TRA na malipo ya fire inspection - nini maana yake? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

TRA na malipo ya fire inspection - nini maana yake?

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Tiba, Oct 26, 2012.

 1. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Wadau,

  Wiki iliyopita nilikwenda pale TRA Mwenge kulipia road licence. Nilipokewa vizuri na mabinti pale reception na baada ya kuwaeleza shida yangu, walinisaidia kujaza form zinazotakiwa na kunielekeza wapi niende kwa ajili ya kukadiriwa ni kiasi gani nilipashwa kulipia. Kulingana na CC ya gari nililokwenda kulipia road licence, gharama yake ni Tshs. 150,000. Cha ajabu yule binti aliniandikia nikalipie Tshs. 180,000 na nilipomuuliza kwa nini kiasi hicho akaniambia Tshs. 30,000 zilizoongezeka hapo ni kwa ajili ya fire inspection. Nikamuuliza hiyo fire inspection ni kitu gani na nani anafanya hiyo inspection. Akaniambia inspection inafanywa na watu wa fire ambao ofisi zao ziko pale Lumumba na akasisitiza kwamba nikija kuchukua hiyo road licence nitaona na kupewa maelekezo zaidi.

  Bahati mbaya sikuwa na kiasi chote hicho hivyo nililazimika kuondoka kwenda kutafuta pesa zaidi ili niweze kulipia. Pamoja na usumbufu nilioupata kuipata hiyo road licence, bado sikupewa kitu chochote kinachoonyesha kwamba nimelipia hiyo fire inspection.

  Kama kuna mwana JF anayejua hii kitu ya fire inspection inafanyaje kazi, naomba atufumbue macho.

  Natanguliza shukrani.

  Tiba
   
 2. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,865
  Likes Received: 6,216
  Trophy Points: 280
  hiyo ni njia tu ya serikali iliyotukuka ya tz kula hela za walalahoi.... kila leo wanakuja na mbinu mpya za kumkamua mnyonge......

  Kidumu chama cha matajiri
   
 3. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2012
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,541
  Likes Received: 2,236
  Trophy Points: 280
  CCM inatafuta pesa ya kampeni 2015 kwani kwenye mifuko ya serikali hakuna kitu hadi watumishi wanakopwa!!hawapewi mishahara!!
   
 4. W

  Wimana JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 2,453
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 145
  Wizi mtupu, soon TRA watapoteza hata heshima walobaki nayo, watakuwa hawana tofauti na madalali wa Majembe Auction Mart na wengineo.
   
 5. R

  Rwechu Member

  #5
  Oct 26, 2012
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 85
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hata mimi nililambwa 180000 alafu hakuna cha ukaguzi wala nini.

  Na road licence niliyopewa haionyeshi chochote kuhusu fire inspection
   
 6. W

  Wakwetu Senior Member

  #6
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 157
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hao ni wahuni tu, tena washenzi kabisa.

  Unalipia road license yako kwa mwaka mzima, than unalipia hiyo fire inspection kisha ukienda zimamoto wanakupa stika ya fire ambayo nayo ni ya mwaka mzima. Cha ajabu na cha ushenzi hapa ni kuwa ile stika ya fire huwa ni ya kuanzia Julai,01 hadi 31june ya mwaka unaofuata.

  Kama road license yako inaisha 20 june 2013 ukienda kulipia wanakuambia ulipe na fedha za fire inspection kisha wanakupa stika ya tarehe 01/07/2012 - 31/06/2013 ina maana tarehe 1/7/2013 trafiki wanaanza kukusumbua stika ya fire na kukudai rushwa.

  Ndio maana nimesema tra wanafanya ushenzi na hiki kipengele cha fire inspection. Kwa nini wasitoe stika ya fire ya mwaka mzima kuanzia tarehe ya kulipi mteja kama ilivyo road license?????
   
 7. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2012
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kha huko ni 30,000 tu? Huku kijijini kwetu ni 40,000!

  Unajua sisi watanzania tuko kama tumelogwa! Haki ya nani tena hatuko sawa!

  Hivi ni watu gani wanakaa na kufikiria wizi kama huo na sisi tuko ka mazuzu tu (sorry kwa kutumia hii kauli kama itamkwaza mtu) na wala hatuhoji! Mimi nilitegemea kuwa ukishalipia hiyo 40,000 ukienda kuchukua road license yako unakuta na mtungi wako mpya unakusubiri. Kumbe ni fire inspection! Inspection of what?

  Pamoja na fire inspection, Pamoja na kuwa na fire extinguishers lakini tumeshuhudia magari mangapi yakiwaka moto bila kusaidiwa na hizo fire extinguishers zao! Siku hizi wamehamia kwenye maduka! Wanataka kila mmiliki wa duka awe na fire extinguishers. Mimi niliwauliza ina maana nikishaweka fire extinguisher inafanya kazi ya kuzima automatically ama ni vipi! Sisi saa hizo labda ni usiku! Itatusaidiaje?

  Nawaambia huu ni wizi wa aina mpya! Serekali inadaiwa na mifuko ya hifadhi za jamii mabilioni ya fedha! Wamehamia huku baada ya jaribio lao la kutaka kuzuia mafao ya mifuko ya hifadhi za jamii kwa wanachama hadi umri wa kustaafu utimie. Wamegeukia kwa wananchi! Na mpaka 2015 tutakamuliwa sana. kama yalikuwa yanatoka maziwa mwisho sasa tutaanza kukamuliwa damu.

  Ifike mahali tuseme sasa yatosha!

  MIMI NASEMA HUU NI WIZI WA KUTISHA KULIKO WIZI ULE WA EPA, MEREMETA, DOWANS, RICHMOND, KIWIRA, WANYAMA HAI KUSAFIRISHWA NJE, MACHIMBO YA MADINI and more you can name!

  SHAME ON THOSE WHO ARE INVOLVED WITH THIS. Iko siku! Ole wenu!
   
 8. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Hii inawezekana ikawa kweli kwani wenzetu wanaamini ukiwa tu na gari, basi wewe unazo pesa za kutoa bila mpangilio ili mafisadi wafaidi kwa nafasi zao!!!!

  Tiba
   
 9. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Mkuu huo ndio ukweli, hiyo fire inspection haijaonyeshwa popote kwenye hiyo road licence. Hivi hakuna mtu wa TRA hapa JF hatupe majibu? Ni nani anapashwa kufanya hiyo fire inspection?

  Tiba
   
 10. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Kwa hiyo hizi pesa wanazokusanya wanazipeleka wapi? Ni kwa ajili ya uchaguzi wa 2015 kama ulivyosema? Na mbona hatupewi chochote kuonyesha kwamba tumelipia hiyo pesa ya ukaguzi na kwamba twende tukakaguliwe sehemu fulani? Huu ni wizi wa mchana kweupe na serikali inapashwa ione aibu kwa kuendesha zoezi kama ili as if wana deal na dead bodies.

  Tiba
   
 11. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #11
  Oct 26, 2012
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Asante kwa ufafanuzi huu. Ina maana ukisha lipia road licence unakwenda fire wanakupa sticker ya fire!!!! Mbona hao mabinti pale TRA Mwenge hawawaelekezi watu what is supposed to be the next step? Je hiyo sticker inasaidia nini? Last time nilisimamishwa na traffic police kule Tarime na waliniuliza ni kwa nini sina sticker ya fire? Nilimwambia yule polisi kwamba nilitarajia aniulize kama nina fire extinguisher kwani nikiwa na sticker na gari ikashika moto hiyo sticker haitanisaidia kuzima huo moto.

  Kuhusu hilo la sticker kuanzia july hadi June, police akinikamata kwamba sijalipia baada ya June next year, itabidi tupelekane kasi tu.

  Wizi mtupu!!!!!!

