TRA wakamata mabomu ya Barrick Mwanza!

Tz inanuka rushwa,ata walinzi wanatoka nje??????????????!!!!!!!!!!!!!!!!
 
SWALI: Je, sheria za nchi yetu zinaruhusu kampuni binafsi kuingiza silaha kali kama kweli itakuwa ni mabomu?
Hapana, haziruhusu.

Mabomu ni silaha za kivita. Bodi ya Ushauri wa Udhibiti wa Silaha za Kivita itapitia na kuamua juu ya maombi ya kibali cha kuingiza na kumiliki mabomu kutoka kwenye idara za serikali tu.

THE ARMAMENTS CONTROL ACT, 1991/2

Preliminary Provisons, Sect. 4

In this Act:
''The Board'' means the Armaments Control Advisory Board;

"Department" means any department or part of a department of the Government, vested with the duties of defence and security;

"Armaments'' means the following arms of war, whether complete or in parts and ammunition for them, namely, firearms, artillery of all kinds, apparatus for the discharge of all kinds of explosive or gas-diffusing projectiles, flamethrowers, bombs, grenades, machine guns, rifles, and small-fire breech-loading weapons of all kinds;

PROHIBITION ON IMPORT, EXPORT OF ARMAMENTS, Sect. 12 (1 )

No person shall import into or export from, or cause to be ported into or exported from the United Republic any armaments except with and under the terms of an authorization in the prescribed form granted by the Board.

FUNCTIONS OF THE BOARD, Sect. 8

The Board shall:
(b) receive and consider all requests by any department for acquisition of armaments;

(c) evaluate and recommend on the need and the request by any department for the acquisition by importation of armaments, taking into account the establishment of that department and its defence and security requirements and commitments.

"Your Black, not even a Nigga, your African" huya nayakumbuka hayo maneno nikiona taarifa kama hii. hayo maneno yaliongewa na General wa UN alikuwa Rwanda wakati wa mauaji ya 1993 (katika movie ya Hotel Rwanda) alimuambia yule Paul aliyewaokoa watu kwenye hotel. Kwa hiyo ndivyo jamaa wanajifanya wanajali haki za binadamu lakini linavyokuja suala la $$ na madini hawajali hilo. Wabongo inabidi tuwe makini wasije wakaua ndugu zetu huko, maana kuna watoto 19 walikufa na watu sijui tumeshasahau? ila wasije wakaongezeka watu wengine kufa kwa ajili ya upuuzi na halafu kila siku hakuna mtu anayewajibishwa.
 
Eee mungu tasaidie sisi waja wako.kama tena jamaa wanaruhusiwa kuingiza mabomu sijui tunaelekea wapi.mungu ibariki tz
 
Kama ni kweli Barrick imeruhusiwa kuajiri wageni kwa kazi ambayo inaweza kufanywa na wazalendo hiyo itakuwa ni dharau kubwa kwa TAIFA. Mh. Masha naona siku 7 zimekushinda kutoa maamuzi kuhusu wewe na Mengi ila nakuomba kwa niaba ya WATANZANIA ueleze umma ni vipi shirika ambalo linachota utajiri wetu linatoa ajira kwa foreigners wakati wazalendo wanataabika mitaani???????? Kwa kuwa wewe ulikacha JKT si wote ambao waliikacha. Kuna watu wengi wana qualifications za kufanya hiyo kazi inayofanywa na NEPALS/NEPALESE whatever you can call.
MASHA TOA SIKU 7 KWAKO MWENYEWE UELEZE UMMA KUHUSU NAPALESE.
 
Hawa wanepal mbona wameajiriwa siku nyingi tu na Barrick Gold hata kabla ya Mh Masha( toka awamu ya tatu) cha msingi ni taasisi husika na ajira iangalie hii maneno ya kuwaajiri wageni katika fani nyeti kama hz ambazo watanzania tunazimudu.
 
IY mbona unashangaa hili? yapo mengi tu........

