Toka bungeni leo: Muswada umepitishwa... Nini hatma yake?

Haiingii akilini wabunge wote mia mbili na ushee wa ccm na cuf wakawa na mawazo sawa . Huu ni uchakachuaju wa kutosha hauna mfano. hawa hawatungi katiba nafiri wanatengeneza Users Manual ya magamba.Katiba haijawahi kutungwa kwa staili hiyo popote duniani na hii ya kwetu itakuwa ni ya kwanza . Katiba hutungwa watu wote wakiwa mezani na wanaelewana.This is unacceptable constitutional bill.
 
Kuna mbunge wa zanzibar alikuwa anapigania maslahi ya zanzibar kwenye huu muungano bunge lililopita yuko wapi wakati huu?? au na yeye ni walewale wanafiki?
 
Katika mjengo wa Bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania hapa mjini Dodoma, Bunge la CCM linapitisha muswada wa wao wa kuanza mchakato wa uundaji wa Katiba mpya ukiwa na masharti magumu sana kwa wananchi amabao watakaihoji tume teule ya Raisi ya kukusanya maoni.

Moja ya sheria kali na ambayo ni kandamizi ambayo inamnyima uhuru Mtanzania ni ile isemayo kwamba "endapo mtu ataonekana kuisubua tume ya kukusanya maoni, kwa kuiuliza maswali au kudai ufafanizu zaidi, mtu huyo atachukuliwa hatua za kisheria". Mtuhumiwa huyo atahukumiwa kwa kosa la kuismbua tume na atatakiwa kulipa fidia kati Tsh 5,000,000 hadi Tsh 15,000,000 au kwenda jela miaka 3.

Kifungu kinawatishia watanzania haki yao ya kimsingi ya kuhoji uhalali wa utaratibu wa uundaji wa katiba hiyo na pia inawalazimisha watanzania kukubaliana na matakwa ya Serikali hasa kwa kutopingana na Hadidu rejea za Raisi.
 
Kwa jinsi mjadala huu ulivyoendeshwa inaonekana kabisa kuna shinikizo fulani kutoka chamani. Maana wabunge wote wanaonekana wana msimamo mmoja kitu ambacho ni nadra sana.
 
Kwa mtindo huu basi ugombea binafsi itakuwa ni ndoto...

Ndio maana tunataka katiba ya wananchi bila kuhodhiwa na kikwete. Kwa katiba huru toka kwa wananchi, mgombea binafsi ipo tu

mgombea binafsi tuipiganie kwani itaokoa pesa za umma kwa kutokuwepo ruzuku

Hili suala mara nyingi tunalichanganya sana. Kinachohitajika ni uwepo wa mgombea huru na si mgombea binafsi. Hakika hivi ni vitu viwili tofauti.

Kuna hitaji la kuwepo mgombea huru hasiefungamana na chama au taasisi yoyote. Wagombea binafsi mbona wapo?
 
kwa akili ya kiwete wazee wako dar na dodoma basi...si aende hata mbeya? .......hao kina selina wanamdanganya sana sasa ngoja ajichomeke aone? huu ndio wakati mwafaka wa kupinga aina ya uozo kama huu
 
Usiogope maana hilo ni bunge la CCM na sio la Tanganyika/Tanzania
 
Kwa jinsi mjadala huu ulivyoendeshwa inaonekana kabisa kuna shinikizo fulani kutoka chamani. Maana wabunge wote wanaonekana wana msimamo mmoja kitu ambacho ni nadra sana.

Kwa CCM si kitu nadra kwa wao kuna na msimamo mmoja! Jambo la ajabu, niliwasikia akina Mwigulu na Chenge wakisema kwamba haiwezekani kwa watu kuna na msimamo mmoja, la sivyo mambo yasingeenda kabisa duniani! Sasa hao hao wanaongea hivyo, halafu wanafanya hivyo.

