Biashara na TRA

Ibrahimeliza

Member
Nov 25, 2020
37
26
Kuna kitu sijakielewa hapa, au hakipo sawaaa, ukitaka kuanzisha biashara lazima ufuate utaratibu wa kisheria mfano lazima uwe na tin na lesseni ya biashara husika, embu fikiria unataka kuanzisha biashara ya miamala ya kipesa imezoeleka kama tigopesa ili upate line za kazi hiyo lazima uwe na lessen ya biashara hiyo, process utaanzia tra kwaajili ya makadilio na kuhifadhi taarifa zako kwaajili ya hiyo biashara yako sio...?? Kisha utaenda manispaa/kata kwaajili ya lesseni kisichokuwa sawa ni hichi.

Ili upate line za kazi lazima uwe na lesseni na ili upate lesseni utapitia tra kwaajili ya kukadiriwa biashara ambayo hata haujaianza, utaulizwa eneo la biashara yako, unaingiza kiasi gani kwa siku, wafanya kazi wangapi, maswali kama hayo nawakati wewe unataka lesseni kwaajili ya kufuatilia line ili uanze kazi, au mimi kuna kitu sijakielewa.
 
Nadhani labda hujawaelewa. Lengo lao hasa ni kupata kodi zaidi na kodi hii ukumbuke utaanza kuilipa kabla hata hujaanza kazi. Kikubwa wakati unajieleza kwenye usaili wao hakikisha hauweki matarajio makubwa kwenye biashara yako ya kijasiriamali ili kupunguza mzigo ambao sio halisi. Baada ya hapo kama utaanza biashara na kukuta mambo ni tofauti hakikisha unawaandikia barua mapema sana kuwajulisha sio ukakaa unalalamika chini kwa chini.
 
Nadhani labda hujawaelewa. Lengo lao hasa ni kupata kodi zaidi na kodi hii ukumbuke utaanza kuilipa kabla hata hujaanza kazi. Kikubwa wakati unajieleza kwenye usaili wao hakikisha hauweki matarajio makubwa kwenye biashara yako ya kijasiriamali ili kupunguza mzigo ambao sio halisi. Baada ya hapo kama utaanza biashara na kukuta mambo ni tofauti hakikisha unawaandikia barua mapema sana kuwajulisha sio ukakaa unalalamika chini kwa chini.
Aiseee hapo kidunchu nimeanza kukuelewa kwamba lazima uwaongopee
 
Mimi sijasema uwaongopee mkuu😂😂😂😂😂 ila hakikisha unatumia akili na ukumbuke hayo ni MAKADIRIO hivyo yanaweza kuwa sawa na uhalisia au yasiwe sawa. Usiogope
Either niwapige au wanipige. Nahakuna anaekubali kupigwa
 
Karibu Tanzania. Hii ndio Tanzania jamaa yangu. Na mambo hayo yapo hapa tu. Na hayaeleweki eleweki. Hata wao wa mamlaka ukiwauliza sio hiyo tu mambo mengi yahusuyo kodi hawaelewi,wapo wapo tu.
Mfano ukimuuliza hiyo mtu wa TRA hawezi kukupa majibu yanayojitosheleza,utaruka ruka kama danadana,huku akijifanye hatambui maswala ya leseni.
Pia ukija kwenye kodi zenyewe siku hizi kuna utitiri wa kodi. Hasa baada ya kuingia huyu na mwiguru wake. Duka moja linaweza kuwa na leseni 6,mpaka 8. Unajiuliza hizi kodi zote kwa serikali moja wanashindwaje kuziunganisha?. Kibaya zaidi huyu anakukamua anajifanya hajui yupo mwingine wa kukukamua.
Hao wa leseni wamekuja na kitu cha kupuuzi kabisa service levy. Hii service levy mwanzo wake ni watozwe makampuni makubwa hasa wenye viwanda. Mfano kama watengeneza nondo, magodoro,kufua vyuma. Wale wenye kuchafua mazingira. Sasa kwa sasa kwa tamaaa tu za akina mwiguru,wametanua kwa sasa wameipeleka kwa yoyote mwenye duka. Muda mwingine inazidi hata ile kodi ya leseni kwa mwaka. Ukiwauliza wengi wanaohusika,nao hawajui chochote. Karibu Tanzania
 
Naje? Kama hukuandika barua yataarifa kua biashara imekua mbaya unafanyaje?
😂😂😂😂 nakumbuka kuna mwaka Mizengo Pinda akiwa bungeni aliwahi kusema; "...kama ukiambiwa ufanye hivi na wewe ukakaidi basi utapigwa... na mimi nasema wapigwe tu....".

Kiufupi ni kuwa utatakiwa kulipa kama report ya makadirio inavyosema. UTALIPA utajua wewe kwa kuotoa hiyo hela lakini kwa kuwa ilitokana na uzembe wako wa kutowajulisha basi nakuambia UTALIPA labda usije kufanya biashara kwa hiyo TIN yako
 
Unaanza kulipia wazo, mengine utajijua mwenyewe...
Hahahahhahaaaaaa aieseeee mpaka wazo unalipia yani wewe sasa nimekuelewa na naunga mkono, yani kifupi tanzania ukiwa na wazo la biashara lazima ulilipie unaanza kulipia wazo daaaaaaaah
 
Back
Top Bottom