Kimsingi tozo bado hazijafutwa kwa sababu zifuatazo

Jerlamarel

JF-Expert Member
Sep 14, 2021
843
2,517
Tozo bado hazijafutwa kwa sababu zifuatazo:

Facts Checks:

1. Wamefuta Tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu pande zote.

Fact: Makato au kodi ya kufanya hii miamala iko juu sana hata kabla ya tozo na watu wengi walikuwa wanaiepuka hii miamala sababu ya ughali wake.

Imagine ukituma 10,000/= kutoka simbanking kwenda kwenye simu yako unakatwa 2,700/=, kutuma 50,000/= unakatwa 5,300/=.

Hivyo kwa sababu hili eneo limeonekana halina maslahi ndiyo maana ni kama linatumika kisiasa kwamba limefutiwa tozo huku kiuhalisia huenda halikuwa linaingiza chochote cha maana.​
IMG_20220920_135326.jpg

2. Wamefuta Tozo ya kuhamisha fedha ndani ya benki moja.

Fact: Bado hii ni danganya toto kwa maana eneo hili halikuwa na kodi au makato yoyote na haikuwa sahihi kuliwekea tozo.​

IMG_20220920_143359.jpg

IMG_20220920_143528.jpg

3. Wamefuta Tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki moja kwenda nyingine.

Fact: Hapa napo wametupiga changa la macho tuu maana makato ya kawaida hata kabla ya tozo yapo juu.

Kutuma pesa kutoka bank moja kwenda nyingine ni 2,000/= kwa kila muamala, haijalishi umetuma elfu 2, 3 10,au 90, wakati huohuo kupokea pesa kutoka bank nyingine ni 4,000/= kwa kila muamala bila kujali kiasi unachopokea.​

IMG_20220920_140631.jpg

4. Wametoa msamaha wa tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia wakala wa benki na ATM kwa miamala yenye thamani isiyozidi TZS 30,000.

Fact: Ukitumia akili ya mtoto wa darasa la 3 tuu utajua tuu hapa ni danganya toto ya kiwango cha lami. Hivi kweli kwa dunia ya sasa na haya maisha yalivyopanda gharama miamala ya 30,000/= nani bado anafanya? Ni wachache sana.

Kwa maana hiyo hapa limelengwa kundi dogo, kisha kundi kubwa limeachwa palepale liendee kutozeka kama kawaida.

5. Watapunguza gharama ya miamala kwa 10% hadi 50% kufuatana na kundi la miamala.

Fact: Hii ni "general term" ambayo inafanana na ile iliyotumika kwenye nyongeza ya 23% ya mishahara kwa watumishi mwaka huu, lakini baada ya calculations sote tunajua kilichotokea, ilikuwa ni vilio na kusaga meno maana kundi dogo ndilo litafaidika huku kundi kubwa likiendelea kukatwa tozo.

In fact kitendo cha kuweka tuu % kadhaa mpaka kadhaa hilo ni fumbo limefumbwa ili kuepusha taharuki, lakini hiyo tarehe 1 Oktoba hakutakuwa na mabadiliko ya maana. Ukitaka uamini hili fanya muamala wa laki 1 leo u-noti makato pembeni, kisha mwezi wa 10 fanya muamala mwingine uone kama kutakuwa na mabadiliko ya maana.

NB: Wanachi siyo kwamba tunapinga tozo, hapana. Ila huu ni wizi wa mchana (Day Roberry) kwa maana eneo lililoguswa ni crucial kwa maisha ya kipato cha chini kabisa ambaye hicho anachokitozwq huenda ndicho ilikuwa kapesa kake ka kununulia panadol au mboga.

Ni eneo ambalo huenda hicho mnachokitoza ndicho faida ya mjasiriamali anayepambana kujikwamua.

Tozo hazitatupeleka popote, its just a shoft term solution, wanasiasa mlioshika usukani wa kuongoza dira ya taifa tumieni hizo bongo zenu kuwaza namna ya kugenerate long term solutions za kulikomboa hili taifa kutoka kwenye utegemezi.​
 
Tozo bado hazijafutwa kwa sababu zifuatazo:

Facts Checks:

1. Wamefuta Tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu pande zote.

Fact: Makato au kodi ya kufanya hii miamala iko juu sana hata kabla ya tozo na watu wengi walikuwa wanaiepuka hii miamala sababu ya ughali wake.

Imagine ukituma 10,000/= kutoka simbanking kwenda kwenye simu yako unakatwa 2,700/=, kutuma 50,000/= unakatwa 5,300/=.

