KWELI Tozo za kutoa pesa kwa wakala na ATM bado hazijafutwa

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Kumekuwepo na mijadala inayoendelea kwenye mitandao ya kijamii ikizungumzia uondolewaji wa tozo kwenye miamala ya kielekroniki.

Baadhi ya watu wamekuwa wakidai kuwa tozo hizi zimefutwa kila sehemu huku wengine wakidai kuwa zimeongezeka tofauti na awali.

96174532.jpg

Ukweli wa suala hili upoje?
 
Tunachokijua
Katika mwaka wa fedha 2021/22, Sheria ya Malipo ya Taifa, Sura na. 437 (National Payment System Act, Cap.437) ilifanyiwa marekebisho kupitia Sheria ya Fedha ya mwaka 2021 na kuanzisha tozo ya miamala ya kutuma na kutoa fedha kwa njia ya simu za mikononi yaani, Mobile Money Transaction Levy.

Sambamba na tozo hii, tozo kwenye mafuta kwa ajili ya kutunisha mfuko wa TARURA na Mfuko wa Elimu ya juu zilipandishwa.

Lengo la kuanzishwa kwake
Lengo la kuanzisha tozo hizi ni kuunganisha nguvu na umoja wa Watanzania wote katika kuiwezesha Serikali kuongeza kasi ya kutekeleza miradi hasa ile iliyokosa fedha kutokana na ufinyu wa bajeti ili kuwakwamua wananchi dhidi ya ukosefu wa huduma za jamii-msingi kwa kuzingatia kuwa sura ya bejeti yetu karibu kila mahitaji ni mahitaji ya lazima.

Tozo hizi zilipewa jina maarufu ya "Tozo za mshikamano"

Kuibuka kwa Madai ya kufutwa kwa tozo
Juni 27, 2023, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye alisema kuwa Watanzania milioni 44 ambao ni idadi ya watumiaji wa miamala ya kifedha kwa njia ya simu kwa nchini kwa sasa watanufaika na kuondolewa kwa tozo kwenye miamala kwa njia ya simu.

Akifungua rasmi ofisi mpya ya kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania iliyopo maeneo ya Kilimani jijini Dodoma, Waziri Nape alibainisha kuwa alipoingia kwenye kiti hicho alikuta suala hilo likiwa 100% na kupambana hadi kushuka kufikia 50% na sasa tayari tozo hizi zimefikia 0%.

Julai 1, 2023, Mtumiaji mmoja wa Mtandao wa Twita anayetumia jina la George E. Mwaipungu aliweka video ikimuonesha Waziri Nape akizungumzia tozo hizo. Video hiyo iliambatana na maneno haya;

"Wapiga makofi wanashangilia utafikiri wazo lakuweka tozo kwenye miamala lilietwa na Rais wa Kenya yani"

Miongoni mwa wachangiaji wa chapisho hilo alikuwa ni Think Different aliyesema;

"Huyu jamaa ni muongo muongo sana, Tozo zimefutwa kwenye mihamala ya simu kwa simu, ila ukitoa fedha tozo ziko pale pale na ndizo kubwa ukilinganisha na zile za kutuma. Hawa watu kila kitu wanaongea uongo, upuuzi mtupu"

Aidha, Julai 3, 2023, Mtumiaji mwingine wa Mtandao huo anayejulikana kama Mchokozi alihoji watu wanaosema tozo zimefutwa huku zikiwa bado zipo, alisema;

"Ukiingia kwenye Mitandao unaona wanasema Tozo zimefutwa, Ukituma hela tozo bado zinakatwa, hizi tunazoambiwa zimefutwa ni tozo zipi hizo? Au mimi ndo sielewi?"

Kama ilivyobainishwa tangu awali, Mjadala wa suala hili umetawaliwa na pande mbili. Julai 4, 2023, Naibu Waziri wa Wizara ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Injinia Kundo Mathew akiwa kwenye ziara ya kikazi Mkoani Rukwa alisema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameridhia ombi la Wizara hiyo chini ya Waziri Nape Moses Nnauye la kufuta tozo katika miamala ya simu.

Waziri Kundo alinukuliwa akisema;


"Fahari ya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Rais ni pamoja na kuwasikiliza Watanzania na Wananchi anaowaongoza, ndio maana ameruhusu na kutoa maelekezo ya moja kwa moja kuondoa tozo katika miamala ya simu"

"Rais wenu kipenzi Mkuu wa Nchi ameruhusu na kutoa maelekezo tozo inayotokana na miamala ya simu iondolewe, hakutokuwa na tozo kwenye miamala ya simu, ile tozo mliokuwa mnasema Rais ameshapangua huyu ndio Mwanamapinduzi halisi wa maendeleo ya Taifa letu"


Kauli hii iliongeza ukubwa wa mjadala, jambo lililoifanya JamiiForums kufuatilia ili kufahamu ukweli wake.

Uhalisia wa kufutwa kwa tozo
JamiiForums imezungumza na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha Bw. Benny Mwaipaja aliyebainisha aina za tozo zilizofutwa. Mwaipaja amesema
Tozo za miamala ya kieletroniki zilizofutwa ni;
  1. Unapomtumia mtu muamala kutoka simu yako kwenda simu ya mtu mwingine.
  2. Unapohamisha fedha kutoka akaunti yako ya Benki kwenda akaunti nyingine.
  3. Unapohamisha fedha kutoka akaunti yako ya Benki kwenda kwenye simu yako.

Ameongeza kuwa "unapokwenda kwa wakala kutoa fedha zako kwenye simu utakatwa tozo; na utakapotoa fedha taslimu kupitia ATM au kaunta utakatwa tozo."

"Lengo la Serikali la kuendelea kukata tozo hiyo ni kuhamasisha matumizi ya njia ya kielektroniki kufanya miamala ama manunuzi. Hivyo vipeperushi vinavyosambazwa pamoja na mijadala inayoendelea kwamba Serikali imefuta tozo zote za miamala ya simu na kibenki vinapotosha jamii."


Juni 16, 2023, Gazeti la The Citizen lilichapisha makala inayodokeza mpango wa kufutwa kwa tozo hizi kama sehemu ya jitihada za Serikali katika kukuza uchumi wa Kidigitali.

Pia soma: Gerson Msigwa: Tozo kwenye Miamala ya kutoa pesa bado ipo
Sasa cha ajabu viongozi wetu wameng'ang'ania tozo zimefutwa. Na hizo mbwmbwe za Eng Kondo ulizonukuu kama ni kweli basi hilo ni tatizo la siasa za praise team
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom