Ukweli Kuhusu CCM Kufifia Kisiasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukweli Kuhusu CCM Kufifia Kisiasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mchambuzi, Jun 25, 2011.

 1. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2011
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Yafuatayo ni maoni yangu binafsi - kwanza kama mtanzania halafu baadae kama Mwa CCM kwani daima Naamini Tanzania Kwanza, Siasa Baadae. Mengi ya sababu hizi zinatokana na wananchi wenyewe ambao nimekuwa nazungumza nao mijini na vijijini na kunipelekea kugundua kwamba kuna mapungufu makubwa juu ya ukweli nini hasa kinapelekea chama changu cha CCM kupoteza mvuto kwani tafiti karibia zote juu ya suala hili, including the recent one iliyozaa dhana ya kujivua gamba sio holistic na badala yake nyingi zimekuwa atomistic. Solutions based on the atomistic approach hazitatatua tatizo bali kukuza zaidi tatizo. Nitaanza kwa kuelezea sababu kumi na nne (14) zinazopelekea CCM kupoteza mvuto kwa wananchi. Then mjadala utajikita katika kuangalia dhana nzima ya kujivua gamba na nitamalizia kwa kujadili changamoto zilizopo mbele ya CCM na maoni yangu juu ya nini kifanyike ili kuiokoa CCM katika kipindi hiki kigumu kuliko vyote tangia kuzaliwa kwake mwaka 1977.
  1. Sababu ya Kwanza CCM kupoteza umaarufu ni Mabadiliko katika silabasi elimu ya uraia mashuleni.
  Baada ya uhuru wa nchi yetu, elimu ya uraia ilikuwa ni moja ya njia kuu ambazo TANU/CCM na serikali iliitumia kufanikisha kuungwa kwake mkono na wananchi kuanzia wakiwa na umri mdogo. Lengo kubwa hapa lilikuwa to mold the masses into becoming good citizens. Enzi za Ujamaa, ‘good citizens’ walikuwa ni individuals waliopenda nchi yao na walikuwa wapo tayari kujitoa mhanga, with only a basic knowledge (not advanced knowledge) ya jinsi gani the government functioned. As one textbook ya civics miaka ile stated: “Civics is more than a collection of facts; it must build up in us a strong conviction…to use all our talents and energies for the building of a nation that is, and will be, truly democratic. Mwaka 1994 kulifanyika a survey among Tanzanian adults ambapo waliulizwa, je, what issues were emphasized when they attended primary school during the Ujamaa period? Majibu yao yalikuwa kama ifuatavyo: “love your country,” 34.9%; “obey authority,” 16.4%; “trust the leaders,” 15.3%; and “how the government is run,” only 4.5% (Source: Tanzania’s Political Culture, 2001). Kutokana na ukweli kwamba ni watanzania wachache sana miaka ile walikuwa na elimu beyond msingi, civic education wakati wa Ujamaa focused almost entirely on ujenzi wa taifa and promoting subject citizenship. In another civic text book cha enzi ya Ujamaa (based on the same source above|), it stated that: “opposition is something not traditional among Africans. When we discuss, it is not to fight each other, but rather to reach an agreement. It is so in our families, it has been so in our tribes, thus it can and must be so in the enlarged family, the nation.” Kwahiyo kwa watanzania wengi, critical citizenship was associated with violence, while subject citizenship was believed to be the traditional, natural way in which a citizen should interact with the state.

  Leo hii, kijana ameondokana na muundo huu kwani following the political liberalization in 1992, civics education has, in theory, aimed at producing knowledgeable, questioning citizens who show their affection for their country by critically examining its existing institutions. This contrast ipo evident just from a comparison of topics covered in various civics textbooks today. While texts books enzi za Ujamaa included long and relatively dry descriptions of every major government function or job - from ministers, RCs/DCs to local party leaders, textbooks za after 1992 content zake zimebadilika and instead focus on controversies in government policy and structure. Mfano, textbook ya mwaka 2001 includes an extensive section about the role of media in a democracy, which was hardly mentioned in the texts za Ujamaa era. Vitabu vya sasa heavily criticize the government for its suppression of the media and free speech. Notable issues that were present in the Ujamaa era textbooks, but are not present in today’s textbooks were frequent inspiring quotes from leaders, incitement to sacrifice for our country, and carefully framed national historical tales/stories. Implication yake sasa ni nini? A good citizen in the Ujamaa years was a “subject” of the state”, whereas a good citizen today is a “participant” in the process of political change. Wakati wa Ujamaa, a good subject citizen was loyal to all leaders and state institutions; leo hii, a good participant citizen shows his love of the country by critically demanding that it does better.Hivi ndivyo vijana wengi katika mazingira ya sasa wanajua kuchagua mchele na chuya.

  1. Sababu ya pili CCM kupoteza umaarufu: Demographic changes (in terms of population).
  Karibia asilimia 60 ya wapiga kura leo walianza elimu yao ya msingi ndani ya mfumo wa vyama vingi i.e. baada ya mwaka 1992. Hawa walikuwa na umri kati ya miaka 6 na 8 mwaka 1992 na kwa sasa wengi wao wapo katika age group ya miaka 27 hadi 29. Katiba yetu inaruhusu mtu kupiga kura akifika umri miaka 18, ingawa ni jambo la kawaida sana watu kuanza zoezi hili wakifikia umri wa miaka kumi na nne au tano. [Mimi binafsi na wenzangu wengi tukiwa Ilboru Sekondari tulimpigia kura Mzee Mwinyi tukiwa form one]. Hii ina maana kwamba katika uchaguzi uliopita (2015), mbali ya wale waliozaliwa mwaka 1992, pia watoto wengi waliozaliwa mwaka 1995 - 1996 pia walipiga kura. Ukichanganya wote hawa idadi yao inaweza kufikia asilimia 70 ya wapiga kura wote. Tusisahau pia kwamba wengi wao wakioa au wakiolewa wanawalea watoto wao katika mazingira ya mfumo wa vyama vingi.

  Leo hii asilimia kama 35 ya watanzania wapo mijini na asilimia 65 bado wapo vijijini. Lakini idadi ya watanzania, hususan vijana mijini inaongezeka kwa kasi sana. Wengi wao wanakimbia hali ngumu vijijini and associate the economic hardship with bad policies under serikali ya CCM; lakini pia they associate urban life na Maendeleo, modernity, access to recreational activities etc. Asilimia karibia 60 ya wapiga kura mijini ni vijana na hawa ndio chanzo cha Chadema kushinda majimbo mengi ya mijini kama Dar-es-salaam, Moshi, Mbeya, Musoma, Mwanza n.k kwani idea ya kuhamia mijini kwa wengi wao ni progressive and this goes hand-in-glove with how they perceive Chadema i.e. see it as a progressive and forward oriented party wakati chama chetu cha CCM is being perceived as a regressive party and backward oriented. Nitafafanua hili baadae.

  Kitu kingine muhimu pia ni idadi ya wapiga kura wengi vijana wenye elimu ya sekondari inaongezeka kwa kasi. Vile vile, idadi ya vijana wanaoendelea elimu ya chuo kikuu inazidi kukua lakini idadi kubwa sana ya hawa tayari ama wana ndugu, rafiki au jirani anaefanikiwa kufikia kiwango cha elimu ya chuo kikuu. Implication ya suala hili tutalitazama baadae.

