Toka mtandaoni : Kizungumkuti cha ndoa

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
140,613
2,000
*DUH AMA KWELI NDOA ZINA MAMBO*
Kuna kijana alikua anajua
kuwa mke wake
anatoka nje ya ndoa basi
akamwuliza mke,
mkewe akakataa,
akamwambia baba yake akaambiwa na babaake tulia
mwanangu ndoa
zina mengi! akawa kila siku
analalamika kwa
babaake, mwisho babaake
akamwambia basi ntakusaidia. Itabidi ujifanye
unaumwa sana hoi
hujiwez halafu
nitakuonyesha jawabu!
Basi kijana akajifanya
anaumwa mzee akaitisha kikao cha ndugu wote pande
2,
Mzee akaanza kueleza
jaman kijana wetu
anaumwa amepata ugonjwa
wa utata hospital zote umeshindikana hivyo
tumeenda kwa mganga
wa jadi amenipa dawa na
ina masharti, inatakiwa
atakaye iandaa hii dawa
awe mwanamke mwenye ndoa ambaye hajawah
kutoka nje ya ndoa tangu
alipoolewa ndo kijana wetu
atapona!
Kama ametoka nje ya ndoa
asiandae dawa hii kwa sababu tukimpa kjana
wetu watakufa wote!
Je kina mama nani
ataandaa? Walitoka nje
wamama mmoja mmoja hadi
mkewe na mamake mzazi wakatoka, akafata
mama ake kijana,
mashangazi na dada zake,
mwisho wakabakia
wanaume peke yao! Mzee
akamwambia mwanangu umeona hali za
ndoa zilivyo?
Acha kujisumbua tulia na
mkeo nadhani
umejionea hali halisi.
Cha zaidi omba Mungu sana juu ya ndoa yako!
Kijana akazimia!
 

Zoë

JF-Expert Member
May 20, 2019
19,440
2,000
Mimi naomba wanaume waendelee kuamini hivyo hivyo kwamba wanawake hawachepuki raha sana mtu anapojipa moyo kwamba yeye ni chui japokuwa kiuhalisia yeye ni paka tu
 

Tieli

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
374
1,000
Haahaa kijana kazingua sana si alitaka kuujua ukweli akazimia ili iweje sasa
 

moj6

JF-Expert Member
Nov 2, 2017
2,666
2,000
Ndio ukweli wa mambo,what I need from my wife is just respect #
 

GEMBESON

JF-Expert Member
Apr 15, 2012
579
1,000
Hayo ni mambo ya mtandaoni yanayofanana na ukweli halisi. Cha kujifunza apo ni ili Ndoa idumu inatulazimu tusamehe mambo makubwa na yanayotumiza, vinginevyo hakuna mkamilifu.
 

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
21,287
2,000
Hayo ni mambo ya mtandaoni yanayofanana na ukweli halisi. Cha kujifunza apo ni ili Ndoa idumu inatulazimu tusamehe mambo makubwa na yanayotumiza, vinginevyo hakuna mkamilifu.
Kikubwa ni kuacha uchunguzi wa mambo ambayo ukiyakuta huwezi yoa maamuzi zaidi ya kumwachia Mungu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom