Toka kwa Wananchi: Kero na vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa

Taja moja tu moja Kwa moja Bila kuzunguka tuone tatizo liko wapi? Taja moja ambalo Kwa mujibu wa katiba lipo ndani ya uwezo wa rais na halihitaji nguvu nyingi zaidi ya maamuzi tu Bila kujali siasa. Jambo lenyewe liwe linagusa kweli kweli Maslahi ya wanyonge liwe linasaidia mamilioni ya watu na unahisi bado halijafanyika na tatizo liko ndani ya mamlaka hio kuu. Moja tu likifanyika utapata Imani kuwa rais magufuli anamaanisha na labda pengine ni changamoto fulani zinatatiza. Moja tu
Aachie uhuru wa bunge
 
Hili naliongea kwa kuwa na mkubali na kumpenda mh Rais. Suala la mkuu wa mkoa wa dsm lina madhara makubwa katika kuaminiwa kwake na jamii ya anao waongoza.

Mh ajifunze kwa watangulizi wake, awamu ya kwanza walifikia hata kutunga wimbo ule wa kuhamasisha jamii iwe na imani na viongozi wao. Wimbo huu maarufu, tuna imani na... yana tajwa majina ya viongozi mbalimbali. Walifanya hivi kwa kuwa walijua ni mzigo mzito kuwaongoza watu kama hawana imani na wewe. Itakuwa ni ajabu sana kitu kinachondoa imani ya wanaongozwa kwa anayewaongoza eti kipuuziwe tu hivihivi.


Ajue tu huku katika jamii kuna ndugu, marafiki na hata watu walio itarakti na huyu mheshimiwa katika maisha ya kila siku na wanamjua vizuri nje ndani.

Hivi nimetoka nje ya maada eeeh!


Na washawasha!
 
Aagize wizara ya kilimo ijenge miundo mbinu mipya mikubwa ya kilimo cha umwagiliaji angalau kila mkoa iwepo iyo project moja ili maisha yakitushinda mjini tuende tukalime bila kutegemea mvua
 
Hilo linasaidia vipi mamilioni ya watu waliopo vijijini Kwa mfano. Na je una uhakika Hilo tu kitakufanya uamini kweli magufuli ni rais wa wanyonge.. Jukumu Hilo umeliona ni gumu Sana na ni muhimu Sana kutekelezwa??? Upo serious

Hizo double standard ni yeye anafanya au vyombo husika.. Kama ni yeye anamuoenea mtu Sasa wewe unakuwa unajuaje kama ni kweli kaonewa au katenda kosa kweli.. Kati yako na rais Nani anauwezo wa kupata taarifa nyingi achilia mbali usahihi wa hizo taarifa... Na kama ni yeye anafanya double standard kutokana na KAULI zake je akiamua kuwa km bubu akawa anafanya kazi na haonekani public mara Kwa mara..je utaridhika?
Mbona unamjibia, au una majibu yako mfukoni? Kuna jamaa kasema au ndo yeye mwenyewe! Nami napata mashaka!
 
Hilo linasaidia vipi mamilioni ya watu waliopo vijijini Kwa mfano. Na je una uhakika Hilo tu kitakufanya uamini kweli magufuli ni rais wa wanyonge.. Jukumu Hilo umeliona ni gumu Sana na ni muhimu Sana kutekelezwa??? Upo serious
Wananchi wa vijijini wanalipa kodi ambayo ndio anatumia mtu aliyefoji cheti,sasa ili kuwasaidia ni bora amtumbue tu kuliko kodi yao kutumika kumlipa mtu aliyetenda jinai
 
Taja moja tu moja Kwa moja Bila kuzunguka tuone tatizo liko wapi? Taja moja ambalo Kwa mujibu wa katiba lipo ndani ya uwezo wa rais na halihitaji nguvu nyingi zaidi ya maamuzi tu Bila kujali siasa. Jambo lenyewe liwe linagusa kweli kweli Maslahi ya wanyonge liwe linasaidia mamilioni ya watu na unahisi bado halijafanyika na tatizo liko ndani ya mamlaka hio kuu. Moja tu likifanyika utapata Imani kuwa rais magufuli anamaanisha na labda pengine ni changamoto fulani zinatatiza. Moja tu
Alipe madeni ya ndani bila upendeleo na Afuate bajeti iliyo pitishwa na bunge
 
1.hataki mijadala.. Mijadala ipi mbona TAASISI nyingi tu zinaendelea na vikao kuhusu masuala yao ya kiutendaji. Mijadala Gani unataka
2.kaiba CHETI, ukiambiwa ulete ushahid unasema Gwajima KASEMA kwanini rais a deal na mambo ya mitandaoni tena mepesi kama haya. Hivi kweli upo serious una amini kaiba CHETI.
3.kuvunjia watu nyumba Unaamini anafanya yeye kabla ya mamlaka husika kufanya uchunguzi na kugundua madhara yatakayokuja.. Embu assume we ni rais na una roho mbaya je kuvunja nyumba za watu unapata faida Gani. Rais ananufaika vipi hapo.. Jamani amkeni ndugu ZANGU serikali ina vyombo vingi wakati mwingine kutimiza majukumu Yake unamuona rais anamkosea mmiliki wa nyumba inayoweza kuingiza maji na kuua watu.
4.fedha zimetumika kufanya jambo Zuri la kuchangia madawati bado tu na Hilo huhitaji kuskia ndugu
5.hivi magufuli kuwaelekeza mahakama kwamba washughulikie kesi haraka nako amekosea? Ila ikumbukwe yeye ni mkuu wa nchi anasimama juu ya mihimili mingine Ila kizuri Anatoa maelekezo ambayo kikatiba yuko sawa
6.ni kosa rais kutoa mwelekeo wa serikali Yake Kanisani.. Na wakati kanisa linakuwa linajua kuwa kutakuwa na ugeni wa mkuu wa nchi. Kosa hapo silioni
7.kumpandisha mtu cheo Utaratib wa nini wakati katiba Inasema kabisa yeye ndio amiri jeshi mkuu.. Mamlaka hiyo yapo chini Yake..
8.hataki kusoma hotuba. Kavunja sheria Kivipi na hayo unaposema madudu HAUPO sawa. Rais ni amiri jeshi HUTAKI aongoze watu Sasa nini maana ya kuwa rais. Mwelekeo wa serikali Yake atautoaje Bila kuongeza maneno anayoyamini
Mimi nasema kwamba magufuli anafanya vizuri Sana Ukitulia na ukijua kuwa tuluchelewa kupiga hatua, hutampinga magufuli.. Pamoja na mapungufu aliyonayo madogo bado anatufaa Sana
We pungwani kumbe
 
Atakapo sema Msema kweli ni mpenzi wa mungu lazima ni wambie ukweli mkuu wa mkoa wa Dar es salaam anaitwa Daudi bashite hivyo ninamtumbua kama nilivyo mtumbua mkurugenzi wa jiji:):):)
 
Back
Top Bottom