  Tiba
   
 12. Head teacher

  Head teacher JF-Expert Member

  #12
  Oct 26, 2012
  Joined: Mar 10, 2012
  Messages: 1,811
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Serikali yetu hii imejaa viongozi mijizi. Mimi sioni kwa nini watu wanalipia fire extenguisher inspection za magari wakati TBS ilishakagua mitungi inayoingia bandarini na kuona inafaa. Huu wote ni wizi na hata risiti pale fire walikuwa hawatoi na wakitoa zinakuwa feki ambazo si za serikali. Aibu kubwa. Mimi nilidhani unalipia elfu 30,000 upewe mtungi mpya kila mwaka kumbe ni kwa ajili ya ushuzi. inauzi sana. Cha kushangaza zaidi magari yote yanatakiwa yalipiwe bima, sasa kazi ya bima ni nini. au kazi ya askari wa zimamoto ni nini, si ndio wamefundishwa kupambana na moto. Sasa serikali inanitaka niwe na fire extenguisha nani apambane na moto. Hii ni kuhatarisha maisha ya watu. Sisi hatuna ujuzi na wala hatujasomea kazi hiyo. Cha ajabu zaidi ni kwamba hili jeshi ni chombo cha serikali hivyo tunalipa kodi ili tupate huduma ya zima moto si bure tunalipia kwa kodi. Mkishindwa acheni gari liungue bima watalipa. Acheni ushenzi akina CCM. Tunalipa kodi ya asiliamia 100 kwa kila litaya mafuta tunayonunua hiyo inatosha kutupa huduma ya zima moto zaidi ya hapo ni uonevu.


  Hebu waza:
  Ukiwa na gari utalipia 1. Vehicle licence 2. Bima 3. Kodi ya mafuta na vipuri 4. Fire extenguisher inspection. 4. Rushwa kwa trafiki 5. Wiki ya nenda kwa usalama (...ni vituko) 6. Road notifications 7. ...

  Mtu anayemiliki gari Tanzania lazima awe tajiri kuweza ku-drive.....khaaaaaa....!!!!!!
   
 13. Uliza_Bei

  Uliza_Bei JF-Expert Member

  #13
  Oct 26, 2012
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 3,109
  Likes Received: 424
  Trophy Points: 180
  Huu ni wizi wa serikali ya CCM tujipange, hatuwezi kukataa kulipa lakini tunaweza kuwaondoa madarakani CCM 2015
   
 14. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #14
  Oct 26, 2012
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hiyo ndiyo Tanzania ndugu yangu, Kila sehemu watu wanajitafutia ulaji; hizo hela zinaishia kunenepesha wakubwa hapo Wizara ya Mambo ya Ndani ambayo imeanzisha kitengo kinachojitegemea cha jeshi la zimamoto na hela zote zinachukuliwa na hilo jeshi.

  TRA Mwanakula kamisheni ya ukusanyaji lakini kimsingi huo ni wizi ama unyang'anyi wa wazi kwani hakuna huduma yoyote inayotolewa na jeshi hilo kutokana na malipo. Wakati Masha akiwa waziri wa wizara hiyo alikataa kuidhinisha ukusanyaji wa malipo hayo kwani kimsingi madhara ama hasara inayotokana na ajali ya moto kwa chombo cha moto kama gari yanalipwa na bima.
   
 15. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #15
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Tatizo tunaishia kunungunika hapa tu na Jumatatu tunaenda kulipa kama kawa na jamaa wanachukua hiyo hela. Mambo ya Fire ni insurance inacover. Huu ni wizi mweupe lakini hamna anayefanya chochote kupeleka Serikali Mahakamani. No action no reaction.
   
 16. S

  Sometimes JF-Expert Member

  #16
  Oct 26, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 4,567
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 180
  Mimi nimelipia hiyo road licence miezi miwili iliyopita. Jamaa wa TRA walinionyesha maandishi ya kulipia hiyo fire. Imeandikwa kwa chini kwenye hiyo leseni. Inabidi uwe na macho makali ili uione! Kuhusu stika ya fire,nilionyeshwa barua inayofafanua kuwa siyo lazima na hazitolewi!
   
 17. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #17
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mangi, nimecheka hapa, mpaka nimekaribia kuugua. Mbavu hazina hali... yaani maandishi haya nimeyaandika baada ya kupata nafuu. HIYO NDIYO CCM ASIYEIJUA CCM, AANZIE HAPO. Ahsante sana, Mungu akubariki
   
 18. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #18
  Oct 26, 2012
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,167
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Fire inspection=inspection of fire= Ukagui wa moto.
  Unakaguaje moto? ****** yao! makalio yao!
   
 19. n

  nlambaa JF-Expert Member

  #19
  Oct 26, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 363
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huu ni wizi mwingine, mchana kweupe,kuna hitajika juhudi, wabunge wetu wasaidie katika kupinga hili, kwani insurance tunayokata ina cover moto pia.
   
 20. Johas

  Johas Senior Member

  #20
  Oct 26, 2012
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 141
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mkuu...! Naona keyboard yako ulikuwa unaicharaza kwa hasila..., kiukweli inakera.!
   
Loading...