Tozo: Wadau Walalamika na Serikali kukosa usikivu

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,321
24,228
Mjadala mkali kabisa ktk kituo cha televisheni cha ITV Tanzania

======



Katika mjadala mpana na wa wazi wadau waonesha wasiwasi kuhusu serikali kutochukua hatua za haraka kupata ufumbuzi wa kusitisha tozo inayolenga chanzo kimoja tu cha mapato kukatwa mara kadhaa.

Mfano mishahara ipitayo benki ambayo ndiyo chanzo pekee cha mapato ya mwalimu kulimwa tozo kila anapokwenda kuchukua hela toka akaunti yake ya mshahara.

Wadau wajiuliza sababu ya serikali kukosa huruma kwa raia wake ni nini.

Waamua kuiambia ni sehemu gani wanaweza kupanua wigo wa kodi zinazoitwa tozo bila kuwaumiza wananchi.

Waiambia serikali ielekeze macho ktk kilimo kikubwa cha kisasa cha mazao wasema kama kilimo cha sukari Kilombero, Mtibwa na Kagera, mashamba ya kisasa kabisa ya kilimo cha kumwagilia maji.

Kwanini kusiwepo mashamba makubwa ya kilimo cha nafaka na mazao mengine kwa ukubwa huo huo kama ya mashamba ya miwa kwa ajili ya sukari ili nchi izalishe nafaka kuishinda Ukraine.

Bandari pia ni eneo lingine wadau wamesema serikali inaweza kuongeza mapato ya kodi ikiwa watavutia wadau wa nchi zisizo na bahari bila kusahau gesi n.k

Source: ITV Tanzania
 
Kila mtu atalambwa.
snoop.png
 
Mama Ana kazi ngumu mno ya kumtimulia mbali msomi mkuu wa nchi, kwa maslahi mapana ya taifa, ukinifutia Tozo haramu ya shilingi Mia nitakuwa tayari kutoa shilingi elfu moja huku nikiwa na furaha kabisa, ila ukinipora 100,nitatafuta njia ya kukuepuka for good! Mwigulu ni tatizo kwa kweli

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom