Toka kwa Wananchi: Kero na Vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa... | Page 21 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Toka kwa Wananchi: Kero na Vitendo vya kifisadi vinavyoendelea nchini vinavyotakiwa kufuatiliwa...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JamiiForums, Feb 13, 2016.

 1. JamiiForums

  JamiiForums Official Robot Staff Member

  #1
  Feb 13, 2016
  Joined: Nov 9, 2006
  Messages: 5,095
  Likes Received: 2,240
  Trophy Points: 280
  Ndugu wana JamiiForums,

  Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.

  Karibuni sana.

  MWONGOZO: Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.

  Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.
   
 2. No Escape

  No Escape JF-Expert Member

  #401
  Nov 27, 2016
  Joined: Mar 7, 2016
  Messages: 4,330
  Likes Received: 3,732
  Trophy Points: 280
  Ikibainika ni fisadi kweli,hakuna kuona huruma aisee! Wametuvuna sana...
   
 3. Kagondo

  Kagondo JF-Expert Member

  #402
  Nov 29, 2016
  Joined: Jun 6, 2016
  Messages: 291
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 45
  4g haipo
   
 4. D

  Daisam JF-Expert Member

  #403
  Nov 29, 2016
  Joined: May 23, 2016
  Messages: 1,259
  Likes Received: 657
  Trophy Points: 280
  Bwana na akainyooshe fimbo ya nguvu zake kutoka mbinguni ili Rais Magufuli awe na enzi kati ya maadui zake wote. Amina
   
 5. cheeter

  cheeter JF-Expert Member

  #404
  Dec 2, 2016
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 448
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Mfalme Sulemani alimwomba mwenyezi mungu ampatie hekima katika utawala wake. Wapo wanaokushangilia kwa kazi iliyombele yako,"Kutumbua unaowaiita Majipu" bila sheria kufatwa.

  Kuna msemo wetu unasema, Kufa-Kufaana.Ila, hakuna jambo lisilo na mwisho.Tumeona baadhi ya viongozi uliowachagua wanadiriki kuongea maneno yasio ya busara kabisa,mpaka kudiriki kuwaambia watu watajuta kuzaliwa kwao!.

  Hivi Majuzi tumekusikia, unazungumzia Suala la Fixed Deposit Account( FDA), na kutaja TRA na taasisi nyingi za serikali ikiwemo TEA kuwa wameweka hela kwenye FDA ili wapate interest huku shule hazina vyoo,madarasa n.k.

  Ukaenda mbali zaidi ukasema, ma chief executive wengi wanakubaliana na hawa wenye mabenki.Waziri upo hapa unanisikia,message sent and delivered.
  Kesho yake, tukasikia Governor wa benki kuu(BOT),mchumi aliobobea akielezea Taasisi kuweka hela kwenye FDA si kosa.

  Juzi tu hapa, tumemsikia tena Msajili wa hazina, kama kumkosoa raisi tena. kuweka hela kwenye FDA si kosa na taasisi za serikali nyingi zilikua zinaweka hela kwenye FDA miaka ya nyuma.

  Kosa ni hizo interest kutumika tofauti.Na akasema ni ngumu kuiba hizo hela maana mwisho wa siku kuna ukaguzi huwafanywa.

  Leo, nimesoma gazeti la mtanzania. Nimeona utumbuaji wa kimya kimya Mamlaka ya Elimu,naibu waziri wa elimu alipoulizwa kuhusina na hizo taarifa akasema hajui na hana hizo taarifa . Where are we headed? wa Tanzania wapi tulikosea?

  Mwisho kabisa, Nakutakia maisha mema mh.raisi.
   
 6. J

  JICHO TAI JF-Expert Member

  #405
  Dec 2, 2016
  Joined: May 27, 2013
  Messages: 1,115
  Likes Received: 316
  Trophy Points: 180
  mkuu mbona nimesoma bandiko lako sijaona unamshauri Mh. Rais? au bado unaendelea kuandika?
   
 7. n

  nyembeason Member

  #406
  Dec 8, 2016
  Joined: May 4, 2009
  Messages: 44
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 15
  Mkoa wa Morogoro ni miongoni mwa mikoa yenye mito isiyopungua 100 isiyokauka kipindi chote cha mwaka. Lakini cha ajabu mji wa Morogoro, chini ya MORUWASA, unakabiliwa na uhaba mkubwa sana wa maji. Kuna mitaa mingi sana, mathalani Bigwa, hukaa kwa muda wa miezi mpaka mitatu bila maji. MORUWASA, bila aibu, kila mwisho wa mwezi hupita na kusoma mita na kuwaletea bili za maji wenye mita .Miitaa kama Kihonda maji kwao ni almasi-hununua kwenye magari ya wauza maji, na uhaba huu wa maji yaelekea hauna jawabu. Ndoo MOJA ya maji, ya lita 20, huuzwa shilingi mia tano za kitanzania.

  Huwezi kuwa nchi ya viwanda ikiwa maji yasiyohiyaji akili HAYAPATIKANI-just laying pipes na kusambaza kwa umma/watu!

  Nionavyo mimi Shida kubwa kwa taasisi nyingi za umma, ikiwemo MORUWASA, ni: Kuwa na watumishi wengi wasio na uwezo,mizigo, wapiga dili na wanaofanya kazi kwa mazoea na pengine wenye maslahi na uhaba wa huduma za umma (mathalani wana magari ya kuuza maji, wana visima, au huduma ambazo zikiwemo kwenye idara za umma wanakosa dili). HAKUNA UBUNIFU, SOGA TU OFISINI NA kufanya kazi kwa mazoea-BUSINESS AS USUAL, ili mradi mwisho wa mwezi ufike waende kwenye ATM-kula kodi zetu.

  Mkuu wa Mkoa wa Dsm, Paulo Makonda aliwahi kusema kuwa SERIKALI ina wafanyakazi wengi sana wasio na KAZI, MIZIGO. Nafikiri ni wakati muafaka kwa serikali kupitisha fagio la chuma, kubakisha watumishi wenye ueledi, tija na wabunifu, WENYE KUFANYA KAZI, SI KUPOKEA SALARI TU. Kuna mizigo mingi sana kwenye UTUMISHI wa umma. Magu pitia huku-watumishi waliopo, ambao si hewa, lakini hawana tija, mizigo, WAPOKEA SALARI TU BILA KUREJESHA HUDUMA ZENYE TIJA, WELEDI NA KWA WAKATI kwa jamii inayowalipa.
  http://moruwasa.go.tz/home/index.php?option=com_content&task=view&id=47&Itemid=64
   
 8. evonik

  evonik JF-Expert Member

  #407
  Dec 8, 2016
  Joined: Jun 12, 2015
  Messages: 1,306
  Likes Received: 651
  Trophy Points: 280
  Polen Mkuu, vp na kwa Wakubwa kwao maji Hamna mfano RC kambi za jeshi n.k lakin mkuu hako nako kafursa cha kutokea, hata kama una corolla gx Unapiga nako kazi Ndo 1=500? hataliii
   
 9. m

  mezakuu Senior Member

  #408
  Dec 8, 2016
  Joined: Apr 19, 2016
  Messages: 126
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 60
  Mbona mi nakaa kihonda bima hapa hamna shida ya maji
   
 10. mtimkav

  mtimkav JF-Expert Member

  #409
  Dec 8, 2016
  Joined: Aug 28, 2013
  Messages: 954
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 80
  shukuru mungu waulize wenzio huko mazimbu road na lukobe wakupe habari kamili
   
 11. mtimkav

  mtimkav JF-Expert Member

  #410
  Dec 8, 2016
  Joined: Aug 28, 2013
  Messages: 954
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 80
  mkuu hii biashara nilipiga sana na ka gari ka dingi kakaja kufa ila hela nje nje yani kama mtu unakirikuu ndo umeulaa

  kufa kufaana huku
   
 12. M

  Maelau JF-Expert Member

  #411
  Dec 8, 2016
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 817
  Likes Received: 731
  Trophy Points: 180
  Inaongelewa kihonda kwa chambo ndugu. Fika kule uone. Infact ni kama hawa jamaa wanafanya makusudi kutengeneza uhaba ili wafaidike kupitia malori ya kuuza maji ambayo nadhani wanakuwa na maslahi nayo. Watu wa kihonda wakikomaa kidogo, huzugwa kwa kuletewa maji kama mara mbili hivi kisha hujisahaulisha kabisa. Kibaya zaidi kila mwisho wa mwezi wananchi hupelekewa bili za maji. Ni shida.
   
 13. mbwea

  mbwea JF-Expert Member

  #412
  Dec 8, 2016
  Joined: Aug 15, 2012
  Messages: 222
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 60
  Nenda ofisini kawambie acha uwoga wakijibu ovyo panda kazi za juu. Maji ni uhai
   
 14. lazalaza

  lazalaza JF-Expert Member

  #413
  Dec 8, 2016
  Joined: Dec 15, 2012
  Messages: 2,057
  Likes Received: 1,356
  Trophy Points: 280
  Mindu na kibwe ni vyanzo vya zamani, wajitahidi kule juu kutunza mazingira ili iwe Moro yamaji yatiririka.
   
 15. krava

  krava JF-Expert Member

  #414
  Dec 8, 2016
  Joined: Nov 17, 2016
  Messages: 226
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 60
  Hata kilakala hakuna maji wanafunzi wa kilakala sec kunakipindi walikuwa wanatoka nje ya uzio kwenda kuchota maji shule ya kiislamu ya darul arqam mimbamimba sidhani kama walikosa
   
 16. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #415
  Dec 9, 2016
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 5,552
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280
  huo ni urasimu na ukiritimba....
   
 17. r

  rongai JF-Expert Member

  #416
  Dec 9, 2016
  Joined: Jan 27, 2014
  Messages: 455
  Likes Received: 272
  Trophy Points: 80
  Maji moro ni shida ila hata vyanzo vya maji vimepungua kwa uharibifu wa mazingira na ongezeko la idadi ya watu.miti mingi haina maji kwa sasa km huko bigwa ni mikavu kabisa. Uongozi ni kubuni njia za kutunza mazingira na kurejesha uoto wa asili wa milima ya uluguru ila mvua sinyeshe na maji yawe mengi huko milimani. Na ni kweli kuna maeneo maji yapo kila siku huko kwani hao wanaouza wanayatoa wapi?
   
 18. D

  Daisam JF-Expert Member

  #417
  Dec 11, 2016
  Joined: May 23, 2016
  Messages: 1,259
  Likes Received: 657
  Trophy Points: 280
  Kwa hakika mheshimiwa Rais Magufuli anafanya vizuri sana. Tanzania ilipokuwa imefika, ilikuwa inahitaji kuwa na Rais kama Magufuli. Historia inaonesha kwamba, MUNGU HUMLETA MTU FULANI KATIKA ENEO HUSIKA KWA WAKATI NA MALENGO MAALUMU.
   
 19. D

  Daisam JF-Expert Member

  #418
  Dec 11, 2016
  Joined: May 23, 2016
  Messages: 1,259
  Likes Received: 657
  Trophy Points: 280
  Naomba Rais Magufuli atoe tamko (amri ) ya kuingiza UMEME katika shule zote zilizopitiwa na line ya umeme. Ninathubutu kusema hivi kwa sababu utakuta nguzo za umeme zimepita uwanjani mwa shule lakini shule hiyo inakaa bila umeme kwa muda wa miaka mingi kana kwamba umeme hauna manufaa kabisa katika shule. Mfano mzuri wa shule ambazo zipo katikati ya mji lakini hazina umeme ni pamoja na SHULE ZA HALMASHAURI YA MJI WA MAKAMBAKO KATIKA MKOA WA NJOMBE. Pamoja na matumizi mengine ya umeme, umeme katika shule hizo ungeweza kutumika kwa ajili ya kuchapa mitihani nk. Kwa kuwa suala la MADAWATI limefanikiwa kwa asilimia nyingi, ninaamini hata hili likitiliwa mkazo linawezekana tena haraka sana. MUNGU MBARIKI RAIS JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI, SERIKALI YAKE NA WATANZANIA WOTE. Amina.
   
 20. Triple A

  Triple A JF-Expert Member

  #419
  Dec 13, 2016
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 750
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  kero yangu kubwa ni kuona kuwa wakuu wa wilaya wanakimbizana na wavuvi haramu wakati sisi wenye leseni ya uchimbaji madini tumepeleka taarifa kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya kuwa kuna wachimbaji haramu,wala hata hawashughulikiwi
   
 21. k

  kemi2011 JF-Expert Member

  #420
  Dec 14, 2016
  Joined: Dec 25, 2013
  Messages: 704
  Likes Received: 243
  Trophy Points: 60
  Mimi kero yangu natamani kujua Lugumi ni Nani na kwa nini hili suala halishugulikiwi
   
Loading...