Tra na usanii wa aptitude test

Sendeu

Member
Jun 29, 2009
59
2
Nikiwa miongoni mwa wadau waliofanya kinachoitwa aptitude test ya TRA iliyofika Mzumbe Dar Campus nitoe machache ambayo yanaonyesha wazi kuwa nchi hii hakuna haki yoyote inayotendeka au itakayotendeka mpaka tubadilike kifikra na kimtazamo.
Baadhi ya yaliyojitokeza ni na yanayotia aibu taasisi km TRA na Chuo cha Mzumbe ni:
1.Baadhi ya candidates kupewa barua mbili za post tofauti na kupangiwa tarehe na siku tofauti za kufanya test ambazo maswali mengi yalikuwa yakijirudia kwa maana hiyo basi uwezekano wa mtu kufaulu kisanii ni mkubwa kwani atakuwa aware na test ambayo in short ni kama pepa ILIYOVUJA. AIBU ISIYO NA MFANO KWA MZUMBE NA TRA!!!!
2.Baadhi ya candidates ambao hawana sifa zilizotajwa kwenye tangazo la kazi kupewa nafasi ya kufanya test na pia kuchaguliwa for ORAL interview huku wakiwa hawana hata PROVISIONAL RESULTS za vyuo vyao kwa kweli ni aibu na ni UFISADI WA KUPINDIKIA KWA MAENDELEO YA WATANZANIA
NAWASILISHA
 
Hivi takukuru hawawezi kuchunguza swala kama hili? Wanaweza fanya kitu kinaitwa "process review" ambapo wataangalia kama taratibu zinatoa haki na usawa and things like that. Anyways trying to think loud.
 
Mdau Pole kwa yalokukuta...!!!

Kimsingi Public Institution zinaruhusiwa kuchukua graduates ambao wanasubiri matokeo yao ya mwaka wa mwisho...!!! unachotakiwa ni kuwasilisha matokeo ya mwaka wa 1 na 2 au 3 kwa kozi zenye zaid ya miaka 4......!!! kama kuna sheria inayokataza basi vema tujulishwe!!!

Ila pia watu walio ktk system ya Ajira sehem X, ndio wenye info ambao wana play na michezo ya kuwachukua wanao wataka.
 
Hao walikuja kuzuga tu hizo nafasi tayari walishaandaa watu
 
Hivi takukuru hawawezi kuchunguza swala kama hili? Wanaweza fanya kitu kinaitwa "process review" ambapo wataangalia kama taratibu zinatoa haki na usawa and things like that. Anyways trying to think loud.

Wakimaliza uchunguzi watasema ulikuwa huru na haki kama tume zetu za uchanguzi
 
Sasa na wewe Sendeu unasema ulikuwepo kny hiyo Aptitude tes....yet title yako unaonyesha kuwa ni tetesi....nani aje aconfirm zaidi ya wewe uliyeparticipate kny hilo zoezi?
 
pole sendeu,
endelea kutafuta kazi mahali pengine, mtu kuitwa interview kwa nafasi mbili tofauti kwa wakati tofauti ni jambo la kawaida, aidha kurudia kwa sehemu ya maswali haimwongezei mtu nafasi ya kushinda hiyo usaili. kuitwa zaidi ya nafasi moja inaingeza probability ya yeye kupata kazi toka TRA. ila kwa maswali kurudia haina msingi, swali laweza kuwa ni moja , lakini likawa linapima kwa kiwango tofauti- hii ikafanya marking scheme ikawa tofauti. labda tahadhari kwa wengine, tusichukulie maswali kiurahisi. ni kama unakwenda intetview saa saba mwenzio alikwenda saa nne asbui, hata akikwambia alichoulizwa waweza ukajikuta ukikosa kazi.
huenda kulikuwa na vimemo, na watu hawakuwa na sifa... lakini ni kwa kiwango gani tuna uhakika wa hilo???. mwisho wa siku TRA wangeajiri idadi ya watu waliotakiwa, kwahiyo lazima kuna watu wangekosa nafasi, sasa kama huna ushahidi, TRA watasema wewe unalalamika kwa kuwa umekosa. Kaza buti interviews zijazo, usikatishwe na TRA na Mumbe University
 
Naungana nawe kabisa, mie nadhani kama alifanya vizuri aweke hofu pembeni. Mie nina jamaa zangu kibao watoto wa wakulima walitoke kwenye apptitude na wengine wameshaacha wanahangaika na mengine. Mie nadhani asubiri matokeo.
 
Mdau Pole kwa yalokukuta...!!!

Kimsingi Public Institution zinaruhusiwa kuchukua graduates ambao wanasubiri matokeo yao ya mwaka wa mwisho...!!! unachotakiwa ni kuwasilisha matokeo ya mwaka wa 1 na 2 au 3 kwa kozi zenye zaid ya miaka 4......!!! kama kuna sheria inayokataza basi vema tujulishwe!!!

Ila pia watu walio ktk system ya Ajira sehem X, ndio wenye info ambao wana play na michezo ya kuwachukua wanao wataka.

