TRA kwa hili mmekosea

TRA kwa hili mmekosea

ujamaajulius

Member
Joined
Jul 28, 2015
Posts
50
Reaction score
66
Sijui ni mimi tu, au na wewe umegundua hii, Unapotaka kukata leseni ya kuendesha gari unaenda TRA na baada ya kukata leseni hivyo hudumu kwa miaka mitatu. Kisha unatakiwa kuihuisha tena(Renew) lakini cha ajabu leseni mpya huanza upya kana kwamba hujawahi kumiliki leseni na hivyo kigezo cha uzoefu (experience) hupotea. Unapotakiwa kwenye interview ili uonyeshe una uzoefu wa kutosha sifa hiyo utaikosa. sasa sasa itaonyesha uzoefu wa miaka miwili na kidogo hivi.

Nadhani ni wakati muafaka wa TRA kurekebisha hilo; zanzibar wenzetu wanafanya vizuri maana leseni ya udereva inaendelea kuonyesha uzoefu wako wote.

TRA; kabla hatujaanza kugoma rekebisheni hili. Wewe angalia leseni yako utagundua hilo, hata kama umeendesha miaka 30 bado uzoefu haupo hapo.
 
Hata zamani enzi za leseni za kale kakitabu kadogo ilikuwa ni kubandika risiti tu, inaonesha tangu mwanzo siku ilipokatwa siku ya kwanza
 
Ukisha renew wanakupa ile leseni ya zamani, kwahiyo unakuwa nazo zote.
 
Kama ukirenew licence, ukigeuza kule nyuma muda wake huanzia ule muda wa leseni ya zamani. Mtoa mada hebu jaribu kuangalia vizuri leseni yako.
 
Back
Top Bottom