Tofauti Kati ya Mwanangu na Binti Yangu

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,145
13,216
Haya maneno yamekuwa yakitumika vibaya,mtu anasema mwanangu kumbe anamaanisha msichana...mwanagu (my son) ni shuruti awe mvulana, binti yangu (my daughter) nimsichana, na haiwezekani ukajumuisha wote yani watoto wa jinsike na jisime ukawaita wanangu, jamani tusaidieni kunyoosha wenzetu
 
Mwana ni neno la Kibantu, na linamaanisha mtoto (awe wa Kiume ama Kike)

Mwana-Shona (Mwana-mutapa)
Ng'wana- Kisukuma
Muana-Lingala
 
Mwana linamaana ya mtoto, haijalishi kama ni wa kiume au wa kike.

Kamusi la Kiswahili linaainisha hivyo.

Kimsingi mwana linahistoria ndefu ya kutumika kwenye majina ya watoto wa kike kama Mwanaasha, Mwanamtama,Mwanakheri,Mwanaidi, Mwantatu, na kadhalika na kadhalika
 
mwana maana yake ni mtoto wa. kama vile mwana adamu, mwanamke, mwanamume nakadhalika kwa hivyo unaposema mwanangu unamaanisha mtoto wangu, wakike binti yangu au wa kiume kijana wangu...vile vile kijana pia hutumika kwa watoto ambao hawaja baleghe mfano kijana kike au kijana dume
 
Mwanangu haijaliashi ni wa kiume au wa kike
Na binti ni wazi mtoto wa kike
 
Back
Top Bottom