huko kwenu vipi
JF-Expert Member
- Jun 4, 2015
- 1,519
- 1,462
Yeah nahisi sahv rate itakuwa kubwa!Hiyo namba mbili wanafanya kitambo indirect sema labda wafanye direct
Yeah nahisi sahv rate itakuwa kubwa!Hiyo namba mbili wanafanya kitambo indirect sema labda wafanye direct
Mfumo wa uchumi ulikua free sana mpaka pesa yetu ikashuka thamani.Chamaana anatakiwa apandishe mishahara kwa watumishi wa chini ili ireflect kwenye maendeleo ya mtu wa chini.Elimu bure si sahihi sana maana uendeshaji wa shule umekua mgumu sana.Arudishe michango ya mitihani na taaluma,mambo yataenda vizuri tu.
Nyumba za serikali zilizouzwa nchi nzima kila mtu shahidi,Lugumi mkataba wake umeisha vipi.Ndugu wana JamiiForums,
Nchi yetu imetafunwa mno na ni wakati sasa tuseme imetosha. Tumsaidie Rais Magufuli na Serikali yake kuweza kuzifahamu kero zetu za yanayotusumbua kama watanzania ambayo tungependa yafanyiwe kazi.
Karibuni sana.
MWONGOZO:
Elezea jipu/kero yako na kama ina ufafanuzi wa kutosha (nani, wapi, lini, kivipi n.k) ukiambatana na nyaraka itapendeza zaidi.
Kero hizi zitachapwa na kupelekwa kwa mamlaka husika ili zifanyiwe ufuatiliaji.
C wamerudishwa form3 wakakuze taaluma zaoWizara ya elimu hebu fuatilieni haraka kinachoendelea shule ya sekondari ya kata ya Matosa iliyoko manispaa ya Kinondoni jijini Dar es salaam wakati huu wa mitihani ya form iv.
Kuna wanafunzi takriban 17 ambao wamezuiwa na academic master wa shule hiyo kufanya mitihani yote ya form iv kwa sababu zisizokubalika kisheria.
Sababu alizotoa ni kwamba wanafunzi hao hawajiwezi kitaaluma na hivyo hataki wafanye mtihani wa form iv.
Sijawahi kusikia kitu kama hiki,labda wana jf wenzangu mnisaidie.
Vijana hao wamesoma pale kuanzia form one,form two mtihani wa taifa walifanya na kupita,wamesoma hadi form four na mock walifanya,cha ajabu jtatu siku ya kuanza mitihani wakati wa kupangwa na kupewa namba mwalimu huyo aliwaita na kuwaeleza kuwa wao hawataruhusiwa kufanya mitihani kwa sababu nilizokwishaeleza hapo juu.
Kwa kawaida katika chumba cha mtihani wa taifa kama kuna mtahiniwa ambaye hayupo huwa namba yake inabandikwa kwenye dawati lake na kubaki wazi na wakaguzi wanapokutana na nafasi iliyo wazi ni lazima waite mwalimu mkuu kupata maelekezo.
Kwa hili la Matosa,madawati ya wanafunzi hao yameondolewa lakini katika karatasi zile za kusaini kila wakati wa kufanya mtihani fulani,wenzao huona majina ya wanafunzi hao na namba zao za mtihani zikiwa kwenye orodha ya watahiniwa.
Nimejaribu kuchunguza na kuuliza huku na kule kuona kama kuna mabadiliko yoyote katika taratibu za kufanya mitihani ya taifa siku hizi lakini sijaona,na hivyo kuhitimisha kuwa hili la Matosa ni la kipekee.
Kwingineko hata wale wanafunzi watoro wazazi wao waliandikiwa barua kuhimiza mtoto aende akafanye mtihani kwa vile ni haki yake na serikali imeingia gharama kuhakikisha kila mwanafunzi anaexercise haki yake hiyo,sasa hili la Matosa limeanzia wapi na lini na kwanini dk za mwisho kabisa tena kwa wanafunzi wenye mahudhurio darasani?
Kwanini hawakupewa namba zao za mtihani wafanye mitihani wakati namba hizo zinaonekana kwenye list toka wizarani?
Nakuwa suspicious hapo kwa kweli.
Naomba wizara itume wakaguzi kwenda Matosa kujiridhisha na kilichotokea kabla mitihani hii haijaisha.
Jf ifikisheni hii taarifa panapohusika haraka kama mlivyoahidi kwenye bandiko hapo juu.
Invisible