Kama kweli serikali hii ina nia na watanzania kwa kungalia mbali wangekuwa wanaangalia succession plan za nafasi zinazoshikiliwa na wageni ili watz waweze kuzishika after a certain period kama wanavyokagua dhahabu na mapata TRA. Kwa kuwa kuwaelimisha wazawa kutakuwa na maendeleo endelevu.

Sijaipata ile ripoti ya Bomani lakini kosa nilionalo mimi ni kuwa hapa kwenye Training ndo muhimu ili baadae waje kudemand wazawa kuajiriwa. I support wageni waje hata kwenye ulinzi but wapewe muda. Mgodi una miaka mitano mpaka leo mlinzi ni mgeni. hapa mimi sielewi hata kidogo. ina maana kuwa sisi ni mambumbu sana? i understand Bsc of Mining Eng ya bongo na ya Canada ni tofauti je, inamaana hio mishimo yetu is too complex mpaka hatuelewi?

Siri moja ni kuwa hawa wageni e.g. mining manager wa geita hataweza kumfundisha local mining mpaka aje kwenye nafasi yake kwa kuwa hapa life is very cheap kwa mshahara ambao ni sawa na ule wa kule kwao, pili he/she can travel allover the world ambapo kama angukuwa kwao asingiweza. Mfano mtu alichukuliwa Australia kuja kufanya kazi hapa bongo, gharama ya kurudi kwao wakati wa likizo ni sawa na kwenda kutanua US kwanini aende Au badala ya US?

Tusisahau kuna watanzania wenzetu wanatuuza. Nasikia hawa jamaa wanauliza kwenye interview wewe umetokea wapi? kama umetokea Kilimanjaro hutapewa kazi ya uhasibu. Sasa wamejuaje kuwa mpaka makabila yanataniana au yana tabia hizo? wanajuaje?

Mimi namshangaa yule Mwanyika wa Barrick analishangaa Bunge, hivi kweli huyu ni Mtanzania au? Ina maana alishindwa kukaa kimya alinde kibarua chake na aonekane utanzania wake?
 
Hawa wanepal mbona wameajiriwa siku nyingi tu na Barrick Gold hata kabla ya Mh Masha( toka awamu ya tatu) cha msingi ni taasisi husika na ajira iangalie hii maneno ya kuwaajiri wageni katika fani nyeti kama hz ambazo watanzania tunazimudu.

Hii inaonehs a ni jinsi gani watanzania wengi walivyo unconsious. Hawa Nepalis wako Tanzania kwa zaidi ya miaka 4. Na hii ilisha semwa zamani tu! tukapiga kelele lakini watu ambao ni unconsius ni taabu tupu!.

Ni hivyo hivyo viongozi wengi wako unconsious kuwa wao ni watanzania na wanawajibu wa kutumikia taifa hili kwa uadilifu wa hali ya juu kwa manufaa ya watanzania wote na siyo kakakibala kamoja au kaukoo kamoja au kafamilia kamoja au kakikundi kamoja!!!!!!!!!
 
Hii sasa too much baadae tutaajiri mpaka Migambo kutoka nje watadai ili kuongeza ufanisi wa Halmashauri nchini.

Kama mgambo wetu wa halmashauri wanaopewa mamlaka ya kuondoa machinga badala yake wanawanyan'ganya bidhaa zao bila ya kuwapeleka mahakamani na bidhaa wanagawana. Mgambo hao wanaochukua rushwa kwa mama nitilie na kuwafumbia macho ili waendelee kuwauzia wananchi chakula maeneo machafu. Ni heri wa nje ambao wanaweza kuwa na nidhamu na kuweka miji katika hali ya usafi.
Tabia yetu baadhi ya watanzania ndio inayotufikisha pabaya. Sasa hivi kwenye duru za benki nchini kuna mawazo kuwa heri kuajiri vijana kutoka Kenya ambao wanafanya kazi kwa bidii na sio wezi. Na kwamba vijana wetu wanapoajiriwa benki akili yao ni kufikiri namna ya kuiba.
 
Mzigo wa Barrick wazua hofu airport

2008-12-19 11:35:08
Na George Ramadhan, Mwanza

Shehena kubwa inayosadikiwa kuwa na baruti za kupasulia miamba, risasi na mabomu ya kurusha kwa mikono na yale ya kutoa machozi, mali ya kampuni ya Barrick, imezuiliwa kwa muda katika uwanja wa ndege jijini Mwanza kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kina.

Habari za kipolisi zilizothibitishwa na Kaimu Kamanda wa Mkoa wa Mwanza, Khamis Bhai, zimeeleza kwamba, shehena hiyo imezuiliwa baada ya kuibuka utata wa nini hasa kilichokuwa ndani yake.

Kaimu Kamanda huyo jana alithibitisha kuzuiliwa kwa shehena hiyo hadi hapo itakapofanyiwa uchunguzi wa kina.

Alisema taarifa za awali zilionyesha kuwa ndani ya shehena hiyo kulikuwa na baruti kwa ajili ya kupasua miamba ya dhahabu iliyokuwa inasafirishwa kwenda katika Mgodi wa North Mara uliopo Tarime mkoani Mara. Mgodi huo unamilikiwa na kampuni hiyo.

Hata hivyo, Bhai alisema baadaye ilitaarifiwa kuwa shehena hiyo ilikuwa na vitu vingine zikiwemo risasi na mabomu ambayo hayakubainishwa ni ya aina gani.

Aidha, alisema kwamba shehena hiyo iliwasili jijini Mwanza kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya (KQ) juzi Desemba 17, 2008, wakati ilikuwa ikitarajiwa kuwa ingewasili siku mbili kabla ya tarehe hiyo.

Naibu Kamanda huyo alisema kuwa kutokana na hali hiyo, ilibidi shehena hiyo izuiliwe kwa muda hadi hapo itakapokuwa imefanyiwa uchunguzi wa kina kwa ushirikiano wa Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Idara ya Usalama wa Taifa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

``Ni kweli kuna shehena ya kampuni ya Barrick tumeizuia hadi hapo itakapofanyiwa ukaguzi, hivi tunavyoongea RCO (Ofisa Upelelezi wa Mkosa ya Jinai wa Mkoa) amekwenda uwanja wa ndege kuongoza zoezi la ukaguzi na baada ya hapo ndipo tutakuwa na taarifa sahihi,`` Bhai aliiambia Nipashe jana asubuhi.

Aliongeza kwamba lengo la ukaguzi huo ni kutaka kubaini iwapo vitu vilivyomo katika shehena hiyo vinaendana na vile vilivyopo katika nyaraka za kuombea kibali cha kuingiza nchini vitu vya aina hiyo.

Hata hivyo, Ofisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (RCO) Mkoa wa Mwanza, Augustine Olomi, alisema kwamba si kweli kuwa shehena hiyo imezuiliwa, bali ni utaratibu wa kawaida mzigo kama huo kufanyiwa ukaguzi pindi unapoingizwa nchini.

``Hakuna haja ya kukuza jambo hili, ni kawaida kwa mzigo kama huo kufanyiwa ukaguzi kutokana na unyeti wake hivyo hakuna sababu ya kusema kwamba umezuiliwa,`` alisema Olomi.

Aliongeza kwamba kimsingi, shehena hiyo ingeweza kushushwa moja kwa moja katika uwanja wa ndege wa North Mara Gold Mine, lakini kwa kuwa ni lazima ufanyiwe ukaguzi kwanza, ndiyo sababu imelazimu ushushiwe katika uwanja wa ndege wa Mwanza.

Hata hivyo, habari za awali zilizopatikana kutoka kitengo cha Usalama cha Uwanja wa Ndege wa Mwanza, zilisema kwamba kuzuiliwa kwa shehena hiyo kulitokana na kugubikwa utata jinsi ilivyosafirishwa.

Ilielezwa kwamba shehena hiyo ilikuwa imefungwa kana kwamba vitu vilivyomo ni baruti ya kulipulia miamba pekee, ingawa baadaye ilibainika kuwa kulikuwepo na vitu vingine zaidi.

