Je, ni sahihi mamlaka za elimu kumbadilishia Mwanafunzi jina lake?

Aug 29, 2018
73
92
Salaam wakuu,

Nimepata shida kwa watoto wangu wawili kubadilishiwa majina.Wa kwanza alifanya mtihani wa darasa la nne mwaka 2020 na mwingine 2022.Nilipata kufahamu tatizo Hilo baada ya matokeo ya darasa la nne.Shule walizosomea majibu yao ni kuwa wao walisajili sawasawa kulingana na vyeti vya kuzaliwa.

Huyu Wa darasa la Saba ameambiwa jina ni hilo hilo atakalo fanyia mtihani wa darasa la Saba mwaka huu.Najiuliza swali mamlaka za elimu zinaweza kumbadilishia jina mwanafunzi?.Tena wananiambia labda nimbadilishie cheti Cha kuzaliwa kiendane na majina hayo mapya. Msaada ndugu zangu niko njia panda juu ya Nini naweza kufanya,

Maana mmoja kapewa jina la mtu mwingine na huyu Wa Darasa la tano sasa hivi ni herufi zimechanganywa hazileti maana kabisa.
 
Swali langu ni je mamlaka za elimu ni sahihi kumbadilishia mwanafunzi majina yake sahihi aliyopewa na wazazi wake?.Pili mzazi kutafuta cheti Cha kuzaliwa upya ni sawa ikiwa hujaridhika kumbadilishia mtoto majina?
 
Kwa mzazi mwenye akili timamu angeanzia kuuliza shuleni kwa mwl mkuu, majibu yakiwa ovyo anaenda kwa afisa elimu msingi wilaya au mkoa, suluhisho linapatikana.

Lakini haujakosea, ndio watz wengi walivyo, mtoto akimwambia kuna mchango shuleni, yeye atasubiri ziara ya waziri mkuu aulize kuhusu huo mchango.
 
Wanaosajili wanafunzi ni Walimu na sio mamlaka za elimu (BAMITA/NECTA). Makosa yamefanywa na walimu. Walimu wa shule za msingi kipindi Cha usajili wanaandika ndivyo sivyo. Mara nyingine huwapa karatasi watoto watoto wa darasa la nne waandike majina yao. Na hao watoto hawajui tahajia sahihi (spelling) za majina yao. Baadae wanafanyia hayo majina mitihani. Na akishafanya darsa la nne jina hilo halibadiliki mpaka chuo. Hivyo wazazi muwe makini na fuatilieni usajili wa watoto wenu mapema kabla ya kuharibiwa majina.
 
Hapa ninakuelewa,itakuwa ni uzembe.Mwalimu alinipigia simu nitume majina sahihi kwa sms nikafanya ivyo. Ila sikuridhika kesho yake nikapeleka na nakala ya cheti Cha kuzaliwa.Bado jina likakosewa.Walimu watuambie tuje kuhakiki majina maana wao ndiyo wenye kujua muda Wa usajili Wa wanafunzi kuliko kuingia kwenye haya tunayoyaona.Pia wasikwepe na kutaka kurushia wengine lawama zao.
 
Kwa mzazi mwenye akili timamu angeanzia kuuliza shuleni kwa mwl mkuu, majibu yakiwa ovyo anaenda kwa afisa elimu msingi wilaya au mkoa, suluhisho linapatikana.

Lakini haujakosea, ndio watz wengi walivyo, mtoto akimwambia kuna mchango shuleni, yeye atasubiri ziara ya waziri mkuu aulize kuhusu huo mchango.
Majibu ya kuwa jina haliwezi kubadilika sijaota ndivyo walivyonieleza.Pia kuwa labda nibadili cheti Cha kuzaliwa kiendane na jina hilo.Ila walikwepa kusema wao ndio hukosea majina.
 
