TRA valuation system ya magari haiko fair

Haya mambo ni hapa bongo tu, nchi yeyote duniani hakuna hicho kitu unaingiza gari ushuru unazidi fedha uliyonunulia gari,fedha ya usafiri,insurance na ukaguzi gari mara mbili au hata tatu, sijui hata inakuwaje nilitaka gari nililoagiza kuwapa mashirika ya dini kwasababu ya uhuni kama huu.
 
In
Kuagiza gari kwa sasa ni kama anasa.....kwann wasipunguze ili watu wengi waagize, hapo wata pata kodi nyingi, mafuta, kodi ya barabara, bima, na kodi nyinginezo.....sasa kubana hivi manake nn
 
Mie naona serikali ndo imetengeneza hayo Magari...

Km mtengenezaji anauza 9mil we kodi 15 mil huu sio uzalendo. Pia its turning our people into poorness...
Ungeandika kwa Kiswahili ungekuwa sahihi na kueleweka zaidi
 
Mie naona serikali ndo imetengeneza hayo Magari...

Km mtengenezaji anauza 9mil we kodi 15 mil huu sio uzalendo. Pia its turning our people into poorness...
Yaani waliotengeneza wanauza milioni 10, huyu aliyekaa Dar anadai inauzwa milioni 24! Kwa vigezo vipi? kwa nini wasitafute taarifa za ukweli kutoka kwa hao wauzaji wenyewe? Na kwa vile serikali yetu inachapa kazi barabara, hakuna mtu mwenye haki ya kulalamika. Labda wale wenye nembo ya kijani wakionyesha rangi wanapata valuation halali.
 
Kama una hela na una muda wa kubishana nao Lodge an Appeal letter to TAX TRIBUNAL APPEAL COURT. Lipa amaount ambayo haiko kwenye doubt (i.e. Tshs 6m), kuzuia penalty au lipa yote na umiliki chombo chako. Then file an appeal to TRA commissioner for unfair Tax assessment. Omba re-assessment na reason tumia unfair tax assessment as compared to Vehicle's CIF. Utarudishiwa change yako mkuu na utakuwa umesaidia wengi, make wanaweza kurevise the whole Formula.
 
Wanapigia hesabu kwa bei ya gari ilipouzwa ikiwa brand new then wanatafuta depreasion. 2009 ina miaka sita tu. Gari za ulaya zina bei kubwa zikiwa mpya na ziko kwenye category ya gari za starehe na ni kitu ambacho ni kweli. Hakuna mteremko hapo. Lipa tu. Ungetaka ungenunua corola ya mwaka huo.
 
Hakuna gari la ulaya la saizi hiyo linauzwa millioni kumi. Kama tu hujawahi kumiliki gari la ulaya utaweza kuyasema hayo.
 
Ndiyo hivyo umeibiwa Volvo iliyotembea km 30 000 haiwezi kuuzwa bei hiyo, na ndiyo maana umepigwa uchakavu, dola 4000 ni gari iliyotembea zaidi ya km 100 000 !
Mkuu haya magari ni mitumba..sasa hakuna formula ya bei za mtumba...unauza bei unayotaka kulingana na uhitaji wako wa pesa au uhitaji wako wa kutokaa na kitu ambacho hukitumii...so inawezekana tu hizo paticulars zikawa sawa na bei pia ikawa sawa, usijastifai kuwa jamaa kapigwa.
Hata masuala ya kilometa, ni inategemeana tu na matumizi ya mwenye gari..assume seller ana gari 4 na zote anazitumia intachenjibli..halafu hana shantingi nyingi
 
calculator hii ni sawa kutumika kwa sababu inasaidia kupata thamani halisi ya gari wakati unanunua (Baada ya kutoa uchakavu) toka mwaka limetengenezwa.

Ndiyo maana gari model flani la mwaka mmoja ushuru wake ni constant..
Otherwise kila mtu angeleta invoice yake.. wewe utasema umenunua USD 1000 mwingine atasema USD 600 Mwingine invoice inasoma Dollar 50 gari la aina moja na mwaka mmoja. Ingekua tafrani. Ndo maana wakaeka hyo calculator. Kwamba watu wote watozwe kodi sawa kwa gari la model sawa na mwaka sawa.

