TRA: Kariakoo lazima EFD kwa wote

Sasa hivi kuna mfumo unaitwa VFD i guess huhitaji kununua hio mashine.
 
Watanzania tunapenda sana janjajanja, ukienda kwa Kagame hadi fundi viatu anatoa receipt ya electronic, Bongo wengi tunapenda kona kona sana
Hamna anayependa janja janja ila kwa kuwa viongozi ndio waasisi wa hizo janja janja wacha nasie tuishi kwa mtindo huo huo.
 
Mteja unaingia dukani unauliza bidhaa...unatajiwa bei...mfano mimi nilienda nunua chandarua cha mbu nkaambiwa bei ni 150000. Nikaomba nipunguziwe. Wakakubali kuniuzia 130000 ila kwenye mashine ya TRA wataandika 70000.
Au bila risiti unaambiwa utoe 100000. Kama mteja unayepambana na tozo unajua maamuzi yanayofuata.
Maamuzi yalikuwa siri yangu mwenyewe.
 
Dah hivi hii VFD inakuwaje?
Unaunganishwa na system ya TRA unaweza kutoa risiti kimtandao hata kwa kutumia simu, mteja unaweza kumtumia kwenye simu/ email au ukipenda unaprint. Kuna mtu anatangaza sana humu JF hio huduma. Mashine soon zinakuwa hazina kazi.
 
Hata anaetandika chini lazima alipe kodi kulingana na faida anayoipata hapo chini.
Haifosiwi, kwani sheria inasemaje ama ile sheria ya faida ya 12M kwa mwaka haitumiki tena?
 
Chandarua cha mita ngapi hicho cha 150000 kama hutajali😂 unijuze
 
TRA hawauzi EFD machine
 
Sasa hivi kuna mfumo unaitwa VFD i guess huhitaji kununua hio mashine.
Hata VFD unatakiwa uwe na printer yake, maana mteja atataka printout ili asisumbuliwe na TRA.
 
Unaunganishwa na system ya TRA unaweza kutoa risiti kimtandao hata kwa kutumia simu, mteja unaweza kumtumia kwenye simu/ email au ukipenda unaprint. Kuna mtu anatangaza sana humu JF hio huduma. Mashine soon zinakuwa hazina kazi.
Bora hio ya kuunganisha na simu kuliko ile ya TRA machine. Wahakikishe pia hio VFD ituoneshe report ya makusanyo ya siku, week, mwezi kwa wote walio kwenye network.
 
Bora hio ya kuunganisha na simu kuliko ile ya TRA machine. Wahakikishe pia hio VFD ituoneshe report ya makusanyo ya siku, week, mwezi kwa wote walio kwenye network.
Inaonesha kila ripoti ukitaka ya siku, mwezi, wiki yote unapata, pia ina option ya kusave risiti unazo toa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…