stephot
JF-Expert Member
- Mar 1, 2012
- 18,114
- 28,013
Wadau nilikuwa naangalia tarifa ya habari ITV nimeona Toyota Landcruiser VX imehuska tena kwenye ajali ambayo imegharimu maisha ya jaji mstaafu Mwaipopo,kilichonifanya niingize hii mada ni kutaka kujua kutoka kwa wadau wenye utaalamu wa mambo ya magari watueleze kasoro zilizopo kwenye hizi gari kwani tokea zilipoingia haipiti miezi 6 lazima utasikia imefanya ajali.Ni imani yangu kuwa lazima kutakuwa na technical problem kwenye hizi gari na kama hazitafanyiwa utafiti wa kutosha zitaendelea kuteketeza maisha ya viongozi wetu.