Kulingana na kitabu The Journey of man. Ancestor wa binadamu aliishi misitu ya Afrika ya kati. Alikuwa kama sokwe(akiwa mweupe na mwenye manyoya mengi kama tu sokwe wa leo. Akiishi mitini na kutembea kwa miguu minne). Msituni ni baridi hivyo alihitaji manyonya mengi ya kumkinga. Pia hakuna jua la kutosha hivyo alikuwa mweupe ili kutengeneza vitamin D za kutosha. Watu wa kale zaidi wanaaoonyesha kuwa binadamu alitoka msituni akiwa mweupe ni Wabushmen(Jamii ya kale zaidi duniani). Hawa, tofauti na Waafrika wengi wao ni weupe.
Kama miaka 200K iliyopita akatoka msituni na kuingia nyika za Afrika Mashariki(Kenya,Tz). Huko sababu ya jua kali akatengeneza melanin ili kujilinda dhidi ya hilo jua. Na sababu hakuna miti na alihitaji kuwinda nyikani akaanza kutembea kwa miguu miwili.
Baadae alipoongezeka akaanza kuhama. Njia aliyotumia kuhama ni kuambaa na pwani ya bahari. Pwani ya Tz, Kenya, Somalia, Yemen, Arabia, India, wengine wakavuka kuingia visiwa vya SEA hadi Australia. Hawa walihama zamani na ndiyo unakuta kuanzia India hadi Australia kuna watu weusi. Baadaye wengine wakapita kuelekea Ulaya na Siberia na kutengeneza rangi nyeupe(yaani polepole wenye rangi nyeusi wanakufa sababu kwenye mazingira ya baridi hawawezi tengeneza vitamin D na wale wenye weupe kidogo wanasurvive hadi mwisho wanabaki weupe watupu.) Baadaye kutoka Siberia wakashuka Tena kuingia China, Asia ya kati hadi Japan. Sababu ya kupigwa na mwanga unaoakisiwa kwenye barafu huko wakatokeza macho ya kujifinya. Ndiyo maana Wachina na Waeskimo(Inuits) wana macho ya kujifinya. Wote asili yao ni huko kaskazini kwenye barafu.
Jamii hii hii baadaye ikavuka mlango bahari wa Bering na kuingia bara la Amerika(wakati wa baridi bahari huganda mtu huweza kuvuka kwa kutembea). Huko walisambaa kutoka Amerika kaskazini hadi kusini. Ndiyo wahindi wekundu. Study za DNA zinaonyesha kuna uhusiano wa karibu sana kati ya wahindi wekundu na watu wa Asia Mashariki kama Wachina na Wajapan, ni watu wale wale walioamua kuvuka bahari kwenda Amerika.
Afrika kuna watu wa kila aina sababu ndiyo asili ya binadamu, hivyo waafrika wana vinasaba vya kutoa watu wa aina mbalimbali. Watu wenye vinasaba vichache zaidi ni wale wa asili ya Amerika.