Aidha, ilidaiwa kwamba kwa kawaida shehena za baruti zinazosafirishwa kupitia uwanja wa ndege wa Mwanza huwa zinakaguliwa na kusindikizwa na kikosi cha usalama cha uwanja wa ndege hadi migodini.

Hata hivyo, ilidaiwa kwamba katika hali ya kushangaza, maofisa wa kampuni ya Barrick walikwenda kupokea shehena hiyo wakiwa na askari polisi wengine ambao ndio walikusudiwa kutumika kusindikiza shehena hiyo hadi mgodini.

``Unajua ukweli wa mambo utajulikana mara baada ya shehena hiyo kufunguliwa na kukaguliwa kwani imeonekana kuwepo kwa hali ya kuficha mambo fulani fulani katika suala zima la upokeaji na usafirishaji wa shehena hiyo,`` alisema Ofisa mmoja wa usalama katika uwanja wa ndege wa Mwanza, ambaye hata hivyo aliomba jina lake lisitajwe.

Hata hivyo, baadaye Nipashe iliwasiliana tena na Olomi ambaye alisema kwamba zoezi la ukaguzi lilikamilika jana jioni na hakuna kitu chochote cha hatari kilichobainika katika shehena hiyo.

``Ni kweli tumemaliza ukaguzi muda mfupi uliopita, lakini hakuna kitu chochote cha hatari kilichobainika na wahusika wamekabidhiwa mzigo tayari kwa kuusafirisha kwenda North Mara Gold Mine chini ya uangalizi wa Polisi,`` alisema Olomi.

Bila kutaja ni vitu gani hasa vilivyobainika kuwemo ndani ya shehena hiyo, Olomi alisema kwamba kama kungekuwa na silaha za hatari wangeendelea kuushikilia mzigo huo.

SOURCE: Nipashe
 
Tatizo la kupokea Rushwa ni moja.

Unapokea kutoka kwa kila mwenye dau la kushiba bila kumwangalia usoni na kumtambua kwanza. Ni rahisi mno kwa mpenda rushwa kupokea rushwa kutoka mikononi mwa Ibilisi, kwani mpokeaji siku zote macho yake yako kwenye Burungutu.

Tunapokea Rushwa ili kuingiza Silaha Hatari?
Kama tumedhamiria kufanya hivyo ni bora tuache kujamiiana na kuongeza idadi ya watu. Kizazi cha pili kutoka kwetu kitarithi nini, kama si vurumai ya kujitakia?

Ukifuga mamba mtoto siku moja atakuwa Mamba mkubwa na kukugeuza Side Dish.
 
Kama mgambo wetu wa halmashauri wanaopewa mamlaka ya kuondoa machinga badala yake wanawanyan'ganya bidhaa zao bila ya kuwapeleka mahakamani na bidhaa wanagawana. Mgambo hao wanaochukua rushwa kwa mama nitilie na kuwafumbia macho ili waendelee kuwauzia wananchi chakula maeneo machafu. Ni heri wa nje ambao wanaweza kuwa na nidhamu na kuweka miji katika hali ya usafi.
Tabia yetu baadhi ya watanzania ndio inayotufikisha pabaya. Sasa hivi kwenye duru za benki nchini kuna mawazo kuwa heri kuajiri vijana kutoka Kenya ambao wanafanya kazi kwa bidii na sio wezi. Na kwamba vijana wetu wanapoajiriwa benki akili yao ni kufikiri namna ya kuiba.

tatizo la wizi au hiyo tabia inajengwa na akina kingunge ngombale na wenzake, sasa ili wengine wasiachwe mbali nao wana fisadi wanapoweza
 
Watu kama hawa wakina Olomi ndio wanaoimaliza nchi. They don't care. They don't even think. Sasa anasema amemaliza ukaguzi bila ya kusema kilichokuwepo. This is immaturity of the highest order! Ingekuwa mimi, hata kama nimevuta mshiko, ningeorodhesha vifaa vichache - just to brainwash spectators. Sasa Bw. Olomi kakagua mzigo lakini hataki kusema kilichopo.

