TPP KULETA UPINZANI MKALI UCHAGUZI MKUU TAIWAN MWAKANI(2024) ?

TPP

JF-Expert Member
Mar 18, 2023
650
782
1152x768_214341539572.jpg

( Mgombea kiti cha urais 2024 bwana Ko Wen-je kupitia chama cha TPP ).

Chama cha kisiasa cha Taiwan ambacho kiliundwa miaka minne(2019) iliyopita kimepanda nafasi mbele ya chama kikuu cha upinzani Kuomintang na kuwa chama cha pili maarufu zaidi katika kisiwa hicho.

Chama cha watu wa Taiwan(TPP) kilipata Uungwaji mkono kutoka kwa 22.2% ya washiriki, kikipita asilimia 20.4% ya chama Cha Kuomintang( KMT ), kulingana na kura kutoka taasisi binafsi ya mawazo (Taiwanese Public Opinion Foundation)iliyotolewa Alhamisi. Uungwaji mkono kwa chama tawala cha Maendeleo ya Kidemokrasia(DPP) ulikuwa 24.6%.

Kwa DPP na KMT wakiwa wamehodhi siasa za Taiwan kwa muda mrefu, hii ni mara ya kwanza ambapo vyama vitatu vya kisiasa vimezidi kila kimoja asilimia 20% katika idhini ya umma. Pengo kati yao pia limeshuka hadi kufikia asilimia 4.2.

Chama cha Watu wa Taiwan kilianzishwa mwaka 2019 na Meya wa Taipei wakati huo, Ko Wen-je. Kimepata kasi kwa kutumia uungwaji mkono kutoka kwa wapiga kura wenye kuchoshwa na vyama viwili vikuu. Ko anapanga kugombea katika uchaguzi wa rais utakaofanyika mwezi Januari mwka ujao.

KMT inapendelea uhusiano wa karibu na Beijing, wakati DPP inachukua msimamo mkali. TPP iko katikati ya pande hizo mbili kwa kutoa kipaumbele kwa kuendeleza uhusiano wa sasa.

Mfumo wa vyama viwili uliibuka Taiwan katika miaka ya 1990 baada ya KMT, ambacho kilikuwa kimeongoza kisiwa hicho chini ya sheria ya kijeshi kwa miongo kadhaa, kukubali madai ya umma ya demokrasia.

DPP imekwama katika kashfa za unyanyasaji wa kijinsia hivi karibuni, na KMT ilipata shida kumuweka mgombea kwa uchaguzi wa rais, hivyo kuwashawishi wapiga kura zaidi kumuunga mkono TPP.

Ingawa bado haijulikani ikiwa kasi ya chama hicho itadumu, "itakuwa na athari kubwa katika uchaguzi wa rais na bunge la Yuan mwakani," Taasisi ya Maoni ya Umma ya Taiwan ilisema kuhusu kuibuka kwa chama hicho.
 
Back
Top Bottom