Hivyo kwa sababu hili eneo limeonekana halina maslahi ndiyo maana ni kama linatumika kisiasa kwamba limefutiwa tozo huku kiuhalisia huenda halikuwa linaingiza chochote cha maana.​
View attachment 2362603

2. Wamefuta Tozo ya kuhamisha fedha ndani ya benki moja.

Fact: Bado hii ni danganya toto kwa maana eneo hili halikuwa na kodi au makato yoyote na haikuwa sahihi kuliwekea tozo.​

View attachment 2362639

View attachment 2362640

3. Wamefuta Tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki moja kwenda nyingine.

Fact: Hapa napo wametupiga changa la macho tuu maana makato ya kawaida hata kabla ya tozo yapo juu.

Kutuma pesa kutoka bank moja kwenda nyingine ni 2,000/= kwa kila muamala, haijalishi umetuma elfu 2, 3 10,au 90, wakati huohuo kupokea pesa kutoka bank nyingine ni 4,000/= kwa kila muamala bila kujali kiasi unachopokea.​

View attachment 2362641

4. Wametoa msamaha wa tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia wakala wa benki na ATM kwa miamala yenye thamani isiyozidi TZS 30,000.

Fact: Ukitumia akili ya mtoto wa darasa la 3 tuu utajua tuu hapa ni danganya toto ya kiwango cha lami. Hivi kweli kwa dunia ya sasa na haya maisha yalivyopanda gharama miamala ya 30,000/= nani bado anafanya? Ni wachache sana.

Kwa maana hiyo hapa limelengwa kundi dogo, kisha kundi kubwa limeachwa palepale liendee kutozeka kama kawaida.

5. Watapunguza gharama ya miamala kwa 10% hadi 50% kufuatana na kundi la miamala.

Fact: Hii ni "general term" ambayo inafanana na ile iliyotumika kwenye nyongeza ya 23% ya mishahara kwa watumishi mwaka huu, lakini baada ya calculations sote tunajua kilichotokea, ilikuwa ni vilio na kusaga meno maana kundi dogo ndilo litafaidika huku kundi kubwa likiendelea kukatwa tozo.

In fact kitendo cha kuweka tuu % kadhaa mpaka kadhaa hilo ni fumbo limefumbwa ili kuepusha taharuki, lakini hiyo tarehe 1 Oktoba hakutakuwa na mabadiliko ya maana. Ukitaka uamini hili fanya muamala wa laki 1 leo u-noti makato pembeni, kisha mwezi wa 10 fanya muamala mwingine uone kama kutakuwa na mabadiliko ya maana.

NB: Wanachi siyo kwamba tunapinga tozo, hapana. Ila huu ni wizi wa mchana (Day Roberry) kwa maana eneo lililoguswa ni crucial kwa maisha ya kipato cha chini kabisa ambaye hicho anachokitozwq huenda ndicho ilikuwa kapesa kake ka kununulia panadol au mboga.

Ni eneo ambalo huenda hicho mnachokitoza ndicho faida ya mjasiriamali anayepambana kujikwamua.

Tozo hazitatupeleka popote, its just a shoft term solution, wanasiasa mlioshika usukani wa kuongoza dira ya taifa tumieni hizo bongo zenu kuwaza namna ya kugenerate long term solutions za kulikomboa hili taifa kutoka kwenye utegemezi.​
Wanakusanya tozo kisha wanazitumia kwa manufaa yao binafsi. Fikiria waziri wa fedha anaagiza mabasi 60 kwa mkupuo nk
 
Shida ya watanzania ni kuingiza siasa kila mahali hata maeneo ya kiuchumi. Hapa wanacheza na hisia za watu na wongo mwingi. They are simply using statistical manipulations na kuja na same result yaani tozo wa watanzania. Tumekuwa na wachumi wa hovyo kabisa nchi hii. Ukiona role ya TRA inachukuliwa na hazina ujue kuna kitu hakipo sawa.
 
Kiukweli tutamkumbuka sana hayati JPM, pamoja na yote, alisaidia watu kufikiri kabla ya kutenda kwa hofu ya kutumbuliwa. Hata kama wanaiita nidhamu ya uoga, ila ilisaidia sana!
Viongozi wa sasa ni waonevu sana!
Majibu na maamuzi yao yanakatisha tamaa
 
Yani wameng'ang'ana na fedha zetu tu ila mungu yupo malipo hapahapa duniani kwani dua za wengi husikilizwa
 
Similar Discussions

47 Reactions
Reply
Back
Top Bottom