KERO TOZO ZA SERIKALI kwenye MIAMALA ya Simu zimerejeshwa tena?

KERO TOZO ZA SERIKALI kwenye MIAMALA ya Simu zimerejeshwa tena?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
1756906103434.jpg


Kama sikosei ni takribani miaka miwili au mitatu imepita tangu serikali ilipotangaza na kupitisha makato maalumu (Tozo za serikali) kwenye miamala ya simu.

Serikali ilisema kwamba tozo hizo zingetumika kujenga vituo vya afya, madarasa, kutengeneza madawati nk (kama sikosei, naomba nikumbushwe).

Wananchi walipinga sana hizo tozo na hata kupunguza kutumia au kufanya miamala ya simu kwa kiasi fulani.

Hata hivyo serikali baadae ilitoa takwimu (kupitia kwa msemaji wake) kuhusu kiasi kilichokusanywa na namna ilivyotumika, lakini bado kukawa na minong'ono kuhusu ukweli wa matumizi ya hizo tozo.

Baadae tulitangaziwa kwamba hakutakuwa tena tozo za serikali katika miamala ya simu na kweli toka wakati huo miamala yote iliyofanyika haikuwa na tozo za serikali bali makato ya mitandao husika tu.

Hata hivyo tangu mwezi Julai 2025 nimeshangaa kuona tena tozo za serikali zimerejeshwa kimya kimya bila taarifa rasmi.

Tunaipenda sana nchi yetu Tanzania na tupo tayari kuijenga kwa moyo wote na kwa namna yoyote ikiwemo kupitia hizo tozo za serikali nk lakini ni muhimu sana kukawa na uwazi na ukweli juu ya malengo na matumizi sahihi ya hizo fedha/tozo, isijekuwa wananchi tunatozwa fedha kwa ajili ya maendeleo yetu wenyewe lakini inaishia kufanya mambo binafsi ya wachache walioko madarakani.
 
Welcome to Tozoland where the innocents are taxed and the crooks steal the taxes.
 
"Tuna akaunti maalum kwa ajili ya kulipa mikopo". Hadi pale dada atakapomaliza muhula wake, tutakuwa hatuna deni kabisa.
 
Back
Top Bottom