kuna jama alinunua gari landcruiser kilimo kwanza jipya uarabuni kuulizia ushuru kaambiwa milioni mia na zaidi, ikabidi aliinue matairi yakawa juu akakanyaga accelerator mpaka likasoma km kadhaa kuulizia ushuru upo chini ya mia akapakia na kulileta bongo.mbona ukinunua gari jipya kodi yake ni kubwa sana ukilinganisha na gari hilhilo ukinunua likuwa kuku?
Nunua pikipikiHawa jamaa wamepandisha ushuru wa kuingiza magari kumbe nao ni wizi tu. Unanunua gari mill 7 ushuru TRA unalipa mil 20. Huu ni uwendawazimu kabisa. Haiingii akilini.
nunua ule mwaka wa mwisho wa kikomo cha uchakavu yanni 2008 hapo umewaweza ila ukinunua la 2009, 2010 utaambiwa value kubwa daa nchi hii shida sana.Wasanii tu hawa. Ukinunuwa gari kongwe wanakwambia lina uchakavu, ukinunuwa mpya wanaipandisha thamani. You cant win!
TRA Wezi kabisa
Ni watu wangapi wa kawaida wanaweza Kumudu kununua gari jipya?Lawama kubwa ziende kwa wabunge especially wa ccm (ndo kwa wingi wao)wangeweza kabisa kuzuia dhuluma hii ovu.TRA tunawalaumu bure,wanatekeleza sheria.
Ilikua ya mwaka gani?
Otherwise tuanze kupitishia mombasa tu sasa.
Tatizo mnanunua magari yaliyo 'hoza' sasa!!!
ndugu yangu kuna jamaa alinunua escudo new model mil 15 kodi ikaja mil 30
Umenichekesha, hivi hayo magari yalikuwa yanatoka nchi gani?
Hilo sio siri silifahamu ila kama ni body appearance nikiliona nitakumbuka utotoni maana nilikaa Upanga karibu na Garage ya Mzee Rupia kulikuwa na Magari ya kizamani ya kila aina hadi Raha...
Nakumbuka Moris nadhani nayo yalikuwa yanakuja Mapya pamoja na Rolls Royce
Daah hio vintage collection yako ni ya ukweli sana bro,those old good days.
Mkuu ahsante to be honest they were really old good days usisikie.
Kuna mshakaji mmoja mtaani baba yake ana vw ya zamani sana kuna siku nilimuomba niitest, asee nilijihisi kweli naendesha Gari kwanza ukikaa kwenye kochi hakuna yale mambo ya leather seat, ukiingiza Gia inakua ngumu flani hivi, ukikata kona Unajisikia kweli umekata sio haya ya siku hizi unakata kona na kidole kimoja ,niliipenda sana radio ya ile Gari!Thnxs sana mkuu kwa kumbukumbu hizo Safi
Majambazi.., maana wezi ni kuwashusha daraja. Hawa jamaa hizo kodi zao zinatuhusu sie walalahoi! Jamaa wanaoingiza kontena zaidi ya elfu mbili bila kuzilipia kodi wao sijui watanzania wenye kitu gani cha zaidi yetu sisi!
Umeona mkuu, halaf mtu katoka dar kenda zanzibar kununua tv na dvd na cattle fridge kwa matumizi yake na familia yake akifika port dar anadaiwa ushuru, tena kama tv ulinunua laki 2 utalipia ushuru laki 3 kama sio wizi ni nini?
Pale port wamekuwa na njaa kama fisi, yaani usije ukapita na hata na kijiko, hujaleta gari hapo.
Mi kinacho nishangaza show room gari ni rahisi kuliko kwenda Japan au kuagiza gari Japan na kugharamia mwenyewe.
Kwa nini.?