Sijui hawa watu wanaajiriwa kwa vigezo gani. And most of the civil servants are like that. Kazi kwelikweli....
 
`Shehena ya Barrick ilikuwa na mabomu`

2008-12-20 14:41:55
Na Grace Chilongola, Mwanza

Ukaguzi uliofanywa kwenye shehena ya kampuni ya dhahabu ya Barrick Tanzania, iliyozuiliwa kwa muda katika uwanja ndege wa Mwanza imebainika kuwa ni mabomu ya kurushwa kwa mkono na yale ya kutoa machozi pamoja na risasi.

Ukaguzi huo ulifanywa kwa kushirikisha Jeshi la Polisi, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Usalama wa Taifa pamoja na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Katika mahojiano na waandishi wa habari ofisini kwake, Meneja Forodha wa TRA Mwanza, Leopold Kihumo alisema wao kama TRA baada ya kupata taarifa ya shehena hiyo waliikabidhi polisi kwa ajili ya utaratibu wa ukaguzi.

``Shehena kama hizo zikiingia TRA (forodha) huwa hatujiridhishi peke yetu na badala yake tunashirikiana na taasisi nyingine kama za jeshi la Polisi, JWTZ na Usalama wa Taifa,`` alisema.

Kwa mujibu wa Kihumo shehena hiyo iliyokuwa ifike Desemba 5, ilichelewa kuondoka kwa ajili ya kuvipa nafasi vyombo vingine kufanya ukaguzi na kwamba ilikuwa na uzito wa tani 1.4 ambapo ililipiwa kodi inayofikia Sh. Mil 144.

Kihumo alisema shehena hiyo ilitumia taratibu zote za kuombewa kibali na ndio maana baada ya kujiridhisha na ukaguzi iliruhusiwa kuendelea na safari.

``Shehena kama hii huwezi kuiacha ikaingia mtaani bila kukaguliwa na ndio maana walishirikisha vyombo vingine na walipojiridhisha Kamanda wa Polisi aliruhusu viendelee na safari na kutoa polisi wanne kwa ajili ya kusindikiza,`` alisema.

Hata hivyo, alisema baada ya ukaguzi walipendekeza shehena kama hizo ziwe zinaagizwa na wakala wa serikali wanaojihusisha na silaha na sio mwekezaji.

Naye Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Khamis Bhai alisema taarifa aliyopewa asubuhi na Afisa Upelelezi wa Mkoa, Agustine Olomi alimweleza shehena hiyo ilikuwa na baruti za kulipulia miamba.

Gazeti hili liliripoti kuwepo kwa shehena inayosadikiwa kuwa na baruti za kupasulia miamba, risasi na mabomu ya kurusha kwa mikono na yale ya kutoa machozi mali ya kampuni ya Barrick imezuiliwa kwa muda katika uwanja wa ndege jijini Mwanza kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kina kubaini vitu vilivyomo.

Wakati huohuo, Simon Mhina anaripoti kuwa kampuni ya Barrick imesema mzigo wake uliodaiwa kukamatwa mjini Mwanza haukuwa na silaha.

Akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam jana, Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Teweli Teweli, alisema Barrick haina sababu zo zote za kusafirisha shehena kama hizo kwa vile hazitumii katika shughuli zake za uchimbaji madini.

Akifafanua, alisema hivi sasa walinzi wake hawaruhusiwi kabisa kutumia risasi za moto, na ndio maana hata mgodi wake ulipovamiwa hivi karibuni na wakazi wa Tarime walilazimika kukimbia.

``Shehena yetu haikuwa na mabomu wala risasi, hatuna sababu yo yote ya kuagiza vitu hivyo,`` alisema.

Gazeti linaripoti kulikuwa na silaha au hakuna ? Hata sielewi makorokosho yaliyomo kwenye hii ripoti.
 
Back
Top Bottom