  • Tatizo kubwa linalowakabili vijana hawa ni nini?
  Ni Elimu na Ajira ndio matatizo ya msingi. CCM chini ya umoja wa vijana yani UVCMM tumeshindwa kuisaidia serikali kulidhibiti hili au angalau kuwapa vijana mwongozo na matumaini. UVCCM have lost touch na kijana wa Tanzania. Tutaliangalia hili kwa undani baadae. Kikubwa hapa lakini ni kwamba upinzani, Chadema hususan (chini ya viongozi makini kama Zitto na Mnyika) umefanikiwa sana kuyaunganisha matatizo yao haya na udhaifu wa utawala wa serikali ya CCM. Kuna ukweli katika ili but only to an extent kwani sababu kubwa ya kushuka kwa kiwango cha elimu, unemployment na mushrooming of the informal sector pia ilichangiwa na economic reforms adopted in mid 1980s under pressure ya IMF and World Bank. Vilevile tusisahau kwamba kwa muda mrefu sana nchini yetu ili experience population growth rate that was higher than GDP growth rate. Lakini the bottom line is, Chadema imeona weakness hii ya CCM na kutumia it as an opportunity to increase its youth-base.

  Kitu kingine muhimu pia kukizungumza hapa ni kwamba, wakati wa ujana wetu, kumkosoa mkubwa wako ilikuwa ni kosa kubwa sana. Ilifikia hatua hata mkubwa wako akipumua, kijana haraka haraka unachukua jukumu lile na kusema “ni mimi” ili kumwondolea mkubwa au mzee wako fedhea. Na iwapo utamwona mtu mzima anakosolewa mbele yako basi unamwona ni dhaifu. Nina mfano mzuri juu suala hili katika Tanzania ya leo. Mwaka jana nilipata nafasi ya kuudhuria mafunzo ndani ya darasa moja shule ya msingi wilaya ya kinondoni ili kujionea mwenyewe matatizo yanayowakumba wanafunzi na walimu wao. Shule hii ilikuwa haina uzio (fence) kwahiyo wapitia njia wengi, walikuwa na tabia ya kupayuka kila wakisikia walimu wanafundisha kwa kutamka “mwongo huyo, anawadanganya” – kila wakati walimu walipokuwa wanatoa mafunzo yao. Hili liliwavutia sana wanafunzi wale na polepole wakaanza kupoteza heshima mbele ya walimu wao kwani walianza kuonekana kumbe sio chochote kwani pamoja na ukubwa wao na heshima yao kumbe hata wao wapo vulnerable na wanaweza kosoleka. Sina maana kwamba Chadema ni sawa na mpita njia, la hasha, hoja yangu hapa ni kwamba vijana na watoto wengi sasahivi wamekuwa wanavutiwa sana na hoja za Chadema za kukosoa utendaji wa serikali ya CCM na hoja hizi zimekuwa zinamvua mtu mzima na heshima zake (CCM) nguo hadharani na hili limechangia sana chadema kuvutia vijana na watoto wengi katika mikutano yao ya hadhara kwani wakisikia mikutano ya chadema, wanajua mkubwa anaenda hadhirika.

  Suala la jinsia nalo ni muhimu kuligusia kidogo. Idadi ya wanawake Tanzania imekuwa inaongezeka kwa kasi zaidi ya wanaume. Hivi sasa, katika watanzania kumi, wanawake ni kati ya sita na saba. Na tunajua jinsi gani kina mama na kina dada walivyokuwa na ushawishi pamoja na msimamo juu ya masuala mbali mbali in the household iwe kiuchumi, kisiasa na kijamii. Mama au dada akifanya uamuzi, mara nyingi ni wa busara na akishaamua mabadiliko, hayumbi na harudi tena nyuma. Mabadiliko ya changes in age and gender characteristics ni masuala ambayo CCM hatujiandaa kuyadhibiti au kuweka mikakati ya kwendana na mabadiliko hayo. Tuna UWT, UVCCM lakini wameshindwa katika hili.

  1. Sababu ya tatu CCM kupoteza umaarufu: Tofauti na sasa, zamani ilikuwa ni wajibu wa kila mwananchi kushiriki shughuli za CCM
  Kwa wale tunaokumbuka vizuri, enzi za mfumo wa chama kimoja, kushiriki shughuli za chama ilikuwa ni mandatory, kwa mfano viongozi wa CCM wakifanya ziara katika maeneo husika, ilikuwa ni kawaida kwa shule na hata biashara kufungwa ili mradi ku-attend public rallies, sherehe za chama n.k. Hili lilichangia sana CCM kuwa mazoea au sehemu ya maisha ya Mtanzania, sana sana vijana kwani shuguli kama za mwenge n.k zilikuwa ni sehemu muhimu sana katika maisha yetu. Vile vile ili kupata ajira au huduma yoyote ndani ya Tanzania ya wakati ule, ilikuwa ni lazima uwe mwanachama wa CCM. Makazini, mashuleni (shule za sekondari), kulijaa matawi ya CCM jambo ambalo kwa sasa halipo (kasoro vyuo vikuu). Kwa ufupi, ndani ya mfumo wa vyama vingi, mambo yote haya yamepungua kwa kiasi kikubwa sana na mengine kutoweka kabisa. Imekuwa jambo la kawaida kwa mtanzania wa leo kutoifikiria CCM kichwani mwake in the span of 24 hours kitu ambacho hakikuwa kawaida chini ya mfumo wa chama kimoja kwa kupenda au kwa kulazimika. Lakini ni jambo la kawaida sana kwa mtanzania wa leo kuwa na fikra juu ya Chadema muda wote kutokana na strategy yake ya kuiweka nchi katika hali ya uchaguzi 24/7/365. Chadema wamekuwa wazuri katika political branding kuliko sisi CCM. Mabadiliko hivi sasa ndani ya CCM yanaelekea kujaribu anzisha mkakati huu lakini bado tuna kazi kubwa.

  1. Sababu ya nne CCM kupoteza umaarufu: Removal of censorship katika muziki wa kitanzania
  Sote tunakubaliana kwamba muziki ni sehemu muhimu sana katika maisha ya binadamu wa sasa, kwani bila ya muziki, maisha ni kama hayapo na hayana tija. Sina haja ya kuelezea sana juu ya susla hili kwani sote tunalielewa. Katika nchi yetu, music has a long history in terms of being the platform for discussions and debates on political and social issues. Miaka ya mwanzo ya uhuru wetu, wana muziki wengi wa musiki wa dansi na taarab, walikuwa wanatunga nyimbo zilizokuwa zina comment on challenges of urban life. Kwa mfano, miaka in the early 1960s, kulikuwa na wimbo mmoja maarufu sana wa Mohamed Bwagajuga titled “Dar-es-Salaam Usiende.” Wimbo huu uliwonya watanzania juu ya dangers of living in the city. Wakati wa Ujamaa, wasanii wa dansi na taarab waliendeleza utamaduni huu. Wasanii wengi walikuwa wanaisifia serikali especially promoting goals that were envisioned by Ujamaa. Kwa mfano, Mbaraka Mwinshehe, a prominent Tanzanian musician miaka ya 1970s alitunga nyimbo kama: “TANU Yajenga Nchi”; “Kifo cha Pesa”, “Miaka 10 ya Uhuru” na “Mwongozo wa TANU”. Sababu kubwa ya uwepo wa nyimbo kama hizi pia ilichangiwa na the influence that the government had on radio stations and studio za kurekodi miziki. Kwani before the emergence of independent radio stations and recording studios in the 1990s, ilikuwa ni jadi kwa wasanii wa mziki kwenda Radio Tanzanian Dar es Salaam (RTD) – kwa sasa TBC kurekodi miziki yao. Lakini kabla ya kufanikisha hilo, wasanii wote walilazimika ku- submit their lyrics to a censor department at RTD, na mara nyingi, such lyrics zilifanyiwa mabadiliko kama they didn’t fit vision ya Ujamaa. Wasanii kama Mbaraka Mwinshee walipendwa sana na serikali na walipewa support kubwa sana kutokana na miziki yao kuwa perceived to be ‘socially and politically appropriate’.