Ninavyojua mimi public institutions hazichukua watu on the basis of provisional results.

TRA kila mtu anakimbilia na wakubwa wanaamini ni mahali pazuri pa kuweka ndugu zao. Kama huna mtu pale basi kupata kazi labda hiyo nafasi asiwepo mtu mwingine wanayemtaka wao,lakini nafasi zote nzuri lazima wapeane na wanao.

Tra huwa wanaweka vikwazo hata kama mtu una vigezo unakosa nafasi. Mfano watu walioitwa kwenye oral interview majina yalibandikwa tu ofisi za TRA ingawa awali walisema watatumia njia nyingine ambayo itakuwa rahis kwa watu kupata habari kama magazeti,kupiga simu nk.

Kwahiyo kama hukuwa na wazo la kupitapita TRA basi imekula kwako. Kuna watu wamerudi mikoani wakitegemea kupigiwa simu na majina yao yametoka. Kilichotokea ni kwamba wameshindwa kuhudhuria interview kwakuwa hawakujua kama wamechaguliwa.
 
Yaani pale TRA, hata kwenye ngazi ya U-Commissioner hamna haki pale. Kwa mfano baada ya kuisha kwa Muda wake Commissioner wa Excise and Customs department ilibidi waanze mchakato wa kumtafuta mtu wa kujaza nafasi hiyo. Ilibidi wawaajiri Deloitted (Auditing Company) kutafuta watu watatu. Deloitte ilifanya hivyo kwa kutumia professionalism na kutuma majina matatu kwenda bord ya TRA. Lakini cha kishangaza baadhi ya majina yalienguliwa haraka. Sasa Deloitted tulitumia vigezo vyote vya kimataifa kuwapata watua 3 ambapo mojawapo alipaswa kupitishwa na na TRA board na kupitishwa na Rais kua Commissioner. Lakini cha ajabu majini yalipanguliwa. Sasa kulikua na sababu gani kuwaajiri Deloitte hali unajua ni process tu? Hapa bwana kama hauko kwenye mkodo wa maji ni vigumu sana kupata maji utishia kuambulia matone tu. Ukicheza hata matone hupati. Mfumo baba. Kila mmoja anataka amuweke mwenzake. Shall we make? Je tutafika?
 
pole sendeu,
endelea kutafuta kazi mahali pengine, mtu kuitwa interview kwa nafasi mbili tofauti kwa wakati tofauti ni jambo la kawaida, aidha kurudia kwa sehemu ya maswali haimwongezei mtu nafasi ya kushinda hiyo usaili. kuitwa zaidi ya nafasi moja inaingeza probability ya yeye kupata kazi toka TRA. ila kwa maswali kurudia haina msingi, swali laweza kuwa ni moja , lakini likawa linapima kwa kiwango tofauti- hii ikafanya marking scheme ikawa tofauti. labda tahadhari kwa wengine, tusichukulie maswali kiurahisi. ni kama unakwenda intetview saa saba mwenzio alikwenda saa nne asbui, hata akikwambia alichoulizwa waweza ukajikuta ukikosa kazi.
huenda kulikuwa na vimemo, na watu hawakuwa na sifa... lakini ni kwa kiwango gani tuna uhakika wa hilo???. mwisho wa siku TRA wangeajiri idadi ya watu waliotakiwa, kwahiyo lazima kuna watu wangekosa nafasi, sasa kama huna ushahidi, TRA watasema wewe unalalamika kwa kuwa umekosa. Kaza buti interviews zijazo, usikatishwe na TRA na Mumbe University

Sendeu,
Kutafuta kazi ni kazi pia inahitaji ujuzi wa kutafuta. Zinapotangazwa nafasi za kazi hakikisha kuwa unaomba nafasi zaidi ya moja endapo unasifa za kufanya hivyo. Kwa kufanya hivyo unajiongezea nafasi ya kupata kazi ya kuajiriwa.
Lakini labda kubwa zaidi ni kwamba weka mkazo wa kuona ni namna gani unaweza kujiajiri wewe mwenyewe badala ya kufikiria wakati wote ni nani atakuajiri. Atitude hii itakusaidia kukuweka katika mtazamo tofauti wa maisha na pia itakufanya usifikirie kulalamika pale unapokosa kuajiriwa.
Afterall, kuna kazi nyingi tu Tanzania ambazo vijana hawataki kuzichangamkia, kama vile ualimu. Wengi wanafikiria kuwa akimaliza BCom pale mlimani ni lazima apate kazi TRA au BoT, no Shule za Msingi zinahitaji resources nzuri kama hizo za Mlimani na kwingineko.
 
Du mdau hapo juu umenichekesha sana, eti shule za msingi zinahitaji watu walomaliza bcom.
Anyway, ndo reality ya nchi yetu, yani kila kitu ni ujanja ujanja tu.
 
ukitaka kuajiliwa TRA bila mizengwe nenda kabadilishe jina lako uwe wale wanaotokea mlima mkuu kuliko yote Afrika kama hutoki huko
 
Back
Top Bottom