Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Toka kwa Wananchi: Kero na Vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JamiiForums, Feb 13, 2016.

 1. JamiiForums

  JamiiForums Official Robot Staff Member

  #1
  Feb 13, 2016
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 4,765
  Likes Received: 1,202
  Trophy Points: 280
  Ndugu wana JamiiForums,

  Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.

  Karibuni sana.

  MWONGOZO:
  Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.

  Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.
   
 2. Daraja Makofia

  Daraja Makofia Senior Member

  #421
  Dec 18, 2016
  Joined: Mar 30, 2015
  Messages: 146
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  BIMA YA AFYA NI JIPU LA KULIANGAZIA

  Wanabodi, hongereni kwa constructive criticism.

  Leo nimeona nije na hili suala la BIMA ya afya, to be specific, NHIF.

  Kwanza niwapongeze waliokuja na wazo hili, ni msaada mkubwa hasa kwa watumishi wa umma ambao majority hawana uhakika wa kujiwekea akiba kwa ajili ya matibabu.

  Lakini kwa upande mwingine BIMA hii imekuwa kama ni upigaji wa mishahara ya watumishi wa umma kutoka kwenye makato ya mishahara yao baada ya kukatwa kwa lazima kama sheria inavyoelekeza.

  Nasema ni upigaji kwa sababu makato hayaendani na huduma zitolewazo pindi wanapozihitaji.

  Katika kuhusisha suala hili, HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA DODOMA nitaichukulia kama CASE STUDY.

  Juzi nilikuwa na uhitaji wa huduma ya afya kwa kutumia mpango wa BIMA ya afya ya NHIF. Nilifika mapokezi na kuandikisha kama kawaida. Nilipoingia ndani ili nihudumiwe, kero zifuatazo zilinikuta:-
  1/ Upungufu wa wahudumu:
  Matabibu ni wachache na waliopo wanaanza asubuhi mpaka jioni bila ya kuwepo kwa wengine waingie kwa shift. Hivyo kwa mtazamo wangu huwa wanachoka kwa masaa mengi ya kazi.

  Pia mtu wa maabara alikuwa mmoja kwa siku hiyo kuhudumia msululu wa watu kwa siku nzima.

  2/ Majibu na kauli mbaya kwa wateja:-
  Ilipofika saa 11 alibaki Tabibu mmoja wa mlango wa Wazee ambaye alikuwa akitoa kauli chafu kwa wateja pale walipohoji uharaka wa huduma. Hii ikizingatia kuwa kuna kinamama, watoto, wazee na wajawazito waliokuwa hapo tangu asubuhi na hawapata huduma kwa wakati.

  3/ Upungufu wa vifaa tiba:-
  Kuna baadhi ya vipimo havipatikani kwenye jengo hilo mpaka uambiwe ukafuate upande wa HOSPITALI ya MKOA.
  Pia baadhi ya dawa hazipatikani kwenye dirisha la dawa mpaka uende Pharmacy za nje.

  HITIMISHO:-
  Naomba kero za hapo juu zifanyiwe kazi ili huduma ziendane na makato ya lazima kwenye mishahara ya watumishi wa umma.

  N.B:-
  MALAIKA MZIMA JF USIIGUSE TENA HII KITU, NI YA MUHIMU KWETU.
   
 3. JembeNaNyundo

  JembeNaNyundo Member

  #422
  Dec 18, 2016
  Joined: Dec 9, 2016
  Messages: 78
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 25
  Pole sana mkuu. Nadhani hayo mapungufu yanawahusu wamiliki wa hiyo hospitali na sio NHIF. Hupati hizo shida kwa sababu una kadi ya NHIF. Na hata kama usingekuwa na kadi ya NHIF bado ungepata shida hizo hizo.
   
 4. L

  Landson Tz Member

  #423
  Dec 28, 2016
  Joined: May 8, 2011
  Messages: 78
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 15
  Ni Leo Asubuhi siku ya Jumatano siku ya tao ya mwisho wa mwaka 2016, yaani zimebakia siku 4 tu kumaliza mwa 2016 na kuanza mwaka mpya wa 2017.
  Namuomba Mh. Rais JPM, aangazie macho yake kwa afya za wananchi, huduma za afya nchini hazirizishi hasa kwa maskini. Tumekuwa tukilalamika bila kuja na mbadala wa matatizo, lakini leo nakuja na mbadala. Watanzania wengi wenye ajira wanachangia BIMA ya AFYA kwa ajili ya jamii ya watanzania kwa ujumla. Ila kwakujua au kutojua fedha nyingi za Mfuko zimeelekezwa kwenye hospitali binafsi na mafamasi binafsi huku vituo vya serikali vikilia ukata, hakuna dawa vitendanishi wala vifaa vingine.

  Mheshimiwa rais, fanya maamuzi fedha zote za BIMA ya Afya zielekezwe kwenye vituo na hospitali za umma utakuwa umesaidia wananchi na huduma zitakuwa bora zaidi kuliko sasa. Hospitali za umma zina wataalam wakutosha, ila huduma zinakwamishwa na kutokuwepo fedha za kutsha, mheshimiwa rais fedha BIMA zipo nyingi muulize Mama Makinda.
   
 5. N

  Ngoso JF-Expert Member

  #424
  Jan 9, 2017
  Joined: May 26, 2012
  Messages: 489
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Mahakama ya mafisadi imeanzishwa na waziri wa sheria na katiba amesema bila kumun'gunya maneno mahakama imekosa kesi za kusikiliza kwa kuwa waliokuwa mafisadi wameogopa na kuacha kwa maana hiyo kulingana na kauli ya serikali kupitia waziri wa sheria na katiba Tanzania sasa hakuna mafisadi.nasema kweli mtupu na msema kweli ni mpenzi wa Mungu
   
 6. R

  Rweye JF-Expert Member

  #425
  Jan 9, 2017
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 13,052
  Likes Received: 1,586
  Trophy Points: 280
  Hii mandhari mnaiongea iko wapi make sioni hata picha yoyote hapa
   
Loading...