Tosamaganga high school

Tosamaganga high school

Shule la kimaskini mnapoteza muda kulipromoti. Na sisi tuliosoma Shaaban Robert kisha Bonn (Germany) tukiweka picha zetu? Mbaaffffff

acha hizo! hivi zikitajwa shule za "kitajiri" shaaban robert itatoka kweli?
miaka ile wenzako walikuwa wanatoka hapo hapo shabaan robert na kuhamia tosa (miaka hiyo
ilikuwa ruksa kutoka private kwenda public). tena sio kwa kushindwa fee bali kufuata elimu.
 
Good memory i did my a'level 1984 -1986 i will find a chance to vist that popular hill 'TOSA'
 
Niliona hata mimi ni vema kulienzi jina la IDETE. Ctosahau maisha ya hapo HALF MILE.
 
mnakumbuka east london kenye maandazi, idete kwenye vitindi vya ulanzi, duu umenikumbusha mbali saaana tumechunga ngómbe sana hapo. long live tosa
 
Shule la kimaskini mnapoteza muda kulipromoti. Na sisi tuliosoma Shaaban Robert kisha Bonn (Germany) tukiweka picha zetu? Mbaaffffff

Haiwezekani kila mtu asome Shaaban Robert na Bonn...na hata hivyo talents zimegawanywa across the board. Tusidharau vilivyo vyetu ati.
 
hahahaha mkuu henge bana.....wengi tumepita pale sana....nilikuwa nalala mandela room 100 na nilikuwa academic prefect..
nilikuwa room no. 99 mandela, sijui miaka ipi ulipita ila room no. 100 iko opposite na room no.99
 
Shule la kimaskini mnapoteza muda kulipromoti. Na sisi tuliosoma Shaaban Robert kisha Bonn (Germany) tukiweka picha zetu? Mbaaffffff

Watoto wa mafisadi lakin ukifuatilia utakuta huyo aliyekusomesha shule za kitajiri yeye pia alipitia huku
 
Khe khe khe khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee watu kwa kujipandisha bana huwawezi ... ...hivi Tosa na Mkwawa na Ifunda kwa Iringa ipi ilikuwa zaidi. Au shule zilizokuwa na hadhi enzi hizo yaani Moshi tech, Ifunda tech, Tabora boys, Mkwawa etc. Wachilia mbali shule koko kama Shaban Robert .... .... ..... ..... wengine tumesoma Internatinal school ooops ulimi umeteleza ... ... .. khe khe kheeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee


BTW hata Jakaya na Che nkapa watachema shule zao zilikuwa za maana sana maana wamekomba hazina yote ya hili taifa na wale wanaojiona ati walisoma shule za maana wamebaki kuwafadhili hawa ma-lofa kuendeleza starehe zao. Nyie mliosoma shule za maana liokoeni hili taifa kutoka kwa wezi wanaoiba mchana kweupe bila aibu kuanzia wanolala magogoni ... .... ... ..
 
Wakati niko form six zaidi ya miongo miwili na nusu iliyopita (tosamaganga sec) kulikuwa na mashindano ya mpira kati ya timu ya shule na wanakijiji....wale wanakijiji walipenda sana kutufunga mara kwa mara .binafsi nilikuwa sio mchezaji bali mtazamaji na mpenzi wa timu yangu ya shule na nilikuwa sipendezwi na namna wale wanakijiji walivyokuwa wanatufunga kila mara.

Siku moja tukiwa na mechi na hawa wanakijiji na mshindi wa mchezo ule alikuwa anaondoka na Mbuzi (beberu)... asubuhi wakati watu wanajiandaa kwa ile mechi na baada ya mwl wa michezo kupanga kikosi ..wazo likanijia kichwani na kusema kuwa sitaki hawa wanakijiji wamchukue mbuzi maana niliamini kabisa kuwa wanaweza kutufunga.. .


Bila kumwambia yeyote nilienda ipamba hosp na kufanikiwa kupata bomba la sindano kisha nikarudi shule na kumfata mzee aliyekuwa anatunza funguo za maabara na kuingia maabara na kujifanya nafanya mafunzo ya practical(chemistry)..lengo langu kuu lilikuwa ni kuiba acid (conc. Sulphuric acid na conc. Hcl)..nilifanikiwa...


Mda wa michezo ukafika tukashuka uwanjani(msiwasi) na mechi ikaanza mda wa jioni saa kumi na nusu....mpaka inafika dakika ya 70 timu ya shule (tosaboys) walikuwa nyuma kwa magolli mawili na dalili za kurudisha magoli hazikuwepo maana walielemewa sana...huku uwanja ukiwa umefurika watu(wanakijiji na wanafunzi+ walimu) nilijipenyeza hadi meza kuu walipokuwa viongozi wa kijiji na walimu na pembeni yake alikuwa amefungwa yule mbuzi...


Pasipo mtu yeyote kuniona wala kutambua na kwa njia ninayoijua mimi nilimchoma yule mbuzi sindano ya acid na kuondoka kuelekea upande mwingine wa uwanja . mbuzi alilala chini na badae kidogo alikufa na wengi pale uwanjani hasa wlaiokuwa karibu na mbuzi walidhani amelala usingizi kumbe alikuwa amelala kweli!!
Timu ya kijiji ilimkosa mbuzi na mpaka leo hawakujua chanzo cha kifo cha mbuzi yule..walimzika...




Ukiniuliza leo kwa nini nilimchoma sindano ya acid mbuzi yule ntakwambia sikutaka kombe(mbuzi) achukuliwe na wanakijiji....ukiniuliza maswali zaidi juu ya ubora wa timu yetu, formationa ya timu uwanjani, na ubora wa timu ya shule na mazoezi naweza nikawa sina jibu ila sikuwapenda tu hawa wanakijiji wamchukue yule mbuzi.....
 
mkuu nimekuaminia, ila nasikitika kama mandela halituiki, ndo lilikua bweni langu, umenikumbusha mbali mno,
enzi za mwalimu mkangwa, duuu kweli life goes on
Tosamanganga katika walimu wakuu majembe haijawahi kutokea mwalimu kama huyo, nakumbuka wakati mimi namalizia A level yangu mwaka 1996 ndiyo alikwa amehamishiwa hapo, tena alikuwa na mke wake ambaye walipendana sana kama mapacha kabla ya Mungu kumchukua mkewe (Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi).

Ikafikia yule mkewe ameteuliwa kuwa DC, basi ilikuwa wakati wakitumia Land rover defender la shule mume anakaa mbele n awakati wakitumia gari la mkuu wa wilaya mume anakaa nyuma na mkewe mbele. Siku moja nikamuuliza, "mwalimu inakuwaje unakaa siti ya nyuma wakati wewe ni kichwa cha nyumba?", akajibu nikitumia gari la shule mimi ni bosi na tukitumia la kwake yeye ni bosi.
 
dah nimepiga hapa 2006-2008,hayo maneno sifongo,flash[sprash] yapo sana,mmesahau siku ikiwa graduation au easter conference kasi ya kuoga inaongezeka watu wana2pia pamba na kujipanga road kutizama mabinti,sherehe ikianza ni kuhaha kusaka wa kucheza nae dah namshukuru Allah Tosamaganga imenitoa sana ndiko nilikojifunzia watu wanasomaje na wanaishije kijeshijeshi maana ukizubaa huli wala uishi kwa raha.
long live Tosamaganga
 
Back
Top Bottom