Hekima Tatu Bora!

Etugrul Bey

JF-Expert Member
Aug 6, 2020
3,524
6,507
Kuna mwanafunzi mmoja alienda Kwa watu WA elimu na kujifunza mambo matatu makubwa.

1) Usimfanyie Ubaya mtu aliyekufanyia wema
2) Ukipita sehemu ukaiona kheri usiiache
3) Usihukumu kitu ambacho hauna uhakika nacho

Alipewa Ngamia watatu na wazazi wake kama gharama ya kusomea hayo mambo matatu, baada ya masomo hakuwa na nauli ya kurudi kwao,hivyo ikabidi atafute mtu ambaye amtasaidia nauli.

Akamkuta bwana mmoja ambaye akamwambia Mimi nitakupa nauli lkn Kwa sharti kwamba utakaa kwangu Kwa Mda fulani ukinisaidia kazi halafu nitakupa nauli,bwana mdogo hakuwa na namna zaidi ya kukubali sharti hilo.

Basi kwakuwa kijana ana elimu,mke WA boss akamwambia naomba utufindishie watoto wetu pia,basi kijana hakuwa na hiana akafanya hivyo. Mwisho wa siku mke wa boss akamtamani Yule kijana,mfano wa Yale yaliyo mtoea Nabii Yusuph Kwa Zuleikha Kule misri.

Kijana akakumbuka kuwa somo la Kwanza kusoma lilikuwa ni "Usimfanyie Ubaya mtu aliyekufanyia wema" Akaona hapana boss wangu amekuwa mwema kwangu na kutaka kunisaidia iweje nitembee na mkewe? Akakataa lo salale! Hakika vitimbi vya wanawake ni vikubwa. Mke akamwambia mumewe huyu kijana ni mjeuri Hana adabu na bla bla nyingine kibao,na akatoa ushauri Kwa mumewe kuwa anafaa akatwe kichwa/auwawe,daah mume kaingia king Kwa ushauri WA mkewe.

Basi wakapanga kesho apeleke chakula shambani kwao,Kule kuna watumwa wanafanya kazi,akifika huko atakatwa kichwa na watumwa,na kumbuka watumwa wameambiwa mtu atakaye leta chakula ndo huyo huyo. Basi bwana hakika Mwenyezi Mungu ni bingwa wa kupindua hila za watu.

Jamaa kachukua chakula anaenda zake shambani,basi njiani akakuta watu Wana mtaja Allah Kwa kufanya dhikri mbali mbali na wengine wanasoma Qur'an,akakumbuka somo la pili "Ukipita sehemu ukaiona kheri usiiache" basi Akaona hapa watu wanamkumbuka Mwenyezi Mungu na wanasoma Kitabu chake hakika hii ni kheri na siwezi kuiacha. Basi akakaa kitako na kushiriki Jambo lile.

Huku Kwa watumwa chakula hakijaenda,ndo ikabidi atoke mtoto wa Yule Mzee akacheki imekuwaje tena mbona jamaa alitoka Mda mrefu,akiwa njiani ndo akamkuta jamaa kwenye kikao cha kheri,akamsema pale na kuchukua kile chakula Kwa ahadi kuwa ataenda kumwambia Mzee wake kilicho tokea. Basi bwana kafika Kule,na watumwa waliambiwa atakaye leta chakula ndio halali yenu.

Watumwa wakamuua Yule kijana pasina kujua ni kijana wa boss wao,boss baadae anapewa taarifa kwamba huku kazi tayar, laa haula boss anafika anakuta kumbe mwanae,daah tui limezidi maji ikabidi pale vilio vitawale,mpaka watu WA mashamba ya jirani kuja pale ndio ikajulikana hiyo Siri.

Baada Yule kijana kamaliza kikao cha watu wema akasema ngoja niende shambani sasa,anakuta makelele mengi,kuuliza akaambiwa mtoto w boss kauwawa Kwa bahati mbaya,aliyekusudiwa hakuleta yeye chakula,jamaa akajua dah kumbe ilikuwa Mimi,Akaona isiwe tabu inabidi aondoke sehemu Ile chap maana sio salama kwake.

Akafika nyumbani kwake akamkuta mkewe nje anaosha vyombo ,basi baada ya salamu akaingia ndani fasta,akamkuta mwanaume kitandani kwake amelala akataka kufanya uamuzi WA kuchukua mkuki na kumchoma,akakumbuka somo la Tatu " Usihukumu kitu ambacho hauna uhakika nacho".

Anatoka nje na kumuuliza mkewe yule ni Nani,ndo akaambiwa huyo ni Baba yako amekuja hapa anaumwa Sana,hivyo amejipumzisha kidogo. Je kama angekurupuka kama wale watu ambao wanacomment Bila kusoma Uzi wote unafikiri ingekuwaje?.

Ni hayo Tu!
 
4) Usipende weka mategemeo makubwa sana katika kila jambo ufanyalo/utegemealo (80 vs 20 / 70 vs 30 etc)
 
GenuineMan labda nikusaidie zaidi

Ungeambiwa usome hii story halafu utaje mafunzo uliyoyapata je utasema Baba Kalala kwenye kitanda cha mtoto wake na mkewe?
 
Akafika nyumbani kwake akakuta mkewe anaosha vyombo".

Mkewe yupi tena mkuu, ilihali anaishi kwa watu na hajapata nauli ya kumrudisha nyumbani????
 
Akafika nyumbani kwake akakuta mkewe anaosha vyombo".

Mkewe yupi tena mkuu, ilihali anaishi kwa watu na hajapata nauli ya kumrudisha nyumbani????
Mkuu umesoma kuelewa au umesoma kumaliza?

Kama umesoma kuelewa mbona sioni la kuuliza hapo?

Baada ya kufika shambani na kukuta msiba Safar ya kwenda home ikaanzia hapo
 
Back
Top Bottom