  Bongo flava na rap zilipo emerge in early 1990s, artists no longer needed kuficha the meaning of their words na kwani sasa walipata uhuru wa kutoa maoni yao juu ya social, political and economic issues surrounding them. Following liberalization of the media, wasanii wengi wakaanza kwenda to independent radio stations and recording studios that were rapidly mushrooming in the early 1990s. Consequently, lyrical messages became more direct compared to enzi za dansi na taarab wakati wa Ujamaa au mfumo wa chama kimoja. Muziki wa rap, lwa mfano haraka ukapata a strong network of support from vijana kwani muziki ukawa jukwaa la vijana to promote and amplify their political and social views, na vile vile kuamsha wenzao across the country about the challenges of life. Mfano wasanii kama Roma Mkatoliki na nyimbo zake juu ya mafisadi, au wimbo mpya wa Izzo Business uitwao ridhiwani where anamweleza mtoto wa rais Kikwete – ridhiwani akamwambie baba yake adha wanayopata vijana. Yote haya yamechangia sana vijana kuamka, kupanuka mawazo na kufanya rational and informed decisions juu ya nini mchele na nini chuya.
  1. Sababu ya tano CCM kupoteza umaarufu: Jina la Chama yani CHAMA CHA MAPINDUZI
  Neno mapinduzi katika siasa na jamii ya Tanzania ya leo is too vague and unpractical kwani mtanzania wa kawaida, hususan hajaona mapinduzi yoyote katika maisha yake zaidi ya hali ya maisha kuwa nhumu siku hadi siku – iwe ni mkulima, mfanyakazi au mfanyabiashara ndogo ndogo. Hii ni tofauti na majina kama CHADEMA au CHAMA CHA WANANCHI. Haya majina meanings zake ni less vague, ni pretty much straight forward and practical katika maisha ya leo. Neno Mapinduzi linatuangusha CCM, ingawa lilikuwa na umuhimu mkubwa wakati wa Ujamaa kwani enzi zile tulikuwa tunazidi kulinda uhuru wetu wa kisiasa (wa bendera) na tulikuwa tunajitahidi kujitegemea yani kuwa a self reliant state. Katika Tanzania ya leo, Mapinduzi is hard to sell. Majuzi katika pita pita zangu pia nilishangazwa sana jinsi gani jina la Chadema lina mvuto mkubwa hata kwa vijana wasio na muda na siasa. Katika pita pita zangu jijini Dar-es-salaam na mwenzangu mmoja, tulishangazwa na mwana dada mmoja tena mwenye elimu ya chuo kikuu pale tulipomuuliza kwanini anaipenda Chadema kwani alitujibu: “The name Chadema is just too sexy”.

  1. Sababu ya sita CCM kupoteza umaarufu: Rangi ya bendera ya Chama Pamoja na Suala la Jembe na Nyundo.
  Katika mazingira ya leo, its very interesting to find out kuna badhi ya watanzania ambao hawaipendi rangi ya kijani sio kwa sababu za kisiasa bali ushabiki wa yanga na simba. Lakini tukumbuke kwamba asili ya yanga was movement of Young Africans in urban areas, Dar-es-salaam in particular wakati wa kudai uhuru na ndio maana hadi leo hii timu ya yanga imekaa kisiasa zaidi kwani ukaribu wake na CCM ni wa kihistoria. By the way mimi ni Yanga damu damu.
  Ukiachilia mbali suala la simba na yanga ambalo halina uzito sana, rangi ya kijani katika bendera yetu inaashiria mimea au mazao. Implication yake ni nini? Wakulima wetu wengi wamekuwa na hali duni katika kipindi karibia chote cha miaka 50 ya uhuru, na suala hili limekuwa linatugharimu sana kisiasa CCM pamoja na serikali. Katika pita pita zangu huko vijijini, nilikuwa nawapa chemsha bongo watu kwa kuwauliza hivi bendera ya chama chetu ina rangi ngapi? Wengi walijibu mbili – kijani na njano. Lakini ukweli ni kwamba rangi ya CCM ni moja tu – kijani na hata katiba ya chama inasema hivyo. Mjadala huu ukapelekea niulizwe maswali, Je rangi ya kijani katika bendera yetu ya CCM na ile ya Tanzania zinawakilisha kitu gani? Nikawajibu haraka haraka kwamba ni mimea au mazao na ustawi wake. Baadhi ya wakulima wakaelekea kukerwa sana na suala la rangi ya kijani kuashiria ustawi wa mimea wakati kilimo chao kipo hoi kwa miaka 50. Utafiti huu ulinistaajabisha sana. Wapo baadhi ya wananchi wakatamka kwamba rangi za Chadema na CUF zina mvuto zaidi.
  Pia alama ya za jembe na nyundo zinaonekana kuwakera sana wananchi walalahoi kwani kuna baadhi walitamka kwamba chama kimetekwa na wafanyabiashara. Mwanakijiji mmoja alienda mbali zaidi na kutamka kwamba ni bora jembe na nyundo vigeuzwe kuwa noti ya elfu kumi na nyumba ya ghorofa ili tujue moja.

  1. Sababu ya saba CCM kupoteza umaarufu: Mfumo wa CCM (As an organization) ni wa kizamani.
  Mfumo wa chama chetu bado ni wa kizamani na haujabadilika sana tangia CCM izaliwe. This is contrary to any other organizations ambazo change is the only thing that remains constant ili to stay ahead of the competition. Chama chetu kwa sasa kipo too rigid, bureaucratic and highy hierarchical. Flat organizations tend to be more successful than hierarchical ones. Matokeo yake ni kwamba katika CCM watu wa juu ndio wanakuwa na maamuzi makubwa na wa chini wanakuwa watekelezaji wa maamuzi hayo wakati ukweli unabakia wazi kwamba nguvu ya chama ipo chini lakini viongozi wa ngazi ya chini wanazidi kutelekezwa. Tutalirudia hili baadae.

  1. Sababu ya nane CCM kupoteza umaarufu: Chama chetu kimeshindwa kusimamia serikali.
  Katika pita pita zangu nimegundua kwamba wananchi wengi wanaona CCM imeshindwa kuisimamia serikali juu ya ufisadi na ubovu wa sera za maendeleo kwa ujumla. Vijana wengi wanaona kiti cha mwenyekiti CCM taifa kina uhusiano zaidi na maisha yao ya kila siku kuliko kiti cha Urais. In other words, wanaona kwamba mwenyekiti wa CCM taifa ana influence kubwa zaidi kimaendeleo kuliko Rais wa nchi. Kutokana na hili, inatoa wazo kwamba kama kofia ya mwenyekiti wa chama taifa na ile ya Rais wa nchi zingetenganishwa zingeweza kumwokoa JK katika mtego huu kwani wananchi wangempunguzia mzigo wa lawama Rais wetu na kuuelekeza kwa mwenyekiti wa chama. Na mwenyekiti wa chama angeweza wajibishwa vizuri zaidi na Rais. Vyama vya siasa kwenye nchi kama marekani vimefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kutokana na kutenganishwa kwa kofia hizi mbili.
  Suala lingine la kugusia hapa ni la Sera na Dira ya CCM. Unlike miaka ya nyuma, leo hii ni vigumu kwa kijana kuelewa CCM inampeleka wapi. Wapiga kura wengi pia wamekuwa wanachanganya sera za serikali, dira ya nchi na ilani za chaguzi CCM. Wanashindwa kuelewa haya yanahusiana vipi. Ili kujijengea uelewa zaidi, vijana wengi wanaamua kuangalia zaidi ahadi wakati wa kampeni za urais pamoja na utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwani kama kigezo kikubwa kuelewa serikali inajiendesha vipi na vile vile kuchambua utendaji wa serikali. Ingawa CCM imekuwa inajitahidi kutekeleza ilani zake kwa kiasi kikubwa, bado impact ya utekelezaji huu kwa kijana wa Tanzania ni ndogo sana. Tuna mikakati mizuri sana ambayo hata wapinzani wamekuwa wanaiga lakini tatizo letu limebaki kuwa utekelezaji.
  Tatizo lingine ni kwamba leo hii CCM inaendesha nchi katika mifumo miwili, wa kwanza ni ule unaotokana na Azimio La Arusha na wa Pili Azimio La Zanzibar. Hii inaleta conflict of interest kwani kwa upande mmoja, kiongozi anaruhusiwa kuwa na mali n.k akiwa kazini lakini kwa upande mwingine linakuwa tatizo. Vile vile katika siasa zetu ndani ya chama, Ujamaa na kujitegemea still features but in practice, hakuna kitu. Inasikitisha kusikia vijana wa UVCCM katika salam zao wakiimba siasa za Ujamaa na kujitegemea wakati in practice hazipo.
  Pengine nimalizie sehemu hii kwa kusema kwamba watanzania wengi walishakata tama na serikali ya CCM (suala la hudua za kijamii) baada ya Mwl. Nyerere kuondoka madarakani mwaka 1985 kwani ni wakati huu ambapo mageuzi ya kiuchumi yalianza kuja kwa kasi na huduma za kijamii zikaanza kutoweka kwa kasi pia. Suala la Ujamaa na kujitegemea likabakia kujitegemea sio kama jamii bali kivyakovyako kimaisha ili mradi chakula kiingie tumboni. Kutokana na hali hiyo wananchi wengi wakaanza kujitafutia huduma wenyewe mfano kiafya by kujilipia wenyewe in private hospitals au kwenda hata kwa waganga wa jadi kwa wale waliokosa uwezi kifedha; in terms of employment, pakatokea massive lay-offs as the government used to be the major employer in the modern sector – wengi wakaishia kwenye informal sector kama mama lishe, machinga n.k. Kwa wale waliobahatika kubaki makazini, real wages zilishuka kwa kasi kwani Basic Salary haziku match na uhalisia wa gharama za maisha, Kwahiyo wakaanza kupunguza kujituma katika kazi zao rasmi na kutumia muda mwingi kwenye informal income generating activities; kuna wengine wengi pia ambao walianza kujisaidia kwa kuiba fedha za serikali, rushwa ikakithiri n.k. Kutokana na hali hii, by 1992 when mfumo wa vyama vingi ulipoingia, wananchi wengi walishakuwa disappointed na CCM kwani baada ya miaka yote ya kujitolea mashambani na makazini kwa bidii mwisho wake ikaishia kuwaweka katika hali mbaya zaidi ya kiuchumi. Pampja na yote haya, wananchi wengi waliendelea kuunga mkono CCM after 1992, sio kwasababu eti sera zetu zilikuwa na tija kwao bali kutokana na perception iliyokuwepo kwamba upinzani utaleta uvunjaji wa amani na utulivu. Kwa kuunga mkono utawala wa CCM iliwaletea matumaini kwamba angalau the future was more predictable – notion kwamba maisha ya tabu lakini amani uhakika wa amani upo.

  1. Sababu ya tisa CCM kupoteza umaarufu: Kufutwa kwa mishahara ya watendaji muhimu wa chama.
  Wakati wa mfumo wa chama kimoja, watendaji wa CCM walikuwa wanapata malipo ya aina fulani kila mwezi ili kuongeza ufanisi wao wa kazi. Lakini baada ya mfumo wa vyama vingi, suala hili kisheria ilibidi libadilike. Katika vitabu vya chama (CCM) imewekwa bayana kabisa kwamba “kufuatia mfumo wa vyama vingi – baada ya mwaka 1992, shughuli zote za chama zitakuwa zinafanywa kwa kujitolea”. Hili limepunguza sana ufanisi wa viongozi wa ngazi za chini kwani wanaolipwa ni makatibu kuanzia wilaya kwenda juu. Kwa wale wa kwenye kata na matawi, malipo ni kama hakuna. Kutokana na hilo, viongozi wa ngazi za chini ambao kimsingi ndio nguzo ya chama chetu hawajishughulishi/hawajitumi sana kujenga chama kama enzi za chama kimoja. Na hili linachangia sana kwa CCM kupoteza mvuto katika matawi na mashina kwani huko ndiko wanapoishi watu. Ili kujikimu ki-maisha, viongozi wengi wa ngazi za chini wanaishi kwa ujanja ujanja tu wa posho za vikao, au Mheshimiwa Mbunge au Diwani awakumbuke kwa lolote, na wengine wengi hutegemea mapato ya miradi ya chama katiba mazingira yao ya kazi. Kwa mtazamo wangu suala hili halistahili kufikia hali mbaya kiasi hiki kwani hivi majuzi Katibu Mwenezi wa CCM Nape Mnauye alielezea kushangazwa kwake kwamba mali (assets) za chama nchi nzima zinafikia thamani ya Shilingi Bilioni 50. Zikiendeshwa vizuri, viongozi wa chama wanaweza kuangaliw vizuri, hence chama kuimarika kwenye mashina na matawi.


  1. Sababu ya Kumi CCM kupoteza mvuto: Kusahaulika kwa viongozi ngazi za chaini - wajumbe wa nyumba kumi kumi
  Suala hili linaendana kidogo na hilo la hapo juu ila nimeonelea niliweke tofauti kidogo. Kimsingi, wajumbe wa nyumba kumi kumi ndio nguzo ya Chama Cha Mapinduzi kwani wanachama wa CCM wapo kwenye matawi na mashina ambapo wajumbe ndio wahusika wakuu kiutendaji. Wanachama hawapo kwenye kata, wilaya au mkoa, ni kwenye matawi na mashina. Lakini licha ya viongozi wa mashina kuwa nguzo yetu muhimu ndani ya CCM, wamesahaulika kabisa katika enzi hizi. Wanakuwa na umuhimu mkubwa wakati wa kura za maoni na chaguzi kuu pekee yake. Suala linguine pia ni kwamba, viongozi hawa wanapochukuaga maamuzi mikononi mwao, mara nyingi hayaheshimiwi na ngazi za juu. Mfano mzuri ni matatizo yaliojiri katika mchakato wa kura za maoni za wabunge na madiwani 2010. Katika jimbo la kawe ambapo ninaishi, viongozi wengi wa matawi na mashina baadae wakati wa kampeni walikuja vutiwa sana na sera za Mgombea Kipi Warioba ingawa kabla ya kampeni kuanza hakupewa nafasi kabisa ya kushinda. Viongozi hawa hatimaye wakaamua kwamba Kipi ndio chaguo lao katika kura za maoni na hatimaye uchaguzi mkuu Kwahiyo wakaamua kumuunga mkono na kumfanyia kampeni. Lakini maamuzi ya viongozi hawa wa mashina yakatupwa na uongozi ngazi za juu ambapo mshindi wa pili Bi. Angela Kiziga akatangazwa kuwa mshindi na hivyo mgombea wa CCM. Viongozi wa matawi na mashina wakaona wamedharauliwa na wakaapa kuelekeza nguvu zao kwa Halima Mdee wa Chadema ili mradi mgombea wa CCM Angela kiziga asipite. Na kweli, Halima Mdee akashinda na nilishuhudia umati wa wana ccm wakiandamana kusherekea ushindi wa Mdee kwa maandamano na kucheza ngoma, wakiwemo wajumbe wa wengi sana wa nyumba kumi kumi kutoka jimbo la kawe. Kimsingi, Halima mdee alishinda kutokana na hasira za wana ccm kuchakachuliwa mgombea wao Kipi Warioba kwani katika jimbo la kawe, wanachama wa chadema per se kiukweli sio wengi. Lakini ukweli pia unabakia wazi kwamba Halima Mdee is very competent for the job. Mimi ni mwana CCM lakini nathubutu kusema kwamba Kawe tumepata Mbunge anaestahili kutuongoza – Tanzania Kwanza, Siasa Baadae. Uchapaji wake wa kazi unanifanya nijivunie kuwa mkazi wa Kawe.

  1. Sababu ya kumi na Moja CCM kupoteza mvuto: Kutokuwepo kwa Baraza kuu la Vijana Taifa Tanzania.
  Tangu tuingie mfumo wa vyama vingi vya siasa, kumekuwa na wito wa kuunda baraza kuu la vijana taifa ambalo lilitarajiwa kuangalia zaidi maslahi ya vijana kitaifa na sio kichama. Inawezekana kukawia kuundwa kwake ni suala la kisiasa zaidi lakini imepelekea perception among many youths kwamba serikali imeamua UVCCM kuendelea kuwa chombo kikuu cha kushughulikia masuala la Vijana kitaifa. A good performance ya UVCCM ingeweza kutusaidia CCM kupata more legitimacy kutoka kwa vijana lakini ni bahati mbaya UVCCM ya kina Seif Khatibu, Guninita, Nchimbi sio ya leo kwani leo hii UVCCM imekosa dira na mwelekeo. Kwa hali hii, kutokuwepo kwa Baraza la Vijana Taifa does more harm than Good to CCM na serikali. Serikali ilikosa nafasi muhimu sana ya kuanzisha chombo hiki mapema na kukitumia vyema to meet needs and aspirations za vijana Tanzania, kitu ambacho kingeongeza mvuto wa CCM na serikali yake kwa vijana Tanzania.Kwa sasa, suala la Baraza hili kuingia mikononi mwa vijana wanaounga mkono upinzani ni kama halikwepeki. Vile vile BAVICHA is perceived as being more progressive that UVCCM. Vijana wamekosa watetezi wao na pia platform to air their views and concerns. Upinzani ulisahona weakness hii ya CCM na serikali yake and decided to capitalize on this opportunity vilivyo.

  1. Sababu ya kumi na mbili CCM kupoteza mvuto: Exposure ya Vijana on What’s happening outside Tanzania
  Liberalization katika media sector hususan T.V na radio kumechangia sana kuwapa vijana exposure on what is happening nje ya Tanzania, kisiasa, kiuchumi na kijamii. Vijana wengi wamejionea wenyewe jinsi gani upinzani katika nchi kama Zambia, Zimbabwe, Kenya, Madagascar unavyofanikiwa kushinikiza na hatimaye kuleta mabadiliko, huku vijana wakiwa ndio chachu ya mabadiliko hayo. Vilevile vijana wengi wamekuwa wakishuhudia harakati za vijana wenzao kuleta mageuzi na mapinduzi huko Misri,Tunisia, Algeria, Morrocco, Yemen, Syria. Ikumbukwe kwamba mageuzi yanayotokea nchi za kiarabu yanaongozwa na vijana wasomi ambao hata Tanzania wanaongezeka kwa kasi sana. Hili ni timing bomb ambalo CCM bado tuna uwezo wa kulitegua otherwise hali itakuwa mbaya kabla hata ya 2015.

  1. Sababu ya kumi na tatu CCM kupoteza mvuto: Failure ya CCM to groom viongozi bora.
  Enzi za Nyerere, CCM ilijitahidi sana to groom viongozi wake ambapo UVCCM lilikuwa ni tanuri la kupikia viongozi wa baadade. Viongozi kama JK, Lowassa, Ulimwengu, Lukuvi, Seif Khatib, Nape na wengine wengi wametokea UVCCM. Tofauti na zamani, leo hii hatuna viongozi wengi vijana wenye maadili na sifa za uongozi. Kutokana na tatizo hili, vijana wetu wengi wenye nafasi katika chama ni bora viongozi na sio viongozi bora. Hatuna viongozi wengi wanaopewa nafasi by merit na badala yake wanapata nafasi kwa kutumia pesa, kufahamiana, au kubebana. Wengi wa namna hii utendaji wao kwa chama chao an nchi yao unakuwa below standard sababu wanaingia kuwatumikia waliowapa nafasi za uongozi. Chadema have managed to capitalize on our weakness. Katika miaka ya hivi karibuni, wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa to groom competent leaders - vijana kama Zitto, Mdee, Mnyika, Lissu na wengine wengi. Kuwa na viongozi competent namna hii ni muhimu sana katika Tanzania ya leo ambapo inakadiriwa kwamba asilimia 70 ya watanzania hawajavuka miaka 30.
  Vijana wengi wanawangalia kina Zitto, Mnyika kama their inspirational figures, especially given the unequivocal level of success katika harakati zao za kupigania maslahi yao na ya nchi kwa ujumla. Vijana wengi sasa wanahisi wamepata viongozi wa kuwasikiliza. Hivi sasa, Zitto, Mnyika, Mdee wanazidi kuonekana kama standard ya viongozi bora, not just among viongozi vijana Tanzania bali pamoja na wazee. CCM tumeanza kubadilika katika hili kwa kuingiza vijana katika nafasi za juu lakini inabidi tukimbie wakati upinzani wanatembea.

  Nikiwa bado katika suala la viongozi bora versus bora viongozi, kwa kiasi kikubwa viongozi wetu wengi ndani ya CCM wamepitwa na wakati na hawana elimu inayohitajika kuongoza Tanzania ya leo. Mfano mdogo tu ni kwamba ukiangalia wengi wa watendaji wetu katika chama, karibia asilimia 90 (Makatibu wa CCM wilaya na Mikoa) ni darasa la Saba, la nane, kumi au kidato cha nne. Hawa wanawaongoza vijana wa Tanzania ya leo ambao wengi wao wamesoma na ndio washauri wakuu wa wazee wetu huko vijijini kuhusu masuala mbali mbali ya kiuchumi na kisiasa (kwani kijamii bado wazee wameshika usukani). Mfano rahisi na wakaribu – kushindwa kwa wanafunzi wa vyuo kuja Dar-es-salaam kupiga kura October 2010 brought more harm than good for CCM kwani utafiti unaonyesha kwamba kubaki kwao mikoa husika walisaidia sana Chadema kupata kura nyingi za ubunge na urais. Tuzidi kukumbuka kwamba leo hii, nyumba nyingi Tanzania aidha ina mtoto, ndugu, rafiki au jirani aliefika au anaesoma elimu ya chuo kikuu.


  1. Sababu ya Kumi na Nne CCM kupoteza umaarufu: Mbinu zinazotumika kupata Rais, ubunge na Udiwani.
  Hili limeshasemwa kwa ufasaha kwahiyo sitalirudia. Kwa kifupi, mbinu zilizopo zinazaa viongozi wanaongia kwa pesa na kuishia kutupatia Bora Viongozi badala ya Viongozi bora. In addition, chaguzi zetu zimetawaliwa na makundi utadhani chama chetu cha CCM sio kimoja tena. Chanzo cha tatizo hili ni mmomonyoko wa maadili, uroho wa madaraka, fikra za tumbo kabla ya nchi pamoja na kufilisika elimu ya uongozi miongoni viongozi wetu wengi ndani ya chama.

  • Dhana ya Kujivua Gamba
  Ukweli unabakia wazi kwamba dhana hii imejaa ushabiki kuliko uelewa wa the issue at hand. Kwa uelewa wangu ambao pengine unaweza kuwa mdogo sana, katika hotuba yake kwenye kilele cha maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCM, nilisikiliza hotuba ile mwanzo hadi mwisho na Mwenyekiti wa CCM Taifa alizungumzia kujivua gamba in the context of kwenda na wakati. Kwa mtu ambae ulisikia hotuba ile moja kwa moja na sio kuisoma magazetini au kuhadithiwa, ni rahisi kutambua kwamba JK hakumaanisha kwamba kujivua gamba maana yake ni kufukuza viongozi wasiokubalika, instead he meant to do whatever it takes to transform the party and coming up with innovative ideas to modernize chama. Suala la kufukuzana ndani ya chama lilikuja ibuka tu ndani ya vikao vya baadae and it remains to be a by – product of kujivua gamba but it’s not the keystone of gamba.

  Ukweli unabakia kwamba dhana ya Gamba ni dhana nzuri sana because it’s all about change. Chama chochote huwa kinahitaji changes aidha kwa ajili ya ku stimulate growth au kurekebisha makosa kadhaa. Chadema kwa mfano kimepitia transformations nyingi kufikia hapa ilipo na hiyo ilikuwa ni dhana ya gamba vile vile kwa maana ya transforming and modernize the party au in other words realizing change is the only thing that’s constant if you want to stay ahead of competition. Chadema ya 1995 sio Chadema ya 2005 na sio Chadema ya 2010 na haitakuwa chadema ya 2015 na hii inatokana na Chadema kujivua gamba kila wakati. Ninadiriki kusema hapa kwamba kwa wasio elewa dhana ya gamba watakuja na shambulizi kubwa sana juu ya hoja yangu hii.

  I personally do not think suala la gamba ni suala la ufisadi pekee kwani ufisadi is ubiquitous – yani lipo kila mahali, na litaendelea kuwepo chini ya chama chochote kwa muda mrefu sana, kama lilivyo nchi hata zilizoendelea. Kitachobadilika chini ya utawala mwingine mfano wa Chadema, CUF etc iwapo watafanikiwa kukamata madaraka ya nchi, itakuwa pengine ni the magnitude ya ufisadi and implementation ya anti – ufisadi strategies. Otherwise tumeona katika nchi nyingi zilizotutangulia kimageuzi jinsi gani vyama vipya viliingia kwa sera za kumaliza ufisadi lakini viongozi hao hao kuishia kuwa mafisadi mara tu walipopata uongozi wan nchi .Ndio maana uamuzi wa Chadema kugundua kwamba mtaji wao haupo kwenye ufisadi pekee ni mzuri kwani kuna masuala mengine mengi muhimu zaidi kuleta Maendeleo na wameanza kuyafanyia kazi.

  Pia nisema kwamba suala la gamba limekaa kishabiki zaidi kwani ni desturi yetu watanzania kufurahia kuona mwenzako anaanguka hata kama anguko halina maelezo yanayojitosheleza. Hata Jenerali Ulimwengu amelizungumzia hili katika current issue ya RAI. Lakini hii haina maana kwamba siungi mkono mafisadi kutolewa, ila napinga approach ya kuwatoa just because umma una perceive ni mafisadi. Sio sahihi kumfukuza mtu kwenye chama sababu tu ni mtuhumiwa. Kabla ya kumfukuza, ni lazima kiongozi huyo apewe nafasi ya kujieleza kwani ni haki yake ya msingi. Wapo wanaosema kwamba tuhuma za kisiasa sio lazima ziwe za kimahakama. Nakubaliana na hilo ndio maana viongozi huwa wanajiuzulu na suala linaishia hapo. Lakini hili la kufukuzana ndani ya chama ni jipya na ni la hatari. Kwa kifupi, kujiuzulu kwa tuhuma ni sahihi, lakini kufukuza mtu ni suala linguine, ni muhimu haki itendeke na wapewe nafasi ya kujieleza ili tusije fanya maamuzi ya hisia na ushabiki. Tuelezwe tuhuma zao ili tuzijue na wao wajieleze ili wananchi tupime. Otherwise tujiulize, hata ndani ya vyama vya upinzani, ni wangapi watapona kutokana na tuhuma based on perception kwani zipo nyingi. Mfano, Chadema is perceived kuwa chama cha wachaga etc. Wananchi wakihukumu based on this perception?

  Kwa mtazamo wangu, kujivua gamba iwe zaidi:
  • To get rid of viongozi wazee na wenye upeo uliopitwa na wakati.
  • To modernize the party in terms of organizational behavioral issues.
  • Kuwadhibiti walaji wa pesa za umma katika ngazi za kata, wilaya ambao wanajulikana wazi na ushahidi upo wazi.
  • Kuwatoa viongozi mafisadi katika nafasi zao lakini baada ya kuwapa nafasi ya kujieleza, sio kushughulikiana based on perception.
  • Tuachane na tabia ya kupeana kazi ndani ya chama kwa njia za upendeleo kama vile undugu, urafiki, na badala yake uteuzi au ajira ziwe based on merit ili wanachama wote waone chama ni chao, sio cha wachache.
  • Ni muhimu viongozi wa chama, haswa ngazi za chini kuacha kuwa miungu watu.
  Chama kama Chadema kiangalie masuala haya kwa ukaribu sana kwani kwa sasa kwasababu chama chao kipo katika growth phase i.e. enjoying increasing returns, mengi hayaonekani mpaka pale chama kitakapofia constant returns ambapo umaarufu au growth utafikia kileleni mwa bell curve i.e. point of bliss/ saturation point/steady-state. This is a normal process. Being at a steady – state ni vizuri na hapo ndipo change (kujivua gamba) becomes important ili kusonga mbele katika ushindani wa kisiasa. Issue such as transparency, increased participation/ involvement ya wanachama in decision making, delivery ya sera, kuondokana na nepotism, na kuishi kwa dira on a day to day basis ni muhimu kuwa effective in a steady-state.
  Kwetu sisi CCM imetuwia vigumu to maintain us at the steady – state and we are in the brink of entering into a decline stage if we don’t take urgent decisions now and leave important decisions for later.

  Changamoto facing CCM Vis-à-vis Chadema
  • Based on the account presented above, it is obvious kwamba Chadema is perceived more as a progressive party na CCM more of a regressive party. CCM needs to reverse this trend.
  • When it comes to mass support, Chadema wana fan-base kubwa kuliko loyal-base na CCM tuna loyal-base kubwa kuliko fan-base. Uanachama wa siasa traditionally unaanza na ushabiki, then tararibu mtu unabadilika kuwa loyal to that party. Lakini the fact remains kwamba chadema has more fans than loyal supporters but their fan base is shrinking faster and loyal base growing faster; CCM still has a larger loyal-base than Chadema but both our fan-base and loyal-base are getting depleted at a high rate. Kielelezo kizuri juu ya loyal-base versus fan-base ni an examination on how wapiga kura wengi Tanzania ya leo wamegawanyika sana when it comes kupigia kura chama versus kupigia kura candidate. Hii ni indication kwamba we are still an infant when it comes to democracy.
  Kwa kumalizia, pengine nigusie suala la wagombea urais 2015. Nakubaliana na Reginald Mengi kwamba mjadala wa hili suala hauna tija katika Maendeleo ya taifa na kwamba kwa sasa tuzungumzie yale yenye tija zaidi. Lakini kwa mtazamo wangu finyu, ukweli unabaki palepale kwamba mwisho wa uchaguzi mmoja ndio mwanzo wa uchaguzi mwingine provided the process doesn’t damage chama husika or governance ya nchi kwa ujumla. Vinginevyo hata ligi kuu ya Uingereza ikiisha kwa mfano mwezi wa aprili, kipindi kati ya aprili na agosti huwa ni cha mshike mshike nani asajiliwe etc ili kujipanga kwa msimu unaofuatia. Siasa nazo ni hivyo hivyo. Ndio maana Chadema nadhani wamegundua umuhimu wa kuliweka taifa katika hali ya uchaguzi baada ya uchaguzi wa 2010, jambo ambalo hawakuwa wanalifanya huko nyuma. Mkakati huu utasaidia hata sisi CCM kuwa makini katika kipindi chote (2011-2015). Ni mkakati mzuri ili mradi haipelekei uvunjifu wa amani na utulivu. Lakini suala linabakia pale ambapo mtanzania anahimizwa kuwa katika amani na utulivu huku akiwa na njaa; hapa amani na utulivu vikipotea wa kumlaumu ni nani, upinzani? CCM? Serikali? au wananchi wenyewe? Vinginevyo kinachochangia Chadema kupata mvuto katika mikutano yao ya hadhara, particularly vijana ni equation ya amani – utulivu – njaa kali pamoja na zile sababu kumi na nne hapo juu.
  Nimalizie kwa kusema kwamba, kwa upeo wangu ambao upo informed na magazeti mbali mbali pamoja na threads za humu ndani ya JamiiForums, inaonekana mwaka 2015 CCM tutakuwa na wagombea wengi sana na watagawanyika katika makundi makuu matano:
  1. Wagombea wataotumia jina au nafasi ya Rais atakaekuwa anamaliza muda wake.
  2. Wagombea ambao ni watuhumiwa wa ufisadi (by perception) au watakao simamishwa na kuungwa mkono na watuhumiwa wa ufisadi (by perception).
  3. Wagombea wapambanaji dhidi ya ufisadi au watakaoungwa mkono na hawa wapambanaji.
  4. Wagombea majeruhi wa uchaguzi wa 2015.
  5. Na independent candidates ambao hawatakuwa katika makundi tajwa hapo juu na badala yake watachukua tu fomu kujaribu bahati zao.
  Kwa mtazamo wangu, njia pekee ya Chama Chetu (CCM) kushinda mwaka 2015 mbali ya kuyafanyia kazi mambo kumi na nne niliyoainisha hapo juu should also involve the following:
  1. Kwanza, tuondokane na siasa za mtu wetu na badala yake kuegemea zaidi katika siasa za chama chetu au nchi yetu. Hapo ndipo tutapata kiongozi bora na sio bora kiongozi. Tujifunze kilichojiri katika kura za maoni ambapo viongozi wa CCM walidhania wanaemtaka wao basi ni huyo huyo wapiga kura watamchagua.
  2. Katika mchakato wa kumpata mgombea wa 2015 tujitahidi kuepuka kuangalia kabila, dini, kanda au zamu ya huku au zamu ya wale; pia utamaduni wa kwamba huyu hana mizizi au uzoefu ndani ya chama. Wapiga kura wengi, may be close to 80% watakuwa ni mixuture ya waliokulia na kuzaliwa ndani ya mfumo wa vyama vingi (i.e. after 1992); hawajui TANU wala Afro shiraz party ni nini;hawajali nani ana uzoefu katika chama; hawajui au kujali suala la amani na utulivu wakati hali halisi ni kwamba njaa zinawauma; wanachojali ni kupata kiongozi mwenye mvuto kwao, asiye na kashfa na mwenye ushahidi wa kuwa mchapa kazi. Kwahiyo, ili CCM tupate mgombea wa kutuhakikishia ushindi mwaka 2015, tuangalie kwanza nani anakubalika na wananchi huko nje, na hata kama hana mizizi mirefu au uzoefu ndani ya chama, au hata kama sio mwenzetu, huyo huyo ambae jamii inamkubali tumchukue na kuanza kum groom tena mapema, san asana baada ya uchaguzi wa CCM mwakani. Lakini kuna hatari ya mtu huyu kuchafuliwa tena na sisi wenyewe kwasababu ya siasa za mwenzetu kwanza badala ya chama chetu au taifa letu kwanza. I am not trying to be pessimistic lakini kuna dalili kwamba siasa za mtu wetu will continue to overshadow siasa za chama chetu au nchi yetu. Hilo ndilo litakuwa beleshi lenye mchanga wa mwisho katika kaburi letu CCM. Kama mwana CCM, nimelelewa kusema mambo bila uoga ili mradi sikashifu mtu na sivunji sheria zilizopo. Isitoshe, hoja ya kusubiri kuyazungumza haya ndani ya vikao vya chama hainigusi kwani mimi ni mwana CCM wa kawaida tu kama kina jumbe, mzee rashidi na mama mazinge mitaani kwetu kinondoni. Vinginevyo, nitabakia kusema ukweli daima kwani fitina kwangu mwiko.
   
 2. A

  Analytical Senior Member

  #2
  Jun 26, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Very informed, analytical and balanced
   
 3. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,494
  Trophy Points: 280
  Well written. Niongezee kitu kuhusu chama kushindwa kuisimamia serikali. Ukweli ni kwamba, CCM imeshikwa na kiwewe kutokana na upinzani iliyoupata ktk uchaguzi wa 2010 kiasi kwamba wameamua kufanya mambo kwa ushabiki badala ya uhalisia. Hili litawaharibia zaidi. Mfano, kuna mambo mazuri ambayo watu wa upinzani wanashauri serikali itekeleze, lakin kwa kuhofia kuwapa 'ujiko', wabunge wa CCM wanapinga na kutokana na wingi wao,wanafanikiwa. Tena wanapinga hata kama hawaamini wanachopinga.

  Matokeo yake mnawafanya wabunge wa upinzani waonekane ni wazuri zaidi na wanawajali zaid wananchi. Mfano suala la posho, huu ni mtego mbaya sana kwenu. Wananchi wanaona kuwa kumbe nyie mnapenda kuishi kifahari wakati wengine hata mlo ni shida. Pia, naona mnapitisha kugombea watu ambao sio makini, hawawezi kujenga hoja na kuisimamia vizuri. Umeona Kigwangala leo anampiga Lissu kwa point za kwenye DS, kesho yake analalamikia mgodi ulioko jimbon kwake kwamba hauna faida na kumpongeza tena Lissu.
   
 4. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  We nawe sasa ulikuwa unasababu gani ya kuquote li riwaya lote kama ulikuwa unataka kusema hivi tu.
   
 5. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,479
  Likes Received: 761
  Trophy Points: 280
  Nina swali moja tu? Hivi unalipwa au unafanya bure tu? Khaaa hata ukininunulia bar mbili na kaunta nne za pombe siwezi kumaliza kusoma.
   
 6. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mchambuzi haya ni maandiko mazuri kwa chama chako ila sina hakika kama umewapelekea wahusika for actions. Nikisummarize maelezo yako ni kwamba CCM yenyewe ndiyo iliyojififisha kisiasa hawana wa kumlaumu na hawatakiwi kulaumu maana wao ni cause na vile vile effect.

  Mkuu Mchambuzi hicho chama chenu CCM hakina jipya kwa watanzania, na the only reform it needs now kubomolewa choote halafu kikae benchi kama miaka 10 hv, huwezi kufanya reform wakati viongozi wa CCM walio wengi bado wanafikiria in the context ya mwaka 47. Infact CCM inaangaliwa zaidi kama ajira na viongozi wake na si dira ya kupropel aspirations za watanzania.

  Kingine kikubwa ni huyo mwenyekiti wenu, he's the biggest liability, they guy can not lead period!!!!. Na kwa utaratibu wenu mnaendelea kumuamini na kutaka kuwaminisha watanzania (uliosema ni makini kiasi flani siku hizi) kwamba anafaa, anaweza na ni mojawapo ya viongozi bora Tanzania imewahi kuwapata. Facts on the ground, completely different. Hivyo mnajikuta chama chenu kinaoneka na ndivyo kilivyo "cha kinafiki" Leo tunaambiwa eti mwenyekiti wenu nik mahiri ila anaangushwa na wasaidizi wake. Wasaidizi kimyaaaaaa. Lakini utashangaa haohao wanaosemwa kumuangusha eti wanatafuta ridhaa ya watanzania kukubalika 2015.
  <br>
  All in all CCM as of now has overstayed, irrelevant and need to go! Nilishasema kwenye thread flani watanzania wasirubuniwe eti mpaka hapo CHADEMA itakapokuwa perfect ndiyo iaminiwe kuongoza nchi. Huo ni urongo wa karne. CCM si perfect na haijawahi kuwa perfect. TANU haikuwahi kuwa perfect, MMD, ODM and ANC likewise. Lichama hilo limeshindwa na litaendelea kushindwa kwa sababu wanaoliongoza ni watu wa kushindwa na hawajawahi shinda. CCM kama ilivyo sasa will never have and attract the mavericks!

  Tukija kwenye hiyo falsafa yenu ya kuvua gamba, kama ulivyosema mwenyewe kwamba the philosophy behind ni kufanya mabadiliko na kukifanya chama kiende na wakati. Hivi unafikiri porojo hizi zingeresonate kwa watanzania? How many programs, reforms and promises zimeshasemwa na CCM in the last 50 years?. At least bwana mdogo Nape alivyoamua kwenda na hiyo different version ya kujivua gamba it did steal the show from CDM for few weeks.

  Hapa chini ntamquote Eng. Burton Bukuku -"Mimi na familia yangu tunaikataa CCM na kazi zake zote"

  Good luck though bro!
   
 7. M

  Mdomo Mwepesi Member

  #7
  Jun 26, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Nimesoma makala yako ndefu jinsi unaelezea kupungua umaarufu kwa CCM, nasikitika kusema kwamba hujaeleza sababu yoyote iliyopelekea CCM kufifia kisiasa. Ulizotaja kuwa "sababu" za kufifia kisiasa kwa CCM siyo sababu bali ni MATOKEO ya kufifia kisiasa kwa chama.Pamoja na kutoa angalizo mapema kuwa TANZANIA kwanza na Siasa baadaye lakini umefanya kinyume na angalizo lako.Umetoa sababu za kisiasa badala ya ukweli halisi. Sijui kama umefanya hivyo kwa kukusudia au huo ndio ukomo wa upeo wako katika kujenga hoja. Tusitafute mchawi hapo

  Sababu zinafahamika kabisa hata kwa kijana wa kidato cha kwanza. Ukweli ni kwamba CCM imeshindwa kukidhi kiu ya maendeleo ya Watanzania licha ya kupewa dhamana ya kuiongoza nchi zaidi ya miaka 40. Watanzania wanahitaji maendeleo lakini CCM inazidi kumsukuma mtanzania katika dimbwi la umaskini huku wale wote wanaojiita viongozi wakiendelea kunawiri na kushibisha matumbo yao. CCM badala ya kumletea mtanzania maendeleo imekuwa ya kumnyang'anya maendeleo. Wananchi wanahitaji vitendo siyo maneno tena

  Sehemu kubwa ya sababu ulizozitoa ni masuala ya kiutawala ndani ya chama ambayo hana uhusiano na wananchi ambao si wanachama wa CCM lakini wamekipa dhamana ya kuwaongoza. Suala la kuondoa mishahara ya watendaji, jina la chama, nembo na uchaguzi wa kumpata mgombea ndani ya chama havina uhusiano na kuleta maendeleo kwa wananchi: kitu ambacho kitasabisha kupendwa kwa chama na wananchi.

  Hivi unataka kutwambia kwamba mapenzi ya watanzania kwa timu yao ya mpira Taifa Stars yamepungua ni kwa sababu ya
  1. jina la timu (Taifa Stars which is not sexy),
  2. rangi na nembo ya jezi,
  3. mfumo mzima unaotumika kumpata kocha wa Taifa Stars, na wasaidizi
  4. utaratibu wa kuchagua wachezaji
  5. Kuondolewa kwa michezo katika shule za msingi na sekondari ( japo imerudishwa hivi karibuni)
  6. Kupungua kwa posho au mishahara kwa kocha, wachezaji na watendaji na wafanyakazi wa TFF
  7. Kutokuwepo kwa timu za vijana ambao wa wachezaji wa baadaye nk.


  Mashabiki wa timu yetu ta Taifa- Taifa Stars wamepoteza mapenzi na imani kwa timu kwa sababu haiwapi watanzania kile wanachotaji-"ushindi". Kila kukicha ni kufungwa na baadaye sababu nyingi za kufungwa. Hivi ndivyo CCM ilivyo, imeshindwa kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli, badala yake ni visingizio na sababu za kipuuzi.

  Kama nawe ni mshauri wa chama basi nakupa pole kwa kushindwa na kuwa na akili ya kawaida ya kuelewa kuboronga kwa chama chako hadi kupelekea wananchi kukichukia.
   
Loading...