kosa sio la walimu kosa ni mzazi kutokufatilia majina ya mwanafunzi kabl hata hajafanya mtihani wa darasa la nne ili kujihakikishia kama majina ni sahihi, unapomuandikisha mwanafunzi au unapotuma mtu kumuandikisha mwanafunzi darasa la kwanza hakikisha unafuatilia kwa mwalimu mkuu kama majina yapo sahihi maana inawezekana mwalimu alipokua ananakilo jina kutoka kweny cheti cha kuzaliwa akaliandika vibaya mfano hamadi kumbe jina hamad halina i mwisho wa siku inakubidi ubadili cheti cha kuzaliwa tu kiendane na majina ya shule

mwalimu au mamlaka za helimu haziwez kubadili jina la mwanafunzi kutoka lile aliloandikishwa kuja lingne makosa yanafanyikaga wakati wa kumuandika mwanafunzi mwanzo kabisa au wakati wa kuhakiki majina kabla ya mtihani
 
Majina mengi uharibikia shule ya msingi, mimi pia ni mhanga wa hilo. Jina langu lilibadilishwa kabisa ikanilazimu baadae kutengeneza tena cheti cha kuzaliwa. Lakini ni wakati huo vyeti hata havikuwa vikizingatiwa wakati wa uandikishaji.

Muwe mnapeleka nakala za vyeti vya kuzaliwa ili majina yafanane.
 
Sijakataa,inawezekana ni tatizo la mzazi ndiyo watueleze ni lini tuende kuhakiki.Maana Wa darasa la tano ambaye alikuwa darasa la nne mwaka Wa jana mwalimu alitaka taarifa nimtumie kwa sms nikatuma.Kisha nikapeleka mwenyewe nakala ya cheti Cha kuzaliwa kesho yake kutokana na kuwa mkubwa wake alipewa jina jingine kabisa lile la mwisho. Bado na yeye jina likakosewa herufi.Huu uzembe Wa mzazi upo kwenye muktadha upi hapo.
 
Majibu ya kuwa jina haliwezi kubadilika sijaota ndivyo walivyonieleza.Pia kuwa labda nibadili cheti Cha kuzaliwa kiendane na jina hilo.Ila walikwepa kusema wao ndio hukosea majina.
Pole sana. Jitahidi kuwasiliana na uongozi wa shule wabadilishe,wakikataa washtaki mamlaka ya juu.
Walimu wengi hasa wa shule za msingi wanabadili majina ya wanafunzi wakati wa kuandikisha.
Mfano mwanafunzi anaitwa fredrick, wao wanaandika furedriki. Au lidya wanaandika lidiya/Ridia etc...sidhani kama ni haki kumbadili mtoto jina bila ridhaa ya mzazi
 
Mdogo wangu yupo kidato Cha Kwanza Sasa

Matokeo ya darasa la Saba yalivyotoka analalamika kabadilishiwa jina

Anaitwa. A.mr,m

Kaandikiwa.. A.m.mr

Nahisi. Itakuja kuwa utata mbeleni
 
Salaam wakuu,

Nimepata shida kwa watoto wangu wawili kubadilishiwa majina.Wa kwanza alifanya mtihani wa darasa la nne mwaka 2020 na mwingine 2022.Nilipata kufahamu tatizo Hilo baada ya matokeo ya darasa la nne.Shule walizosomea majibu yao ni kuwa wao walisajili sawasawa kulingana na vyeti vya kuzaliwa.

Huyu Wa darasa la Saba ameambiwa jina ni hilo hilo atakalo fanyia mtihani wa darasa la Saba mwaka huu.Najiuliza swali mamlaka za elimu zinaweza kumbadilishia jina mwanafunzi?.Tena wananiambia labda nimbadilishie cheti Cha kuzaliwa kiendane na majina hayo mapya. Msaada ndugu zangu niko njia panda juu ya Nini naweza kufanya,

Maana mmoja kapewa jina la mtu mwingine na huyu Wa Darasa la tano sasa hivi ni herufi zimechanganywa hazileti maana kabisa.
Ulizia mkondo wa mahakama jinsi ya kubadili au kurekebisha jina. Naamini kuna njia.
 
Back
Top Bottom