  #16
  Dec 18, 2008
  Joined: Mar 24, 2008
  Messages: 2,858
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 0
  Nakumbuka Darwin nightmare!

  Hivi waziri wa ulinzi na huyo wa mambo ya ndani wapo? au hapa anahusika waziri wa viwanda na biashara, waziri wa madini sijui au waziri wa fedha?
   
 17. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #17
  Dec 18, 2008
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  UFISADI ni tatizo kubwa sana.
  Uharibifu wa mfumo wa utendaji na ukiukaji wa sheria kanuni na taratibu za kiserikali, utokanao na UFISADI ni mpana kuliko matarajio walionayo Mafisadi wengi.
  Nia na madhumuni ya Fisadi yeyote ni kupata kujenga mazingira ya kupata yeye na kunyima wengine wote, bila kujali matokeo.
  Siku si nyingi tutasikia Barick wameingiza Jet Fighter, Vifaru, RPG hata IBM wakidai ni vifaa kwaajili ya kujilinda.
  Kuna mengi yanakuja.
   
 18. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #18
  Dec 18, 2008
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145

  Ahsante mkuu kwa habari hii,
  Kwa kweli hii ni habari mbaya sana kwetu wakazi wa tarime.Serikali imekuwa ikitunyanyasa muda mrefu tangu iwaruhusu hawa wakwapuaji kucchukua maeneo yetu bila kutulipa fidia inayolingana na thamani ya ardhi waliyopora.
  Ukichukulia hatua ya wapiga kura wa tarime kuamua kukipigia kura chama mbadala mara mbili, tunaona kuwa vile vitisho vya msekwa ukijumlisha na vikosi vya mkamata wapika gongo Tossi sasa wamepata sababu ya kuhalalisha umafia wao dhidi ya watu wa tarime.Lakini tunaamini kuwa pamoja na mateso yote tunayofanyiwa tarime hatutarudi nyuma, tutazidi kusonga mbele hadi hapo haki yetu itakapopatikana.Ipo siku Mungu atasikia kilio chetu na atawatia gerezani wote wanaotunyanyasa.
  Nimalizie kwa kuwapongeza hao maafisa wa TRA, kwa uzalendo wao na ninawaomba wasilegeze msimamo hata kidogo hadi ijulikane kama ni mabomu au ni mlipuko gani huo unaofichwa
  .
   
 19. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #19
  Dec 18, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  The entire govt is in deep shit in this
   
 20. Waga

  Waga JF-Expert Member

  #20
  Dec 18, 2008
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 321
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Aaaah hii ni hatari sasa, kama ni kweli wacha mi niendelee kupiga box maana Amani ipo wapi hapo? Mnataka kuangamiza wananchi ambao wanahaki ya kufaidi rasilimali zao? Mmeaondoa kwenye maeneo yao kwa nguvu kwa kuwahadaa kuwajengea vijumba ambavyo miundombinu ni mibovu ajabu, mmekata kata mazao yao kwenye mashamba ili mradi mkidhi haja yenu ya kuchukua mchanga wa dhahabu na kwenda kuupima huko mnapojua nyinyi hiyo yote haikuwatosha sasa mnawapelekea mabomu ili muwamalize kabsaa wasipige kelele dah natamani kulia kwa kweli... kama mikoa yote watu wangeamka kama huko Tarime basi nchi ingekuwa kwenye mstari ulionyooka
   
Loading...