Topic gani ilikusumbua sana O-level au A-level

Nadhani wengi tuliopita advance na tuliosoma Physics ngoma ngumu ilikua Rotation of rigid bodies
 
Kwenye kiswahili kuna mambo ya ngeli zile mambo za ki-vi cjui pamuku i-vi. Mpaka leo cjazijua na sitaki kuzijua
 
Wave Part 2 A level mamaee...nkasema liwaloo na liweee sikugusa hata defn.

O level Account[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] walahi mpaka nikaona wanaosoma Biashara ni wachawiii mambo ya credit sijui debt duu nilisota nazo sikuelewa nilikuja kuelewa Chuo tena mwaka wa mwisho nkagundua tatizo sio soma tatizo aliekuwa ananifundisha nae alikuwa amekariri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Density form one..kiingereza sikijui halafu unaniambia mass b to a mass a. Naijulia wapi? Nilichukia physics hapo nilitoka na c mwishoni
Daa miaka hiyo form one nakumbuka wiki ya pili tu baada ya kuripoti niliandikwa kama main speaker kwenye debate , kiingereza chenyewe cha kuvutavuta aisee .........siamini lakini hatimaye siku iliisha........
GLU™
 
Mambo ya vitabu somo la kiswahili(kiswaz) sijawahi kuelewa kabisa! OLevel sijawahi jibu swali linalohusu vitabu na A level pia. Ila chakushangaza sijawahi kukosa credit(C-B).

5/5
 
Na bora usi deal na Roger Muncaster au Tom Duncan.
GLU™
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…