Sahakazulu;
Du! Asante sana kwa kumbukumbu nzuri. Nilikuwa hapo wakati wa ule mgomo uliomuondoa marehemu "Dudu". Walikuwepo akina Boyd "Mnazareti", Biga Kipemba, Joseph Paschal, Patrick Rwehumbiza, Kimti, Japhet Makau, Bruce Mwile, Msasalaga na wengineo wengi.
Mkuu umenikumbusha mbali, mimi nilikuwa high school class of 1993 na baadhi ya watu uliowataja hapo. Wengine ni Waziri Rajab, Robert Mwaikambo, Terrence Ngole, Ernest Mbaga, Maluli, Immanuel Mnada n.k.
Nakumbuka siku ya vurugu watu tulilala porini maana FFU walitanda hapo shule palikuwa hapaingiliki. Vurumai hilo lilisababisha baadhi ya wanafunzi kushtakiwa ila sina uhakika kama kuna aliyefungwa. Dah!