Tiba
JF-Expert Member
- Jul 15, 2008
- 4,604
- 3,163
Wadau,
Wiki iliyopita nilikwenda pale TRA Mwenge kulipia road licence. Nilipokewa vizuri na mabinti pale reception na baada ya kuwaeleza shida yangu, walinisaidia kujaza form zinazotakiwa na kunielekeza wapi niende kwa ajili ya kukadiriwa ni kiasi gani nilipashwa kulipia. Kulingana na CC ya gari nililokwenda kulipia road licence, gharama yake ni Tshs. 150,000. Cha ajabu yule binti aliniandikia nikalipie Tshs. 180,000 na nilipomuuliza kwa nini kiasi hicho akaniambia Tshs. 30,000 zilizoongezeka hapo ni kwa ajili ya fire inspection. Nikamuuliza hiyo fire inspection ni kitu gani na nani anafanya hiyo inspection. Akaniambia inspection inafanywa na watu wa fire ambao ofisi zao ziko pale Lumumba na akasisitiza kwamba nikija kuchukua hiyo road licence nitaona na kupewa maelekezo zaidi.
Bahati mbaya sikuwa na kiasi chote hicho hivyo nililazimika kuondoka kwenda kutafuta pesa zaidi ili niweze kulipia. Pamoja na usumbufu nilioupata kuipata hiyo road licence, bado sikupewa kitu chochote kinachoonyesha kwamba nimelipia hiyo fire inspection.
Kama kuna mwana JF anayejua hii kitu ya fire inspection inafanyaje kazi, naomba atufumbue macho.
Natanguliza shukrani.