Wiki iliyo pita nilijibana kumwezesha dogo afanye hiyo interview lakini it backfired against me! Ifuatayo ndio budget :
1. Nauli - Tunduma ~Dar~Tunduma = 86,000/=
2. Malazi - siku 2= 30,000 /=
3. Chakula 10,000/day x3days= 30,000/=
4. Calculator - 15,000/=
5. Passports size - 4,000/=
6. Nauli za dala dala-10,000/=
7. Matumizi njiani - 30,000/=
8. Pesa ya sintofahamu - 35,000/=
Kwangu hiyo ni pesa mingi aisee!
Baada ya dogo kufika, akaniambia "Kaka hapa tupo kama buku nane hivi" nikaishiwa pumzi, nikamwambia dogo achana na hiyo interview rudi "boda", lakini dogo akasema, lazima afanye as long as ameshatumia Nauli.
Sasa nyie TRA hivi mngeita watu 500 au 600 mngekosa wenye sifa?
Hivi mna maslahi gani kuita watu zaidi ya 11,000 wakati ajira inahusu watu 300?
Je,kwanin mkawaambia wasailiwa majibu yanatoka ndani ya saa 24! (kusahihisha mitihani 11,000 kwa mkono na kupanga matokeo hadi kubandika ndani ya saa 24? That's amazing speed!
Kinachoniumiza zaidi huyu dogo alikuwa day worker somewhere hapa mpakani, boss wake ashaweka mtu mwingine baada ya dogo kushindwa kurudi ijumaa!
Sasa mmeniingizia gap la 260,000 Tsh for no good reasons! Huyu dogo amerudi na anaendelea kuzunguka na bahasha! kwa sababu ya "uzembe" wenu!
Binafsi Nimetumia muda mwingi kufuatilia updates za viji posts vyenu kwa mitandao kumbe ni bure kabisa!
Naziomba taasisi zingine zizingatie haya malalamiko ya wengi kwani naamini wapo walioumia zaidi yangu!
Mwisho niseme tu "hii serikali HAIJIHESHIMU na tumefika hapa kwa udhaifu wa SERIKALI hii hii!"
Pole sana mkuu!, naona km ni mm vile. Yaani siku hizi kazi ipo, hata mm kuna watu wananipigia simu kuwa niende lakini nikiwauliza mmetuita wangapi? kuna dada mmoja shilika fulani akanidanganya kuwa tumeitwa watano na nafasi ni moja nikamwambia mm huwa nikiona tumeitwa wengi sana huwa siendi "Naji-disqualified", nikafunga safari nikaenda cha ajabu nikakuta pipo kibao alafu session zilikuwa tatu, asbh, mch, & jioni. (Ila Mungu anisamehe; huyu dada aliyenidanganya namtafuta kwa upelelezi wa chinichini ili nimjue tupeane heshima mtaani,
ile nmeona watu nikafanya oral yao japo kwa hasira za yule mwehu aliyenidanganya kwenye simu kuwa tupo watano, na bahati mbaya nikakosa kazi).
Ila hawa watu wajirekebishe!, wajitahidi wawe wanaweka interview zote mbili one day, mbona inawezekana sana tu!, usahishaji wa interview zote mbili unaweza ukaendelea baada ya watu kutawanyika. Kwanza watakuwa wanasahisha rough sana hawa, nmeona huu mchezo umeanza hata kule utumishi wameanza kusahisha siku moja, hivi wanasahishaje kwanza!
Hayo mambo yenu yaangalieni vizuri!