TRA valuation system ya magari haiko fair

Sasa Ku bargain watakutolea zaid ya $1000? Nani Ana muda wa kuja kuchoreshana hapo kwa $200? au mnasema tu mradi mnasema... Hampo fair bhana
 
Mkuu humu kuna watu wazima kabisa wanakaribia kustaafu maisha. Bado wanatembelea gari za shemeji. Usipoteze muda kubishana. Hayo uliyoyasema mi yamenikuta mara mbili mara ya mwisho nidhani bora nipitishie gari znz nilikoma
 
Kwanza ninakupa pole lakini ninadhani kabla ya kuanza process ya kuagiza gari [baada ya kupata all specs] ungeenda TRA wakakufanyia provisional est ambayo ingekuwezesha kufanya maamuzi sahihi.
 
Hii ya TRA ni hatari balaa juzi mi niliwauliza gari Toyota Land Cruiser Prado ya 2002,4200cc nikaambiwa kodi ni sh milioni 19.6 hapo nikabroo mapigo,nikasema ngoja waendelee kuagiza wenye pesa
Hapa kazi tu!!
Ninadhani wanachokifanya ni wanachukua thamani ya hiyo gari kama ikiwa mpya halafu pengine wana consider depreciation value na thamani ya mwisho ndiyo huichukulia kama kigezo cha kodi stahili
 
Wee kiazi kweli unayajua magari au unasikia kadanganya nin huyu jamaa was post ,unafikili tunavotumia magari sisi bongo na wenzetu wanatumia hivo?kuwa na km hizo mbpna possible uliza kwanza kabla hijakoment
 
Mkuu achana na hiyo kiazi hajui magari
 
Ninadhani wanachokifanya ni wanachukua thamani ya hiyo gari kama ikiwa mpya halafu pengine wana consider depreciation value na thamani ya mwisho ndiyo huichukulia kama kigezo cha kodi stahili
Duh,sasa sisi wenye vipesa vya madafu hatutomiliki gari aisee,kama kodi ni kubwa kuliko thamani ya gari!!
 
Ndiyo hivyo umeibiwa Volvo iliyotembea km 30 000 haiwezi kuuzwa bei hiyo, na ndiyo maana umepigwa uchakavu, dola 4000 ni gari iliyotembea zaidi ya km 100 000 !
Cha ajabu nini? Gari inaweza ikawa hata ya mwaka 1998 na ikawa na kms hizo. Hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya mwaka wa kutengenezwa na kms inazotembea
 
Inaezekana huyo ni mfanyakazi wa tra na calculations hizo za ajabu ndivyo wanavyoagizwa wafanye!
 
Ninadhani wanachokifanya ni wanachukua thamani ya hiyo gari kama ikiwa mpya halafu pengine wana consider depreciation value na thamani ya mwisho ndiyo huichukulia kama kigezo cha kodi stahili
Ndio hivyo wanavyofanya. Na wmefanya hivyo kwasababu ya ujanja wa kibongo bongo kuzidi. Walipokuwa wana-calculate kwa kutumia bei ya manunuzi watu wakajiona ni wajanja, hivyo mtu akinunua gari kwa mfano dola 4000 anaongea na muuzaji anamwambia aandike 600 ili ushuru upungue. Hivyo ikabidi sasa watumie bei ya lile gari na model linapokuwa jipya halafu wanafanya depreciation kulingana na miaka gari lilivyotumika na kupata common price kwa magari yote yanayofanana. Huyo jamaa mwanzisha thread alikuwa bado anadhani zinatumika kanuni za zamani.
 
Ninadhani wanachokifanya ni wanachukua thamani ya hiyo gari kama ikiwa mpya halafu pengine wana consider depreciation value na thamani ya mwisho ndiyo huichukulia kama kigezo cha kodi stahili
Na hiki ndicho kinachofanyika.
Kwa hiyo hata ukija na gari umeuziwa Tsh elfu hamsini.. hawata deal na hyo invoice yako watatumia bei elekezi (ya kwenye calculator).

Ila iwapo utajiloga ukaleta invoice kubwa kuliko bei ya kwenye calculator, hawa hapa TRA watafata hiyo invoice na kuacha bei ya kwenye calculator katika kukokotoa kodi..

kwa maana ingine watatumia bei ambayo itakua kubwa kati ya invoice na bei elekezi (bei ya kwenye TRA calculator).
 
hapa suluhisho ni kutafuta jopo la wanasheria wa kodi wapambane na sheria na hiyo kalukuleta kandamizi. pia TRA watafute namna ya kuhakikisha watu hawachakachui hiyo CIF. haiwezekani waumize wananchi wengi kwasababu watu wachache walikosa uaminifu. kuna chama kinaitwa cha kutetea abiria, tukichangie pesa kitafute wanasheria.

pia tujiulize nchi nyingine za Africa zinafanyaje.
 
Mfumo huu kwangu umesaidia sana kufahamu kodi ya kulipa kabla ya kuagiza gari...na ni mfumo rafiki ukilinganisha na ule wa awali...kinachotumika ni retail selling price ya gari(bei yake ikiwa mpya)halafu wanatoa uchakavu kwa utaratibu huu gari la 2013 itakuwa na kodi kubwa kuliko ya 2006 kwa sababu haijatumika sana..
 
mwenye mawasiliano na hicho chama atupatie tuwauzie hiyo biashara hawa tra wameshatuchosha sasa,
 
iweje invoice ikiwa kubwa kuliko bei elekezi wanatumia invoice? na hiyo tozo ya reli ya kazi gani? wakati hilo gari litakuwa linatumika kwenda kazini na kurudi tu, tena hapahapa dar es salaam, cha ajabu hizi kodi sijui wanazifanyia nini! barabara za kwenda majumbani kwetu ni mbovu mno wala hawajali kama unalipa kodi katika kulitumia hilo gari.
 
Sheria ya kodi kwenye ushuru wa forodha inaelezea mambo ya kuchukua bei kubwa pale unapofanya makadirio sikumbuki ni kifungu cha ngapi lakini ni kwenye sheria ya ushuru wa forodha..railway development levy ilianza mwaka 2015 na kupitishwa na bunge letu tukufu kodi hii imeanzishwa mahsusi kwa ajili ya kuboresha reli nchini mwetu kuhusu matokeo ya kodi inayokusanywa kwakweli sijui..
 
Hili la reli unanichanganya, tunajenga reli kwa kutumia mkopo wa exim bank china na hiyo reli inatakiwa ijiendeshe kibiashara iweze kurejesha mkopo, sasa unapokusanya tozo kwa wenye magari kwa ajili ya reli huo ni uonevu kabisa, niambie mkazi wa kinondoni anayefanya kazi azikiwe reli inamhusu nini? kama tumeweka kodi ya uchakavu ili watu wasilete gari kukuu mbona gari mpya bado inakodi kubwa kuliko hiyohiyo kukuu!
 
Yes. Hata mimi nimeshuri hivyo. Kwamba siku hizi ni muhimu kukokotoa kodi jinsi itakavyokuwa kabla hujaagiza gari. TRA Calculator inapatikana online.
ubaya wake pale kwenye CIF ya TRA sio blank hivo ukinunua zaidi yake imekula kwako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…