Tatizo pekee hapa ni hizo rate(%) za kodi kuwa kubwa.. Labda "private car" inachukuliwa kama luxury good.. Kama vile ilivyo bia au sigara.
 
Ni hatari tupu
 
Ukiwauliza watakachojibu ni kua Pale Kwao Ni Kazi Tu, huu msemo ukiongeza na ule wimbo wa kuisoma namba unatamalaki sana kipindi hiki.
Kabla ya kulipa kodi agent wako huwa anapewa nafasi ya kufanya makadilio.baada ya kufanya makadilio ya kodi anapeleka Tra .tra wao wanafanya makadilio yao baadaye agent anapewa akubali au akatae Tatizo maagent hawanaga muda wa kubagein wanakubali tu ili walipwe chao pole sana hukuomba kupunguza bei kupitia agent wako
Dah, mimi ndio kabisa sielew, labda Kodi hiyo ingetumika kutoa incentives kwa kiwanda cha kutengeneza magari ningeelewa, ila hata kagari ka $300, unakapata kwa >10M.....
Unazungumziaje uchakavu wakat huna viwanda??
 
Na kwa mujibu wa kodi huwa wanaangalia historian ya Gari yaani mwenzako wa mwisho alilipa sh ngapi
 
hatuna kiwanda cha magari sasa iweje gari jipya liwe na kodi kubwa kuliko gari la zamani? sasa kuna haja gani yakuwepo kodi ya uchakavu? hapa sio bure ni mambo ya kijinga tu, haya mambo yaliletwa na kale kazee kanakonyea ndoo. Kichekesho ni kwenye malori, unanunua lori kukuu mil 12m unakutana na kodi ya 50m bila kujali hilo lori ni capital goods litaendelea kulipa kodi na utaajiri madereva mataniboi na wapiga debe.

Kwa ajili ya haya mambo ya hovyo nchi nzima imeenea vicastal ya kopo ist passo virtz premio, ukipata nacho mzinga kinajikunyata kama mfuko wa rambo uliotupiwa kwenye jiko la mkaa. Magufuli hebu ayapige bei mashangingi yote ya serikali kila mtu atumie gari binafsi nao waonje adha ya kodi hizi za hovyo hovyo.
 
Tatizo pekee hapa ni hizo rate(%) za kodi kuwa kubwa.. Labda "private car" inachukuliwa kama luxury good.. Kama vile ilivyo bia au sigara.

Probably Yes

Kwa siku hizi gari ni kama kitu cha lazima...its not luxury anymore
 
haya mambo yaliletwa na kale kazee kanakonyea ndoo


Kumbe ilikuwa kipindi cha Kitilya? Ajabu sana hii

It doesn't make sense at All

No wadays wameweka Railway Levy...sasa Sijui railway Levy inamhusu nini mwenye gari?

Hizi ni kodi za kukomoa

Kodi yoyote inapaswa isiwe ya kukomoa
 
Sio magari tu bidhaa nyingi ukileta unapewa assessment ya ajabu. Mtu umeleta mzigo wa biashara ambao ni obvious umenunua at wholesale price, customs officer analeta assessment mara tatu ya invoice yako, ushahidi wake eti ameangalia market price Ebay!

Sasa ukiwa na assessor aka customs officer mwenye akili na upeo huu unategemea nini?!

Customs officer ana mentality kila anaeleta bidhaa kashusha bei. TRA bado kuna kazi kubwa sana.
 
Hyo ndo Tra,nadhan wanazuia kila mtu kuwa na gar.
 
Kumbe ilikuwa kipindi cha Kitilya? Ajabu sana hii

It doesn't make sense at All

No wadays wameweka Railway Levy...sasa Sijui railway Levy inamhusu nini mwenye gari?

Hizi ni kodi za kukomoa

Kodi yoyote inapaswa isiwe ya kukomoa
Haya ndio mambo ya jabu sana, pesa ya kujenga reli tumekopa exim bank china, kwanini sasa tuwekeane kwenye kodi ya gari? passo na reli wapi na wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…