Tofauti ya makaburi ya viongozi na ya watawala

Tofauti ya makaburi ya viongozi na ya watawala

mulaga

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2019
Posts
3,153
Reaction score
2,914
Hapa ni tofauti ya makaburi ya watu waliowatawala watu wao na kuwaachia umasikini wa kutupa pia na viongozi waliotumikia vyema watu wao.
 

Attachments

  • Tombeau_Bokassa_Berengo.jpg
    Tombeau_Bokassa_Berengo.jpg
    7.6 KB · Views: 45
  • FB_IMG_1568892941220.jpg
    FB_IMG_1568892941220.jpg
    33.2 KB · Views: 40
  • FB_IMG_1568892922925.jpg
    FB_IMG_1568892922925.jpg
    51.7 KB · Views: 45
  • FB_IMG_1568892932370.jpg
    FB_IMG_1568892932370.jpg
    37.6 KB · Views: 48
  • FB_IMG_1568892915972.jpg
    FB_IMG_1568892915972.jpg
    22.3 KB · Views: 47
  • FB_IMG_1568892907064.jpg
    FB_IMG_1568892907064.jpg
    33.1 KB · Views: 39
  • FB_IMG_1568892898846.jpg
    FB_IMG_1568892898846.jpg
    31.7 KB · Views: 51
  • FB_IMG_1568892814975.jpg
    FB_IMG_1568892814975.jpg
    23.8 KB · Views: 48
  • FB_IMG_1568892866066.jpg
    FB_IMG_1568892866066.jpg
    17 KB · Views: 44
Hapa ni tofauti ya makaburi ya watu waliowatawala watu wao na kuwaachia umasikini wa kutupa pia na viongozi waliotumikia vyema watu wao.
Dah Afrika Nani katuroga? Yaani nimepata somo kubwa Sana....i.e leadership vs Administrators!
 
Iungwe Kwenye Thread Kuu Iliyoanzishwa Muda Wa Siku Kadhaa Na Member Mshana Jr
 
Kaburi utadhani jengo la historia au hoteli wakati kifo ni kimoja
Interesting!
 
Weka la Nyerere au hata Sokoine halafu uweke na la Karume tuone.

Mambo mengine yanatofautiana sababu ya tamaduni moja na nyingine toka enzi za uchifu kuna jamii zilijengea makaburi refer pyramids.

Hata Mwakitolio kuna makaburi yamenakishiwa kuliko hilo la Bush na ni ya peasants tu.
 
Gharama za kodi za wananchi zilizotumika kuyajenga hayo mahekalu ya makaburi yasiyokuwa na maana Kwa kizazi cha sasa zaidi ya historia heri zingetumika kujenga vyuo,shule,au library,visima vya MAJI,kuwasaidia wananchi.
Yalijengwa mapiramidi sembuse kaburi la Kenyatta? Embu tushughilikie issues
 
Wangezikwa kaburi la hovyo ungesikia "wamemtupa tu Rais wao, hakuheshimiwa kabisa"

Linalosema haya ndilo hilo hilo linalosafirisha marehemu toka Dar to Kigoma wakati huyo aliyekufa angeweza kuzikwa popote ili kuondoa gharama za kusafirisha.

Kwa unafiki blacks tunaongoza.
 
Structure ya hayo makaburi inadhihirisha kumbukumbu and how grateful we are to our founding fathers.

Hilo kaburi la George Bush ni halali kua hivyo sababu hakua distinct figure kati ya marais waliopita marekani, kwahiyo usili pimanishe na makaburi ya watu kama Nkurumah, Samora Machel na Kenyatta watu ambao walio komboa nchi zao toka kwa wakoloni.

Ku praise watawala kupitia makaburi sio swala la Waafrika tu, ni dunia nzima.

Jaribu kuangalia kaburi la Abraham Lincoln raisi wa 16 wa marekani, fuatialia urusi mwili wa Lenin mwasisi wa USSR bado unatunzwa mpaka leo for exhibition, ingawaje una gharimu mamilioni ya dola za matunzo.

Waafrika tuachane na ideology ya ku criticize kila kitu tufanyacho.
 
Naona hata dhamira zinakusuta mleta hoja ndo maana hujathubutu kuliweka la huyo wa kwako. Mnataka kuonesha nyie mko poa sana. Fikiria; mwanamke kafiwa na mume wake, tena bado kijana tu miaka 43. Kaachiwa watoto 6, hana kazi ya kuajiriwa, hawajajenga nyumba kwao. Mnachanga mamilioni ya fedha za kumsafirisha maiti hadi kwao let's say Bukoba, Mbeya, Arusha or Musoma kutoka dar. Mnatumia mamilioni halafu mnafika pale mnakaa siku 6 mkila rambirambi. Siku ya kuondoka mnamwacha huyo mjane huko kijijini kwa wakwe. Mjane sio wa huko na mlichomwachia ni shs 100,000/=. What a shame?? Mlichanga 6m mmezila zote mnamwacha na msongo wa mawazo.
Mwafrika nadhani amelogwa
 
Back
Top Bottom