Top 10 Airliners for 2016 - Hongera ATC!

Top 10 Airliners for 2016 - Hongera ATC!

Kwa Africa nawakubali SAA kisha Air Maroc pia Egypt Air
 
Huu uzi wa uchochezi ,mwanafunzi wa mwisho apewe zawadi? ATC?
 
Pengine ada ya kusomea u-pilot ni kubwa kutokana na walimu ni ghali, mafunzo kwa vitendo ni aghali maana inabidi kuwa na simulator+ndege halisi pia. Kiukweli nimeweka nadhiri angalau mtoto wangu mmoja aje kurusha ndege nitafanya kazi na ku-save sana aje arushe midege ya maana duniani huko
 
afrika sisi tunasindikiza kwenye suala la ndege za biashara kwa mbaali labda SOUTH AFRICAN AIRWAYS lakin KQ majanga matupu chakula chenyewe wanatoa kimagumashi nilipanda AMSTERDAM, Schiphol to NAIROBI (JKIA) wakaanza kugawa chakula kikaishia siti za katikati sisi wengine huku siti za nyuma wakatukaushia. Duuh masaa 8 angani kavu kavu!
 
Nimefika pazuri mpaka sasa nina laki 6 tsh. Nikiendelea ku-save mpaka 2027 nitakuwa na ada na ziada ya kusomesha mwanangu.
 
Nimefika pazuri mpaka sasa nina laki 6 tsh. Nikiendelea ku-save mpaka 2027 nitakuwa na ada na ziada ya kusomesha mwanangu.
 
ATC ikipata uongozi usioingiliwa na wanasiasa tunatoboa kabla ya 2020.
 
Ifike mahala watu wapewe kazi kwa sifa zao kazini. Mtu mwenye experience na biashara.
 
hivi bodi ya mikopo wanatoaga mikopo ya kwenda kusomea urubani?
 
Back
Top Bottom