TRA, tazameni mlivyoniongezea umaskini

GreenCity

JF-Expert Member
May 28, 2012
5,620
4,265
Wiki iliyo pita nilijibana kumwezesha dogo afanye hiyo interview lakini it backfired against me! Ifuatayo ndio budget :
1. Nauli - Tunduma ~Dar~Tunduma = 86,000/=
2. Malazi - siku 2= 30,000 /=
3. Chakula 10,000/day x3days= 30,000/=
4. Calculator - 15,000/=
5. Passports size - 4,000/=
6. Nauli za dala dala-10,000/=
7. Matumizi njiani - 30,000/=
8. Pesa ya sintofahamu - 35,000/=

Kwangu hiyo ni pesa mingi aisee!
Baada ya dogo kufika, akaniambia "Kaka hapa tupo kama buku nane hivi" nikaishiwa pumzi, nikamwambia dogo achana na hiyo interview rudi "boda", lakini dogo akasema, lazima afanye as long as ameshatumia Nauli.

Sasa nyie TRA hivi mngeita watu 500 au 600 mngekosa wenye sifa?

Hivi mna maslahi gani kuita watu zaidi ya 11,000 wakati ajira inahusu watu 300?

Je,kwanin mkawaambia wasailiwa majibu yanatoka ndani ya saa 24! (kusahihisha mitihani 11,000 kwa mkono na kupanga matokeo hadi kubandika ndani ya saa 24? That's amazing speed!

Kinachoniumiza zaidi huyu dogo alikuwa day worker somewhere hapa mpakani, boss wake ashaweka mtu mwingine baada ya dogo kushindwa kurudi ijumaa!

Sasa mmeniingizia gap la 260,000 Tsh for no good reasons! Huyu dogo amerudi na anaendelea kuzunguka na bahasha! kwa sababu ya "uzembe" wenu!

Binafsi Nimetumia muda mwingi kufuatilia updates za viji posts vyenu kwa mitandao kumbe ni bure kabisa!

Naziomba taasisi zingine zizingatie haya malalamiko ya wengi kwani naamini wapo walioumia zaidi yangu!

Mwisho niseme tu "hii serikali HAIJIHESHIMU na tumefika hapa kwa udhaifu wa SERIKALI hii hii!"
 
Ndo tanzania yetu hiyo mimi nimewahi kufanya interview nao mara mbili bila mafanikio watu wanakuwa nyomi hata nilivyoona tangazo lao la kazi hzo waliyofanya interview majuzi nikapotezea kuhofia nauli yangu kupotea bure bora wangekuwa wanafanya kikanda kama utumishi.
 
kweli ni changamoto ila mwache dogo apambane tu as long as wanahitajika watu anaweza kuwa kati ya hao 300!!
 
Tra
Udom
Nssf
Tanapa
Tbs
Nk
Interview za aina hii zipo sana! sina hamu nao!
 
Pole sanaa mkuu...adhabu yao unayo mikononi mwako...hakikisha unajiandikisha kwa uchaguzi ujao...

Nasikia kawe-dar wameanza kuandikisha ktk daftari la kudumu..lakini wametoa wiki moja mpaka trh 21 dec, kama ni kweli basi njama ya ccm itafanikiwa maana vijana wengi mda wa wiki ni ngumu kutokana na kuhangaika na maisha

Lengo lao ni kupata wamama wanyumbani na wazee....tafadhari kijana wa kitanzania wewe ndo unayo hatima ya maisha yako ya 2016 kwa kuleta mabadiliko, jiandikishe mda ukifika
 
Ndo tanzania yetu hiyo mimi nimewahi kufanya interview nao mara mbili bila mafanikio watu wanakuwa nyomi hata nilivyoona tangazo lao la kazi hzo waliyofanya interview majuzi nikapotezea kuhofia nauli yangu kupotea bure bora wangekuwa wanafanya kikanda kama utumishi.

Ni shiida ndugu, ule uharaka wa kutoa majibu ndani ya siku moja kwa wasailiwa zaidi 11,000 sijauelewa kabisa. Uenda na Mimi ikawa mwisho kuomba kazi kwao maana naona hizi gharama tunazotumia ni kheri tuzifanyie shughuli nyingine khaaaa!!!
 
Pole sanaa mkuu...adhabu yao unayo mikononi mwako...hakikisha unajiandikisha kwa uchaguzi ujao...

Nasikia kawe-dar wameanza kuandikisha ktk daftari la kudumu..lakini wametoa wiki moja mpaka trh 21 dec, kama ni kweli basi njama ya ccm itafanikiwa maana vijana wengi mda wa wiki ni ngumu kutokana na kuhangaika na maisha

Lengo lao ni kupata wamama wanyumbani na wazee....tafadhari kijana wa kitanzania wewe ndo unayo hatima ya maisha yako ya 2016 kwa kuleta mabadiliko, jiandikishe mda ukifika
Mimi huwa nina waadhibu miaka yote, na juzi Nimefurahi kuona dogo nae akiilaumu TRA kumkosesha nafasi ya kupiga kura kwa interview yao feki!
 
Nadhani tra (serikali)walikuwa wanakusanya taarifa za watu na sijui kwa malengo gani??......kwa nini walichukua passport-sized photos za watu at that very early stage????
 
Back
Top Bottom