Toka bungeni leo: Muswada umepitishwa... Nini hatma yake?

Kule zenji sijui mtatoa maoni gani ya muungano. Chondechonde msichane tena katiba yenu mpya mliyopitisha na magamba
 
Sio Siri, ni dhahiri CCM wamepora Katiba ya wananchi. CCM wamezoea kupora mali ya Umma, Nchi inalalamikiwa kwa ufisadi.

Jamani watanzania wenzangu, tutegemee katiba mpya ya CCM itatukomboa? Itatuondoa hapa tulipo?

Misingi ya katiba mpya ni kupata tume huru, kupunguza madaraka ya raisi, kupata mahakama huru, kulinda rasilimali za taifa, kuondoa ufisadi, na kutoa haki kwa wananchi.

Wananchi, Haki mmenyimwa na serikali ipi, ufisadi uko kwa serikali ipi, Chama kipi kinaiba kura???

Tunategemea kweli ccm itatenda haki kwa hii katiba>??

je wananchi tufanyeje???

Hapa nina wazo: Kwanza tuelimishane. Kila mtu anayeguswa aanze kuelimisha ndugu zake, marafiki zake na wafanyakazi wenza.

Kivipi: Tutumiane message - Text message. Mimi nimeanza kutuma kwa ndugu zangu, marafiki zangu, na wafanyakazi wenzangu wengi wao wanapinga huu muswada huu wa wa kiwizi.

" Salaams, nakusalimu kwa jina la tangannyika. Ukiwa kama Mtanzania, sidhani kama umefurahia muswada uliopitishwa na hawa Wabunge wa CCM!!!?? Kaa tayari kuupinga huu mchakato wa katiba ipya wa CCM. mafisadi wale wale, wezi wa kura wale wale ndo watuletee katiba mpya??? Chukua hatua, kaa tayari, usiogope"

Hiyo hapo juu ndo message ya kutuma kwa rafiki au ndugu yako.
 
Nchi imekwenda mrama! Nadhani sasa wamehalalisha wazee wa kazi kuingia mitaani kudai katiba!!
 
" Salaams, nakusalimu kwa jina la tangannyika. Ukiwa kama Mtanzania, sidhani kama umefurahia muswada uliopitishwa na hawa Wabunge wa CCM!!!?? Kaa tayari kuupinga huu mchakato wa katiba ipya wa CCM. mafisadi wale wale, wezi wa kura wale wale ndo watuletee katiba mpya??? Chukua hatua, kaa tayari, usiogope"
 
Si ajabu muswada kupitishwa kwanza.
Pili, kwa kuwa katika maamuzi wanayosema ni ya kidemokrasia ni uwingi wa kura kuliko uzito wa hoja walikuwa na haki zote.

MATOKEO YAKE NINI?

Kwanza kwa hali ilivyo wananchi wengi hawajafurahia namna ambavyo mjadala wa muswada ulivyokwenda kuanzia kwa wazee wa siku na waasisi wa taifa hili letu, TANZANIA, TANGANYIKA, ZANZIBAR mpaka vijana wa enzi za mzee mwinyi na mkapa ambao ndiyo wanaoshikilia mustakhabali wa taifa kwa maana ya next Tanzania is theirs.

Nchi sasa iko katika hali tete kwa kuwa mawazo ya wananchi wengine ambao kwa kuwa tu hawashabikii CCM na CUF wanapuuzwa na hili ni kukiuka ibara ya 8 ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania, inayosema kuwa mamlaka ya kutawala hutoka kwa wananchi na ibara ya 18 yahusuyo uhuru wa kujieleza.

Katika kipindi cha miaka 4 kutoka sasa nchi hii itakuwa si tena salama kama CCM-MAGAMBA-MAFISADI-WAKUJIKWEZA-DHARAU-U VITI MAALUM hautadhibitiwa vyema, tutaona nchi inayotawaliwa kwa mkono wa chuma, na umaskini ukiongezeka kwa kiwango cha kutisha.

KUPUUZIA MAWAZO YA WANANCHI WENGINE KWA KUWA TU MAWAZO YAO NI SAWA NA CHAMA FULANI, WANAHARAKATI NA WAPINZANI KUCHIMBA KABURI LA CCM NA UTULIVU WA TAIFA HILI
 
Hili suala mara nyingi tunalichanganya sana. Kinachohitajika ni uwepo wa mgombea huru na si mgombea binafsi. Hakika hivi ni vitu viwili tofauti.

Kuna hitaji la kuwepo mgombea huru hasiefungamana na chama au taasisi yoyote. Wagombea binafsi mbona wapo?

na sikuwepo mgombea huru tu, bali kuwepo na tume huru ya uchaguzi ambayo haitaegemea upande wowote.
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Mie nafikiri demokrasia hamuiujui-> demokrasia sio kujenga hoja zenye hoja, demokrasia ni kupiga kura wengi wanapata wachache wanakosa hiyo ndo kanuni ya demokrasia. Kiwe kibaya lakini wengi wamekipigia kura basi ndo hichohicho.

Kwani humo bugeni wachache ndo wameipitisha ama wengi? demokrasia ni quantity ndiyo qualifying perameter na sio quality. Sijui mnalalamika nini?
 
Nilitegemea! nawasikitikia cdm kushindwa kutoa mawazo na michango yao! pengine wangebadili baadhi ya mambo.
 
Well said.
Hiyo demokrasia ya wabunge wa CCM ya kuliibia taifa? Ila kwa sasa sisi wananchi ndio tunachukua nchi yetu kwa kutokuwa na imani na viongozi wote wa bunge na serikali, hiyo demokrasia yao ya kubaka, kandamizi nk ndio demokrasia? Jukumu ni letu sote sasa kudai nchi yetu

Imeungwa na wengi ama wachache humo bungeni? hiyo ndo demokrasia. Wewe unachoongelea ni mahakama mhimili wa haki za maisha. Sio demokrasia
 
Imeungwa na wengi ama wachache humo bungeni? hiyo ndo demokrasia. Wewe unachoongelea ni mahakama mhimili wa haki za maisha. Sio demokrasia

mkuu wewe ni MKAMA P katibu mkuu wa CCM? sitarajii uungane na wanaharakati kuupinga muswada mnaopitisha bungeni, hao wengi unaowataja bungeni walichaguliwa kihalali na wananchi wengi au mizengwe ndo imejaza hao wengi huko bungeni? naona unapotosha kabisa maana.
 
Nilitegemea! nawasikitikia cdm kushindwa kutoa mawazo na michango yao! pengine wangebadili baadhi ya mambo.

Wangeshiriki vipi katika kutoa mawazo kwenye jambo ambalo wao hawakukubali jambo hilo liwepo pale? Msimamo wao ulikua ni muswada huo usomwe mara ya kwanza ili upelekwe kwa wananchi kutoa mapendekezo yao; sasa wangeshiriki vipi hapo wakati muswada ulikua ukisomwa kwa mara ya pili?!?
 
Back
Top Bottom