Utofauti wa majina ya vyeti vya kuzaliwa,Taaluma na Nida unaweza kukupelekea kukosa ajira na Hati zako za msingi

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,183
3,547
Hili jambo watu wengi hulichukulia ni la kawaida ila limeumiza watu wengi sana wengine hubakia kutoa machozi

Mwaka 2019 kuna jamaa yangu aliitwa kazini baada ya kufaulu usahili wa utumishi aende kuchukua barua ya kuanza kazi akiwa na vyeti vyake halisi akiwa na documents zake zote jamaa alokwenda na vyeti vyote ila katika ukaguzi walivyogundua herufi moja imekosewa kwene kitambulisho cha Nida tofauti na cheti cha kuzaliwa akazinguliwa yaani hata alipoulizwa kuhusu affidavity au Deadpool hakuwa navyo finally aliondolewa nafasi yake akapewa mtu mwingine japo alijaribu kubembeleza lile swala analifanyia kazi lakini wapiiii

Hivyo basi wenye majina yenye utata fanyieni kazi hili jambo mtakuja kunishukuru

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
 
Herufi moja tu?

Hatari sana!
Yes kama vyeti vyako vina shida katika majina vifanyie kazi haraka sana hakikisha vitu kama deed Pol au affidavity unakuwa navyo mapema

Kwa mfano mshikaji wangu aliekosa kazi anaitwa jumanne Rashidi cheti cha kuzaliwa ila kitambulisho cha nida ni jumanne Rashid yaani ile herufi i kukosekana imempa shida

Aisee na mimi nina shida hiyo vyeti vya shule na kuzaliwa ni Fikili ila nida wakandika Fikiri,,,,, tatizo tayari hili.

Kuna dogo mmoja anasema yeye jina zima lina utofauti na cheti cha kuzaliwa ameambiwa hatua inayofuata akatangaze gazeti la serikali na gharama elfu 20,,,so serious !!!

Hyo deed pol au affidavity naipataje/wapi ? Mkuu!?

Process zipoje ?
 
Mtu aliandikishwa jina kwenye cheti cha kuzaliwa kuwa Clara Maria Evodia Baba yake anaitwa John Elisante Marealle. Shuleni wakaamua ku drop Evodia, na Elisante na akaitwa Clara Maria John Marealle. Una maanisha majina yote hayo yanapaswa yawepo?
 
Labda nijaribu kukujibu nilivomwelewa mimi.

Issue ni kwamba vyovyote vile majina yalivyo INATAKIWA YAFANANE CHETI CHA KUZALIWA YAWE KAMA YALIVYO KWENYE NIDA NA VYETI VYA SHULE.

Mfn: Jina cheti cha kuzaliwa A B C
Jina NIDA A B C
Jina vyeti vya shule A B C

sio vinginevyo, issue ni majina yafanane kama ilivyo kwenye kila cheti cha kuzaliwa,nida na shule.
 
Hizo nenda mahakamani mimi nilikosewa majina mpaka sasa ,natumia kimeo .

Nilienda pale mahakama ya Magomeni usalama nikampa kama 20k fasta nusu saaa nikapata hati ndo naitumia mpaka leo kuambatanisha na vyeti vyangu ni kitambo sana.
 
Yupo sawa kama lake na baba ake yapo sawa na la ukoo lipo hilo Marealle haina shida sio lazima kuweka la babu.

Mimi natumia jina la ukoo kama la tatu yaani jina la tatu la baba angu lile la pili ( la babu) situmii..Ila yote yanaonekana kweny vyeti ndo uzuri wake
 
Hizo nenda mahakamani mimi nilikosewa majina mpaka sasa ,natumia kimeo .

Nilienda pale mahakama ya Magomeni usalama nikampa kama 20k fasta nusu saaa nikapata hati ndo naitumia mpaka leo kuambatanisha na vyeti vyangu ni kitambo sana.
Kuna jamaa kanambia nende NIDA makao makuu, na barua ya kuomba kubadilisha halafu niambatanishe na vyeti vya shule na cha kuzaliwa wao nida ndo watanibadilishia.
 
Sawa NIDA lakini mfano mimi ilikuwa majanga sana🤣🤣

Cheti za kuzaliwa jina limekosewa, kadi ya kura ipo tofauti ,Cheti za form four &six vipo tofauti kabisa.

Majina ni hivi : Mohamed, Mohammed,Mohamedi unaweza kucheka🤣🤣🤣ila la baba na ukoo lipo sawa

Ilikuwa ishu ya NIDA bado ila ishu ya Nida nilikuwa makini sana kujaza details niliwaletea tabu sana..
 
Mimi nilikua makini sana kwenye Hilo la kwanza na nilikua nahakikisha haliandikwi tofauti kabisa kama Hilo la pili au la tatu na nashkur Mungu nlifanikiwa na yapo sawa kwenye vyeti vyote.

Nilikua nikiona anataka nimtajie namwambia ngoja nikuandikie mwenyewe linavyoandikwa.
 
Sawa NIDA lakini mfano mimi ilikuwa majanga sana

Cheti za kuzaliwa jina limekosewa, kadi ya kura ipo tofauti ,Cheti za form four &six vipo tofauti kabisa.