Hakika kuwa mwanaCCM na haswa mbunge kupitia CCM kwa sasa ni sawa na kujitoa au kujivua UTU.
 
kuna member aliongea hili jana kama tetesi na akasema hiki kifungu kimeongezwa. duuh wanachotafuta CCM watakipata
 
Kwa kweli wabunge wa ccm wanafinywa sana uhuru wao wa kuongea. Nimemwona Mhe. Zambi leo wakati bunge likiwa kwenye Kamati akieleza kutoridhishwa kwake na kitendo cha kuteua wajumbe kwenye chombo cha muungano bila kujali uwiano wa idadi ya watu. Ameongea kwa woga sana na nadhani amejitahidi kujizuia kutoongea lakini ameshindwa. Kweli ukitaka uwe na uhuru wa kusema unachoamini ni bora usiwe nwanachama wa ccm.

Du! Hizi elimu zetu za kuunga unga... hiyo issue imeelezwa vizuri.... hapa tatizo Zanzibar ni nchi.... kwani kwenye baraza la umoja wa mataifa nchi kubwa zinakuwa na wajumbe wengi zaidi ya nchi ndogo? Tatizo ni katiba ya sasa huwezi kui-fumua ni mpaka utakapotunda nyingine.
 
Tatizo serikali inaogopa sana Zanzibar, sijui kwanini na wazanzibar wanalijua hili ndio maana wana kiburi sana.
 
moja ya kifungu cha huo mswaada ni hiki hapa chini...je watanzania mnahitaji hii kitu???? tuamke

Moja ya sheria kali na ambayo ni kandamizi ambayo inamnyima uhuru Mtanzania ni ile isemayo kwamba "endapo mtu ataonekana kuisubua tume ya kukusanya maoni, kwa kuiuliza maswali au kudai ufafanizu zaidi, mtu huyo atachukuliwa hatua za kisheria". Mtuhumiwa huyo atahukumiwa kwa kosa la kuismbua tume na atatakiwa kulipa fidia kati Tsh 5,000,000 hadi Tsh 15,000,000 au kwenda jela miaka 3.
 
Mswada ndiyo huo imepitishwa, vifijo na vigelele ndani ya Bunge, sasa utasomwa kwa mara ya tatu.
 
ndio maana naesma huu ndio ule mda kulipua umefika..huwezi kuwa na sheria za kijinga ama hizi
 
moja ya kifungu cha huo mswaada ni hiki hapa chini...je watanzania mnahitaji hii kitu???? tuamke

Moja ya sheria kali na ambayo ni kandamizi ambayo inamnyima uhuru Mtanzania ni ile isemayo kwamba "endapo mtu ataonekana kuisubua tume ya kukusanya maoni, kwa kuiuliza maswali au kudai ufafanizu zaidi, mtu huyo atachukuliwa hatua za kisheria". Mtuhumiwa huyo atahukumiwa kwa kosa la kuismbua tume na atatakiwa kulipa fidia kati Tsh 5,000,000 hadi Tsh 15,000,000 au kwenda jela miaka 3.

Ama kweli tumeichoka amani... mbona hakuna kifungu cha namna hiyo!!! Du!
 
Kuna mbunge wa zanzibar alikuwa anapigania maslahi ya zanzibar kwenye huu muungano bunge lililopita yuko wapi wakati huu?? au na yeye ni walewale wanafiki?

Alishabandikwa plasta mdomoni siku nyingi.
 
Katika mjengo wa Bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania hapa mjini Dodoma, Bunge la CCM linapitisha muswada wa wao wa kuanza mchakato wa uundaji wa Katiba mpya ukiwa na masharti magumu sana kwa wananchi amabao watakaihoji tume teule ya Raisi ya kukusanya maoni.

Moja ya sheria kali na ambayo ni kandamizi ambayo inamnyima uhuru Mtanzania ni ile isemayo kwamba "endapo mtu ataonekana kuisubua tume ya kukusanya maoni, kwa kuiuliza maswali au kudai ufafanizu zaidi, mtu huyo atachukuliwa hatua za kisheria". Mtuhumiwa huyo atahukumiwa kwa kosa la kuismbua tume na atatakiwa kulipa fidia kati Tsh 5,000,000 hadi Tsh 15,000,000 au kwenda jela miaka 3.

Kifungu kinawatishia watanzania haki yao ya kimsingi ya kuhoji uhalali wa utaratibu wa uundaji wa katiba hiyo na pia inawalazimisha watanzania kukubaliana na matakwa ya Serikali hasa kwa kutopingana na Hadidu rejea za Raisi.
Mkuu huu ni utani au?
 
Back
Top Bottom