Majina ni hivi : Mohamed, Mohammed,Mohamedi unaweza kuchekaila la baba na ukoo lipo sawa

Ilikuwa ishu ya NIDA bado ila ishu ya Nida nilikuwa makini sana kujaza details niliwaletea tabu sana..

Mimi shida ipo hapa

Cheti cha kuzaliwa na vyeti vya taaluma ni FIKILI lakini NIDA pekee ni FIKIRI

Hii case si inamalizikia NIDA mkuu au ?
 
Mimi nilikua makini sana kwenye Hilo la kwanza na nilikua nahakikisha haliandikwi tofauti kabisa kama Hilo la pili au la tatu na nashkur Mungu nlifanikiwa na yapo sawa kwenye vyeti vyote.

Nilikua nikiona anataka nimtajie namwambia ngoja nikuandikie mwenyewe linavyoandikwa.
Hapa ulishtuka kishujaa kumuandikia.

Form za NIDA nilijaza vizuri tuu jina: Fikili sasa inaonekana yule mdada alisoma akaacha kuzingatia herufi akajikuta kaandika Fikiri nida namba inatoka ndo nashtuka ila sikujuwa kama inaleta tabu.
 
Labda nijaribu kukujibu nilivomwelewa mimi.

Issue ni kwamba vyovyote vile majina yalivyo INATAKIWA YAFANANE CHETI CHA KUZALIWA YAWE KAMA YALIVYO KWENYE NIDA NA VYETI VYA SHULE.

Mfn: Jina cheti cha kuzaliwa A B C
Jina NIDA A B C
Jina vyeti vya shule A B C

sio vinginevyo, issue ni majina yafanane kama ilivyo kwenye kila cheti cha kuzaliwa,nida na shule.
Sidhani kama ni kweli cheti ya kuzaliwa haina uhusiano wowote na ajira jombaaa,hakuna sehemu utaenda utaombwa cheti ya kuzaliwa ila NIDA fresh,eti mtu anaenda chukua barua ya ajira aombwe cheti ya kuzaliwa?? Hii haijawahi tokea suppose hiyo barua ingekuja kwa njia ya posta nani angekuomba hiyo cheti ya kuzaliwa??
 
Ni kweli herufi huwa ndo zinaleta shida ila majina kuchanganyika huwa haina tatizo kwa mfano chet Cha kuzaliwa unaitwa Isack Idris Isack alaf vyet vya elim na Nida yako ikawa Isack Isack Idris hapo hamna tatizo ilimradi majina yote yawepo

ila ukikutana na mwenye roho mbaya ndo atakusumbua
 
Sidhani kama ni kweli cheti ya kuzaliwa haina uhusiano wowote na ajira jombaaa,hakuna sehemu utaenda utaombwa cheti ya kuzaliwa ila NIDA fresh,eti mtu anaenda chukua barua ya ajira aombwe cheti ya kuzaliwa?? Hii haijawahi tokea suppose hiyo barua ingekuja kwa njia ya posta nani angekuomba hiyo cheti ya kuzaliwa??
Hapa tunazungumzia GOVERNMENT mkuu, kuhusu taasisi binafsi hawanaga hizo!

Nenda UTUMISHI na hizo majina zimejichenga hivo hutoboi, cheti cha kuzaliwa gvt ni mandatory.
 
  • Thanks
Reactions: apk
Hili jambo watu wengi hulichukulia ni la kawaida ila limeumiza watu wengi sana wengine hubakia kutoa machozi

Mwaka 2019 kuna jamaa yangu aliitwa kazini baada ya kufaulu usahili wa utumishi aende kuchukua barua ya kuanza kazi akiwa na vyeti vyake halisi akiwa na documents zake zote jamaa alokwenda na vyeti vyote ila katika ukaguzi walivyogundua herufi moja imekosewa kwene kitambulisho cha Nida tofauti na cheti cha kuzaliwa akazinguliwa yaani hata alipoulizwa kuhusu affidavity au Deadpool hakuwa navyo finally aliondolewa nafasi yake akapewa mtu mwingine japo alijaribu kubembeleza lile swala analifanyia kazi lakini wapiiii

Hivyo basi wenye majina yenye utata fanyieni kazi hili jambo mtakuja kunishukuru

Sent from my SM-A037F using JamiiForums mobile app
Hayo waliyo mfanyia ni roho mbaya iliyo pita kiasi,watu wanatumbua kabisa miaka ya nyuma teknolojia yetu ilivyo kuwa na hata wataalamu wetu walivyo kuwa,yani,kitendo cha kukosea herufi ni kugusa tu.
Kitendo kama hicho ni kumkomoa mtu na kumpa mzigo asio stahili,saili zote hizo alizopita hawakuliona hilo leo uje umnyime mtu barua ya ajira kisa herufu moja na ukizingatia tabu zote za saili alizo pitia!

Huyo mhanga kama yupo mwambie mimi nipo tayari kujitolea dumu la petrol akawashughurikie mahayawani hao wasio jali mahangaiko ya tabu wanao pata vijana wasio na ajira.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom